mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,251
Nimeshangazwa Na kauli ya Msemaji wa CCM Bw.Olesendeka Jana alipokuwa anawahutubia wananchi wa Kilimanjaro eti CCM itawaletea Maendeleo ya haraka watoke vyama vya upinzani.Ina maana wananchi waliopo ndani ya CCM wana maendeleo? Mbona ni masikini wa kutupwa hata mlo wao wa siku unasumbua?CCM kuanzia TANU IPO madarakani Kwa zaidi ya miaka 50 lakini hali za maisha ya watanzania zinazidi kuwa duni licha ya nchi kuwa Na Rasilimali nyingi badala yake viongozi wa CCM Na Serikali akiwemo Bw.Ole Sendeka ni matajiri wa kutupwa .Tunawaomba viongozi wetu waacha kauli za kuwadhihaki watanzania eti wakijiunga na CCM watapata maendeleo hakuna lolote wataishia kupewa T' Shirt Na Vitamba vya kichwani Na Kofia hayo ndio Maendeleo ndani ya CCM.