CCM kuhatarisha uhuru wa chama kwa kutegemea wafadhili matajiri ni kusaliti wananchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kuhatarisha uhuru wa chama kwa kutegemea wafadhili matajiri ni kusaliti wananchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chal, Apr 10, 2011.

 1. C

  Chal Senior Member

  #1
  Apr 10, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wakuu,
  Taarifa zilizotufikia humu jamvini ni JK (mwenyekiti wa CCM) Kulalamika kuwa CCM kuendelea kutegemea wafadhili matajiri ni kuhatarisha uhuru wa chama. Maswali ya kujiuliza hapa ni kuwa,
  1. CCM kama chama kinachounda serikali kimelinda maslahi mangapi ya hawa matajiri kwa kukosa kwao uhuru?
  2. Je, CCM ilikuwa wapi siku zote mpaka leo ndiyo iamke usingizini na kujua hai
  3. Kimya hiki cha CCM kilichosababisha matajiri kupoka uhuru wa chama na kuzidi kujinufaisha si usaliti kwa wananchi masikini?
   
 2. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ndo leo wamegundua? na bado.
   
 3. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ukitaka kujua ukubwa wa tatizo la CCM kuwaachia matajiri chama tembelea Mikoani,uwezi kuamini kuna miungu watu huko si kidogo.Uliza wametoa wapi madaraka [Power] jibu wao ndio wafadhili wakuu wa chama.
  Sipati Picha CCM viongozi wake walikua wanafikiri nini?Nani asiyejua dhamira za tajiri hata katika picha ya kawaida.Japo si matajiri wote lakiini kwa hili la nchi yetu ni la aina yake.

  Matajiri walipo ingia kwenye chama kama wafadhili walianza kuchua madaraka,wengine wakawa madiwani, wenyeviti, makatibu,makamanda,wajumbe wa halmashauri, wengine wabunge wa vikao muhimu vya chama vya maamuzi.
  Ni wazi CCM ni chama chenye alama zinazowakilisha nembo ya wakulima na wafanyakazi, lakini ukitizama viongozi wakuu wengi kuanzia level ya mtaa,shina, tawi, wilaya mkoa na mpaka Taifa, baadhi ni matajiri kuanzia ngazi hizo tajwa.Wengine wamekwea na kuwekwa na matajiri kwa nia ya kuwalinda,haswa wale muonekano wa kuwa ma-alwatan.

  Ni bomu tena lenye mlipuko mkubwa na wenye kishindo, si amini CCM kama chama cha ukombozi kinawezekana kuishi kwa kutegemea nguvu na ufadhiri wa Pesa za wafanyabiashara wengi ambao historia ya upatikanaji wa Pesa yao unatia shaka na unadosari kubwa mbele ya uso wa wananchi.

  Japo CCM kingeweza kuchangiwa na wanachama wake ambao ndani yake wapo matajiri pia lakini matajiri wanaotakiwa kuchangia chama lazima wawe ni matajiri wasiotiwa shaka na jamii na pia si sehemu ya watawala ama watendaji ndani ya chama na ndani ya serikali na katika utaratibu wa wazi.

  Matajiri wengi walioingia kwenye kukifadhili chama ndio waliokiingiza chama kwenye michakato hatari na kutoa picha tofauti ambayo chama cha mapinduzi leo hii imekuwa mwathirika wa hayo.CCM ndio kilikua chama cha kutetea wanyonge leo hii imekua viceversa kimbilio la matajiri .

  Inauma pale ambapo chama chenye mwelekeo na mwasisi wa kutetea wanyonge KIITIKADI kinapotekwa na KUTENDA [Realitity] matendo ya Kibepari [Kitajiri].Matumaini ya watanzania waliowengi yalikua kutetewa na kulindiwa masilahi yao kupitia chama cha mapinduzi.Lakini leo hii vyama vyenye mrengo tofauti na chama husika KIITIKADI vimekuwa watetezi wa wawanyonge hao.

  Ili CCM ivuke na kuludi kwenye kuipriment ITIKADI YAKE ni vyema ikaanzia kujisafisha kwa kuondoa Matajiri Viongozi na Ma-Alwatan,na kuingiza safu ya viongozi wanaokubalika kwenye jamii na kama ni mfanyabiashara basi rekodi yake kwenye jamii aina utata na anasifa njema na yuko tayari kusema mali yake kaipataje.Usafi huo uanzie ngazi ya Mtaa,Shina mapaka Taifa.

  Umefika wakati wateule wa kugombea nafasi za uongozi wachagulie kwa uwezo wao [Content/character] na sio uwezo wa kifedha muhusika alionao.Hapo chama kitakua kimepata viongozi wa hatma ya uhai na uwepo wake haswa kwenye kipindi hiki chama kinaitaji vijana [Modern Youth] wenye upeo wa kuona mbali wenye uwezo wa kuyaona maitaji ya wananchi na kuyafanyia kazi kichama kwa haraka na kwa kasi kubwa ili kimudu kusimama kama chaguo la wananchi kipindi cha uchaguzi.

