• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

CCM kukata rufaa kwenye majimbo 4, yalaani Wafuasi wa UKAWA kuchoma moto ofisi za CCM

TandaleOne

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Messages
1,622
Points
1,250
TandaleOne

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2010
1,622 1,250
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wana-CCM na kwa umma:

MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO

Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo, uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi. Majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe. Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi. Kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. Kwa msingi huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya. Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa. Bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura. Hata hivyo, tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge, tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi, na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na kuyarekebisha.

MAONI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI

CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi. Tumefarijika kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa wa haki na huru, uliofanyika kwa uwazi na kwa amani ? na kwamba changamoto zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa. Tumepokea mapendekezo waliyoyatoa kwa wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha mchakato wa uchaguzi kwa miaka ijayo, na hivyo kuimarisha demokrasia nchini mwetu. Kwa kauli za waangalizi hawa, kwamba, kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, matokeo yanayotangazwa sasa ni kielelezo sahihi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka.

MALALAMIKO YA UKAWA

Tumesikia malalamiko ya viongozi wa UKAWA kupitia mkutano wao na waandishi wa habari jana. Tumeshangazwa na kauli kwamba hawakubali matokeo ya Urais yanayotangazwa na Tume. Hata hivyo, matokeo ya Ubunge wanayakubali na, kule wanakoshinda, wanayasheherekea. Tunashangazwa kwasababu Tume iliyoandaa uchaguzi wa Rais ni hiyo hiyo iliyoandaa uchaguzi wa Wabunge, wasimamizi ni walewale, vituo ni vilevile, na sheria na taratibu zilizotumika ni zilezile. Hata fomu ya matokeo walizosaini wakala wao kwenye vituo vya kupiga kura, zimegawanywa katika sehemu (columns) tatu: Urais, Ubunge na Udiwani. Mawakala wao walisaini fomu hizo kwenye vituo vya kupiga kura. Wameanza kuwa na matatizo na matokeo haya baada ya kuona mwelekeo wa kushindwa. Kama mwelekeo ungekuwa tofauti, wangekuwa na imani na Tume, wasimamizi na taratibu zote.

Tunaomba ifike pahala sasa kwamba, katika kuijenga demokrasia yetu na kuliimarisha taifa letu, tuanze utamaduni mpya wa anayeshindwa kunyanyua simu kumpigia anayeshinda na kumpongeza. Nafasi ya mwisho aliyonayo Mgombea wa UKAWA kuendelea kujijengea heshima katika jamii yetu, na kuwa mwanademokrasia, ni kwa kufanya hivyo siku Dkt. Magufuli atakapotangazwa mshindi.

Kwetu sisi CCM, kuchagua wagombea bora na kuwanadi na kutengeneza sera bora na kuzinadi, pamoja na rekodi yetu katika uongozi wa nchi, ndio njia zetu pekee za ushawishi. Katika uchaguzi huu, wananchi wamefanya maamuzi yao kwa uhuru na utashi, ikiwemo kuwaangusha mawaziri sita ambao tuliwasimamisha kama wagombea wetu katika majimbo mbalimbali. Nguvu na utashi wa wananchi umejidhihirisha katika uchaguzi huu.

Mchakato wa uchaguzi sasa unakaribia kufikia ukingoni, tutawapata madiwani, wabunge na Rais, tunapaswa kuendelea na maisha na tuwape nafasi watutumikie. Jitihada tunazoziona sasa za viongozi wa UKAWA za kuendeleza siasa za uchaguzi kwenye mitaa ya miji yetu kwa njia za vurugu na maandamano hazikubaliki hata kidogo.

Tunalaani kitendo cha wafuasi wa UKAWA kuchoma ofisi za CCM katika Wilaya ya Mbozi. Amani ya nchi hii ina thamani kuliko hitaji la madaraka la mtu yoyote. Wenzetu wa UKAWA wana haki ya kulalamika lakini hawana haki ya kuiingiza nchi yetu machafukoni kwa kuwakusanya vijana na kuwaingiza mitaani wafanye vurugu na kuhatarisha maisha, kuharibu mali na kusimamisha shughuli za watu wengine. Tunawaomba Watanzania waendelee na shughuli zao kama kawaida huku kila mmoja akitambua wajibu wake wa kuilinda amani ya nchi yetu.

January Makamba
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
28.10.2015
 
fundi25

fundi25

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Messages
7,759
Points
2,000
fundi25

fundi25

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2013
7,759 2,000
wata ambulia aibu kubwa kuliko
 
mcubic

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Messages
10,251
Points
2,000
mcubic

mcubic

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2011
10,251 2,000
Mbowe anawatumia vijana vibaya
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
45,189
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
45,189 2,000
CCM andaeni pesa za kulipia gharama za kesi.
 
