CCM kujivua gamba; (DC Urambo Ana Magoa) sasa hakuna ajira kwa CHADEMA serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kujivua gamba; (DC Urambo Ana Magoa) sasa hakuna ajira kwa CHADEMA serikalini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SUTU BUTUGURI, May 6, 2011.

 1. S

  SUTU BUTUGURI Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilikuwa ni kikao cha KUU (Kamati ya Ulinzi na Usalama) kwa ajili ya kusaili vijana wa kujiunga na JKT.

  Mara akaingia kijana mmoja OFINI KWA DC, Mkuu wa Wilaya ya Urambo kwa kile kilichoonekana kuwa alikuwa ametonywa historia ya kijana SEFU ALI bila shaka na TISS akamuuliza, "Wewe ni mwanachama wa chama gani?" Kijana akajibu "CHADEMA." MAMA ANA MAGOA akasimama na kusema, "Mimi siwezi kuajiri CHADEMA." Wajumbe wa KUU wakasema, "Hizi ni ajira kwa ajili ya Watanzania." MAMA akawa mbogo, "Hakuna ajira kwa CHADEMA." Mmmh.............
   
 2. K

  KIJIGOJUNIOR Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  CCM wanazidi kujipandikizia chuki kwa wananchi wake. Haya anayoyasema huyu ndugu yangu hapa kuhusu kunyimwa ajira kwa kuwa tu muombaji ni Mwana CDM nayo yamemtokea jamaa yangu ambaye yuko kwenye mchakato huohuo wa vijana kuingia JKT.Dogo baada ya kuandika barua yake ya maombi, alikwenda kwa Mtendaji wa Kijiji, kufika huko akaulizwa, "Mjumbe wa eneo unalotoka anaitwa nani tusije tukawa tunaajiri vijana wa Cdm". Hii inasikitisha sana ndugu zangu, yaani kumnyima mtua ajira kwa kuwa tu si mwanachama wa chama unachokifuata wewe? Huu kwanza ni ukiukwaji wa Katiba ya JMT, kwa kuwa kuna ubaguzi wa wazi hapo. Ngoja waendelee kufanya hivyo wazidi kuvimbisha mioyo ya watanzania waliokaribia kujikomboa upya
   
 3. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Uvunjifu wa amani huanza kwa vitu kama hivyo,kubagua watu sio sawa mbona kulipa kodi hawakatai kodi za wana CDM..
  Tutafakari..
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Afadhali hata Mama Magoa kasema live, hiyo ni campaign ya chinichini for YEARS!!!

  Actually hata hamisho za wafanyakazi utaona jinsi targets wako upande gani
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Ndo maana hatuitaji dc's na rc's kuwepo maana hawa wapo kisiasa wanataka hata kwenye ajira serikalini ccm ndo wapewe nafasi,kwa hili dc kavaa gamba,hataweza kuwazuia wote kwa mda wote,kwa mfano mie tayari niko Cdm na tayari niko serikalini na naamini ipo siku serikali itakuwa chini ya Cdm japo sie hatutawabagua maana Cdm kamwe hatulipi baya kwa baya

  lakini ndugu zetu msikate tamaa vumilia miaka3 hamtakufa,hadi 2014 tutakuwa na katiba mpya na hapo mtarudishiwa kila haki yenu mliyoporwa,hata BOT mtafanya kazi ilimradi huwe na sifa muhimu kuondoa ile ya Uccm ama mtoto wa familia flani...msife moyo na ala msijisikie vibaya kuonekana wapinzani kwani mwanzo ni mgumu
   
 6. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  huyo magoa asituletee mambo ya ubaguzi hapa tz. Mambo kama haya yalisababisha genocide rwanda.
   
Loading...