Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Demokrasia kamili na uhuru katika hatua yake ya juu kabisa, vinafanya kazi kwa ufanisi katika jamii yenye kiwango cha juu sana cha kujitambua, ustaarabu, kuweza kuchanganua mambo na kuamua kwa busara. Ikiwa jamii ina kiwango cha chini cha tabia tajwa hapo juu, kwa kadiri kiwango cha demokrasia na uhuru wa watu kinavyoongezeka, ndio hatari ya kutokea majanga inavyoongezeka na kinyume chake. Hili tutalifafanua zaidi baadae.
Kwa bahati mbaya ni kwamba Afrika bado tupo watu wengi sana/wapiga kura ambao uelewa wetu juu ya mambo na uwezo wetu wa kuchanganua vitu na kufanya maamuzi sahihi ni mdogo. Kwa mfano, % kubwa ya watanzania hatuelewi falsafa, itikadi, misingi na sera ya vyama achilia mbali kuzifuata. Jiulize mfano ukisema chama cha mrengo wa kushoto, mrengo wa kati kushoto, mrengo wa kulia ujamaa wa kidemokrasia na vitu kama hivyo, ni watanzania wangapi wanaelewa unasema nini?
Wapiga kura wengi Afrika amma hupiga kura bila kujua nini wanafanya, au baada ya kuchanganywa ‘Manipulations’ au kwa mihemko ‘emotions’au kwa ushabiki usiokuwa na sababu za kueleweka. Ili hili lieleweke vizuri, nitatoa mifano michache.
Moja, Ushawahi kuona bungeni kwa mfano, mtu anatoa hoja nzuri sana, lakini wajumbe wakiulizwa ‘Mnaikubali hiyo hoja’ wanasema ‘hapanaaaaaaaa’ lakini sio kwamba hawaitaki hoja, ni kwa sababu ya nani katoa hoja, kwa hiyo wajumbe wakishaona mtoa hoja washaikataa hoja tayari hawana haja hata ya kuielewa kwanza?
Mbili, Unajua tunaweza kwenda wote kwenye uchaguzi, wewe ni muadilifu na unahoja nzuri, mimi nikawa ni mjinga flani tu, ila nikasubiria masaa kadhaa kabla ya uchaguzi nikakuzushia kwamba wewe unauza meno ya tembo huku nimetumbua mimacho kweli kweli, na wapiga kura wakakukataa na kunikubali mimi, kisha baada ya uchaguzi (kukushinda), nikasema nilikuwa natania tu, sijawahi kuuona ukiuza meno?
Tatu, Unajua wapiga kura kwenye nchi za kiafrika wakipewa rushwa humchagua mtoa rushwa na kuacha watu wenye maono?
Nne, Unajua kwa mfano wewe ukipiga kampeni kwa kuongea mambo ya maana mwingine akawa anakatika, una uwezo wa kushindwa uchaguzi, na hata mzee wa mauno alishinda kimzaha hivyo hivyo? N.k
Kwa mantiki hiyo basi;
- Kwa sababu ya uelewa wa waafrika tuliowengi, demokrasia peke yake haiwezi kutusaidia kuwa na nchi zenye ustawi na uongozi bora bali inahitajika mfumo wa ziada kujazia demokrasia ‘Complementary system’
- Kwa kuwa wapiga kura wanaweza kupiga kura kwa kuvurugwa ‘Manipulation’ kura pekee hazituwezeshi kupata viongozi wa maana, Hivyo utaratibu uliowekwa na CCM kuchuja majina kwa kuzingatia vigezo vingine zaidi ya kupigiwa kura sio tu kwamba ni mzuri bali ni muhimu sana kwa ustawi wa Taifa na hatma ya nchi.
- Hoja ya Rais Magufuli kwamba watu ambao tayari wana vyeo vya kutumikia wananchi kama wakuu wa mikoa ni bora wasigombee ubunge, inaegemea kwenye mantiki zaidi kwa kuangalia ‘motive’ na inatokana na ‘complementary system iliyotajwa hapo juu kwa ajili ya maslahi ya Taifa
- Kwa kuwa tatizo la rushwa kwenye uchaguzi bado ni kubwa, kazi anayoifanya polepole kukemea rushwa na kuwatahadharisha watakaotoa rushwa kukatwa majina sio tu kwamba ni nzuri bali pia ni muhimu.