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2011
Messages
27,871
Points
2,000
OKW BOBAN SUNZU

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2011
27,871 2,000
Sisi tunakata yote mpaka uliloshinda wewe.na hao mliowaficha Mlimani city yatawakuta tu
 
L

liwamba

Senior Member
Joined
Nov 20, 2012
Messages
144
Points
170
L

liwamba

Senior Member
Joined Nov 20, 2012
144 170
uwaziri mkuu unatafutwa kwa kila njia
 
G

goodluck5

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Messages
3,417
Points
2,000
G

goodluck5

JF-Expert Member
Joined Jan 8, 2014
3,417 2,000
Huyo bebwa bebwa simshangai, anaasili ya unafki kutokana na jamii anayotoka!
 
pipikali

pipikali

Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
43
Points
70
pipikali

pipikali

Member
Joined Oct 4, 2007
43 70
Hivi wale waliomfungulia Lema kesi waliwahi kulipa gharama za kesi?. Vipi wale wa Tundu Lissu
 
anonymous x

anonymous x

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
1,751
Points
2,000
anonymous x

anonymous x

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
1,751 2,000
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM inapenda kutoa taarifa ifuatayo kwa wana-CCM na kwa umma:

MALALAMIKO YA CCM KUHUSU MATOKEO KWENYE BAADHI YA MAJIMBO

Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo manne kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utaratibu wa uchaguzi, hasa katika kujumlisha matokeo, uliopelekea wabunge wa upinzani kutangazwa washindi. Majimbo hayo ni Iringa Mjini, Mikumi, Ndanda na Kawe. Wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo haya wamevuruga uchaguzi. Kutokana na utata uliokuwa umejitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura, CCM iliomba kura zihesabiwe upya lakini ikanyimwa haki hiyo ya msingi ambayo iko kwenye sheria. Kwenye baadhi ya majimbo, ikiwemo Nyamagana, wapinzani walipewa haki ya kura kuhesabiwa upya. Kwa msingi huo, CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya. Tunataka sote tujiridhishe kwamba utashi wa wananchi umeheshimiwa. Bado tunaendelea kukusanya taarifa za maeneo mengine kama kulikuwa na ukiukwaji mkubwa uliobadilisha matakwa ya wapiga kura. Hata hivyo, tunakiri kwamba kwenye maeneo mengi tulikopoteza viti vya Ubunge, tumepoteza kihalali, hatuna malalamiko, tunaheshimu maamuzi ya wananchi, na tutafanya tathmini baada ya uchaguzi ili tubaini makosa na kuyarekebisha.

MAONI YA WAANGALIZI WA UCHAGUZI

CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi. Tumefarijika kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa wa haki na huru, uliofanyika kwa uwazi na kwa amani ? na kwamba changamoto zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa. Tumepokea mapendekezo waliyoyatoa kwa wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuboresha mchakato wa uchaguzi kwa miaka ijayo, na hivyo kuimarisha demokrasia nchini mwetu. Kwa kauli za waangalizi hawa, kwamba, kwa jinsi uchaguzi ulivyoendeshwa, matokeo yanayotangazwa sasa ni kielelezo sahihi cha utashi wa Watanzania kuhusu viongozi wanaowataka.

MALALAMIKO YA UKAWA

Tumesikia malalamiko ya viongozi wa UKAWA kupitia mkutano wao na waandishi wa habari jana. Tumeshangazwa na kauli kwamba hawakubali matokeo ya Urais yanayotangazwa na Tume. Hata hivyo, matokeo ya Ubunge wanayakubali na, kule wanakoshinda, wanayasheherekea. Tunashangazwa kwasababu Tume iliyoandaa uchaguzi wa Rais ni hiyo hiyo iliyoandaa uchaguzi wa Wabunge, wasimamizi ni walewale, vituo ni vilevile, na sheria na taratibu zilizotumika ni zilezile. Hata fomu ya matokeo walizosaini wakala wao kwenye vituo vya kupiga kura, zimegawanywa katika sehemu (columns) tatu: Urais, Ubunge na Udiwani. Mawakala wao walisaini fomu hizo kwenye vituo vya kupiga kura. Wameanza kuwa na matatizo na matokeo haya baada ya kuona mwelekeo wa kushindwa. Kama mwelekeo ungekuwa tofauti, wangekuwa na imani na Tume, wasimamizi na taratibu zote.

Tunaomba ifike pahala sasa kwamba, katika kuijenga demokrasia yetu na kuliimarisha taifa letu, tuanze utamaduni mpya wa anayeshindwa kunyanyua simu kumpigia anayeshinda na kumpongeza. Nafasi ya mwisho aliyonayo Mgombea wa UKAWA kuendelea kujijengea heshima katika jamii yetu, na kuwa mwanademokrasia, ni kwa kufanya hivyo siku Dkt. Magufuli atakapotangazwa mshindi.

