CCM kujenga shule ya uongozi, Julius Nyerere School of Leadership Kibaha

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Comrade Abdulrahman Kinana amesaini mkataba wa ujenzi shule ya viongozi Mjini Luanda, Angola, itakayoitwa Julius Nyerere School of Leadership itakayojengwa Kibaha Mkoani Pwani
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Comrade Abdulrahman Kinana amesaini mkataba wa ujenzi shule ya viongozi Mjini Luanda, Angola, itakayoitwa Julius Nyerere School of Leadership itakayojengwa Kibaha Mkoani Pwani
hizo hela mnazipoteza bure. mgawane za mwisho maana 2020tapotea katika ramani ya Tz
 
Mbona kila kitu Nyerere, kwa nini waasisi wengine majina yao hayatajwi kivile?

Kosa tunalodhani ni kuwa Tanzania au CCM ina waasisi wawili wachache tu, kumbe wapigania uhuru wengine wale, na walioshiriki ktk mchakato wa kuianzisha CCM wote wale ni WAASISI ama wa Tanzania ama CCM, lakini majina yao hayaenziwi kivile.

Mwalimu keshapewa vifuatavyo

1) Ubaba wa Taifa
2) Barabara ya Nyerere
3) Kampasi ya Mwalimu Nyerere
4) Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere
5) Daraja la Mwalimu Nyerere
6) kituo cha mikutano cha kimataifa cha mwalimu Nyerere
7) Chuo cha Kigamboni cha Mwalimu Nyerere

Hivi kweli hakuna wana wengine wa nchi hii walioshiriki kuliasisi Taifa ambao wanastahili majina yao kuenziwa?
 
naona sielewi, wenye chuo ni waangola au ndo partnership nao:eek::eek:
but good thing, vyama vya upinzani muhimu kuiga vitu kama hivi, vijana wadogo wakuzwe kwenye falsafa za chama toka wakiwa wabichi
 
Back
Top Bottom