Ccm kujikwaa si kuanguka, waache wapinzani walalame! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm kujikwaa si kuanguka, waache wapinzani walalame!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAFILILI, Apr 30, 2011.

 1. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wandugu, nachukuaa fursa hii kuwafagilia CCM kwa hatua inazochukua ambazo zimeendana na utafiti wa kisayansi. Uamuzi uliochukuliwa White House, Dodoma ulikuwa mgumu hatahivyo wa lazima kuendana na kipindi tulichoko.
  CDM wameropoka sana kuhusu UFISADI ndani ya chama, Uongozi wa Kamanda JK ukawa kimya ukipanga mikakati, hatimaye kikosi kazi cha wasomi waliobea katika masuala ya siasa wakiongozwa na Profesa ukipewa kazi ya kufanya utafiti kwa kuhusisha makundi mbalimbali ya wanachama na watanzania kwa ujumla.
  Data zikakusanywa toka kwa wananchi wakiwemo wana CDM ndipo ripoti ikatoka pamoja na mapendekezo yakawasilishwa CC. Watz inabidi tuwape dole CCM kwa kutambua hali halisi na kuchukua hatua za kuunda kikosi kazi cha wasomi. CDM poleni sana, kwani CCM tatizo limetambuliwa, limefanyiwa kazi na sasa wananchi wamerudisha imani kwa CCM yao.

  CDM utaendelea na kususia vikao vya madiwani, wakati CCM ikichanya mbuga; kaskazini - kusini na mashariki - magharibi.

  CDM tafadhali tumieni nafasi ya CCM kuondoa magamba kama changamoto kubwa kwenu na muanze na sera mpya kama mkiwa na nia ya dhati kuiondoa CCM mtaa wa Magogoni, vinginevyo mtabaki kupambana na vijana wa Saidi Mwema barabarani.

  CCM Oyee na Operesheni Ondoa Magamba; BRAVO kOMREDI MUKAMA
   
 2. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mawazo mfu.
  Mimba si mtoto. Hata si Kila kujamiiana kutokeza mimba.
   
 3. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Upupu.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wewe uko usingizini unaota.ati utafiti wa kitaalamu.ccm wote ni wezi kuanzia juu mpaka chini.sasa tafuteni mbeleko ya kuwabebera hao kina lowasa,rostam na chenge ndipo uje na porojo zako hapa.
  taka usitake ccm ina kansa kuisaidia sio kuvua gamba ni kuikata shingo tu.
  mimi bado nina kadi ya ccm sijairudisha kwani bado nasubiri mazishi nisijeonekana sina fadhila hata kwa mgonjwa mahututi.
  na kama ni dawa basi mgonjwa kapewa dozi na kreti la bia anywe kwa wakati mmoja kinachofuatia watu wazima tunasubiri siku tisini.
   
Loading...