Kwetu sisi CCM, kuchagua wagombea bora na kuwanadi na kutengeneza sera bora na kuzinadi, pamoja na rekodi yetu katika uongozi wa nchi, ndio njia zetu pekee za ushawishi. Katika uchaguzi huu, wananchi wamefanya maamuzi yao kwa uhuru na utashi, ikiwemo kuwaangusha mawaziri sita ambao tuliwasimamisha kama wagombea wetu katika majimbo mbalimbali. Nguvu na utashi wa wananchi umejidhihirisha katika uchaguzi huu.

Mchakato wa uchaguzi sasa unakaribia kufikia ukingoni, tutawapata madiwani, wabunge na Rais, tunapaswa kuendelea na maisha na tuwape nafasi watutumikie. Jitihada tunazoziona sasa za viongozi wa UKAWA za kuendeleza siasa za uchaguzi kwenye mitaa ya miji yetu kwa njia za vurugu na maandamano hazikubaliki hata kidogo.

Tunalaani kitendo cha wafuasi wa UKAWA kuchoma ofisi za CCM katika Wilaya ya Mbozi. Amani ya nchi hii ina thamani kuliko hitaji la madaraka la mtu yoyote. Wenzetu wa UKAWA wana haki ya kulalamika lakini hawana haki ya kuiingiza nchi yetu machafukoni kwa kuwakusanya vijana na kuwaingiza mitaani wafanye vurugu na kuhatarisha maisha, kuharibu mali na kusimamisha shughuli za watu wengine. Tunawaomba Watanzania waendelee na shughuli zao kama kawaida huku kila mmoja akitambua wajibu wake wa kuilinda amani ya nchi yetu.

January Makamba
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
28.10.2015

Sasa mbona kule Zanzibar Mwenyekiti wa Tume kasema Uchaguzi haukuwa huru na haki!
 
V

victor kay

Member
Joined
Sep 21, 2015
Messages
45
Points
0
V

victor kay

Member
Joined Sep 21, 2015
45 0
ulimsikia mbowe akiwaambia nendeni wanadai haki yao wenyewe sasa hilo nalo ni la kujiuliza jitambue m tz
 
TandaleOne

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Messages
1,622
Points
1,250
TandaleOne

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2010
1,622 1,250
Sasa mbona kule Zanzibar Mwenyekiti wa Tume kasema Uchaguzi haukuwa huru na haki!
Yanayohusu NEC ama ZEC nenda ukaulize kwa msemaji wa NEC na ZEC mimi sio msemaji wao, hivyo nasikitika kuwa sintoweza kukusaidia chochote katika swali lako kuhusu Mwenyekiti wa Tume kutoa kauli hiyo. Linalohusu CCM, wagombea wake na ofisi zake unakaribishwa.
 
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Messages
12,343
Points
2,000
Faru Kabula

Faru Kabula

JF-Expert Member
Joined Mar 26, 2009
12,343 2,000
Chama cha Mapinduzi hakijaridhishwa na utaratibu wa kukusanya na kujumlisha matokeo kwenye baadhi ya majimbo. ...CCM imeamua kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo haya.

CCM imepokea maoni ya awali ya waangalizi wa uchaguzi. Tumefarijika kwamba karibu wote wametoa kauli ya pamoja kwamba uchaguzi huu ulikuwa wa haki na huru, uliofanyika kwa uwazi na kwa amani ? na kwamba changamoto zilizojitokeza ni ndogo na zimetokea katika maeneo machache kiasi zisingeweza kubadilisha matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa sasa.
Kauli zinapogongana huwa nampuuza mtoa kauli hizo
 
anonymous x

anonymous x

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
1,751
Points
2,000
anonymous x

anonymous x

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
1,751 2,000
Yanayohusu NEC ama ZEC nenda ukaulize kwa msemaji wa NEC na ZEC mimi sio msemaji wao, hivyo nasikitika kuwa sintoweza kukusaidia chochote katika swali lako kuhusu Mwenyekiti wa Tume kutoa kauli hiyo. Linalohusu CCM, wagombea wake na ofisi zake unakaribishwa.Oooh Mkuu kumbe ni wewe uliekuwa unasafirisha yale 'mahindi' kule wilayani?
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
47,307
Points
2,000
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
47,307 2,000
Sasa hivi kila mtu anasema lake.

Nchi imekosa mwelekeo.

CCM haiwezi kutoka madarakani kwa makaratasi.
 
J

Juliana Shonza

Verified Member
Joined
Dec 19, 2012
Messages
2,009
Points
2,000
J

Juliana Shonza

Verified Member
Joined Dec 19, 2012
2,009 2,000
Taarifa muhimu lakini hili suala la Zanzibar lina mkanganyiko mkubwa sana...nadhani viongozi wa Chama wanapaswa kutoa neno.
 
Forum statistics

Threads 1,404,200
Members 531,529
Posts 34,447,091
Top