  Vyama vya upinzani vipo kuakikisha makosa ya chama cha mapinduzi ndio tiketi ya kuwaingiza madarakani ilo li wazi, ingawa kizazi cha viongozi wengi wa CCM hawataki kulitambua hilo na kuviona vyama vya upinzani kama maadui wa nchi,kumbe wote ni wajenzi wa Taifa kupitia Fito [ITIKADI] tofauti.

  Ni Jukumu pia la CCM KUJIVUA GAMBA [REJUVINATES] kujiweka katika kipindi na zama za kisasa.Kujiondoa kwenye misemo na matendo yenye mwelekeo na tafsiri mbaya kwenye jamii kama
  1: MWENZETU AU NDUGU YETU [Hii katika Picha ya kawaida ni kuonyesha mhusika ni tofauti na wadau wengine katika jumuhiya husika].Kujitoa kwenye dhama za sisi ni sisi na wao ni wao, si wenzetu.
  2: NYIMBO ZA VIJEMBE [Mfano Wimbo huu.....wapinzani tuwachanechane tuwatupe....] nyimbo zenye mwelekeo wa kishari wakati itikadi ya chama ni kubebe jahazi la wakulima na wafanyakazi.Ndani ya vyama vya upinzani kuna wakulima na wafanyakazi ambao chama ndio nguzo yao.
  3: Kubeba picha ya utaifa na si picha ya kundi la watu wenye lengo fulani.
  4: Kukubali pia jamii ya watanzania imebadilika haswa vijana, ufahamu wa wanatanzania umebadilika tofauti na miaka ya nyuma.
  5: Kuheshimu vyama vingine, na kukubali kuwa upinzani ni sehemu ya mchakato mzima wa ujenzi wa Taifa kidemokrasia.Uwanja wa Demokrasia lazima uwekwe kwa ajili ya ujenzi wa misingi ya utawala bora.
  6: Uwajibikaji wa viongozi wa chama ngazi zote, kuleta tafsiri kiongozi ni kwa ajili ya wananchi [Wanachama] na uongozi si siraha dhidi ya wananchi [wanachama].Kuepuka upatikanaji wa viongozi kwa njia ya Pesa.
  7:Kujipanga na kutayarisha mikakati na mipango ya kichama [Vision and Plan] ya muda mrefu kwa ajiri ya makundi yote katika jamii huku chama kikizingatia ukweli na si mapenzi ya viongozi na wadau wa chama.Vision na plan za chama zenye kubeba uzito wa makundi ya jamii kuanzia miaka 5-10 10-20 15-25, na yenye kutekelezeka.
  8: Kuwa na taasisi za kisasa zenye kuendeshwa kisomi, mfano taasisi ya Propaganda, ni taasisi muhimu zama hizi, si taasisi tena ya kupiga porojo bali kujua ukweli [facts] na kutumia ukweli huo kuwakilisha maahitaji ya jamii,ukizingatia mahitaji ya jamii, wakati husika na mazingira mengine muhimu.
  9: Chama cha Mapinduzi kiludi kwa walengwa wake yaani wadau wake WAKULIMA NA WAFANYAKAZI kuanzia level ya chini mpaka Taifa.

  10: Enzi za Chama kushika hatamu [Where power SHOULD reside in the system and how SHOULD power be EXERCISED?] ni swala la watanzania wote si swala la CCM peke yake tena.Zama/Enzi ya CCM kuamua kwa niaba ya watanzania zimekwisha, bali chama kujitambua kuwa kinajukumu la kufundishana kuonyesha watanzania kuwa wao ni bora katika kusimamia nafasi ya kuexercised Power katika kuwaletea Maendeleo na Ustawi wao, na SI KUMILKI POWER.

  CCM mpya ni ile itakayotambua MADALAKA NI MALI YA UMMA [WATANZANIA] na siMALI YA CHAMA CHA MAPINDUZI.Kulitambua ilo CCM na kulifanyia kazi CCM itapata nafasi nyingine ya kuwatumikia wananchi.vinginevyo itajiunga na KANU na vyama vingine vilivyopoteza jukumu la kuexercise POWER.Na hivyo kupoteza heshima yote iliyotafutwa na waasisi wa CCM.

  CHAMA CHA MAPINDUZI KITAMBUE WAFANYABIASHARA NDIO WALIOKIFIKISHA HAPO KILIPOFIKA KWA KUACHA MISINGI YAKE MIKUU YA KUJALI MASLAHI YA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI,NA MADARAKA YA NCHI NI MALI YA WATANZANIA WOTE NA HAYANA KIKUNDI CHA WATU [CCM].

  Mifumo ya uendeshaji wa chama ni sehemu ya mafunzo ya ITIKADI ya baadhi ya nchi ambazo walikua marafiki wa nchi yetu miaka ya VITA BARIDI [COLD WAR-EAST AND WEST]. Leo hii mifumo ya utendaji ule hauna tena nguvu [POWER]. [The Party State system is one where the party as such is the respiratory of the wisdom].Dunia imekua kijiji mfumo ya chama kuamua dhidi ya wananchi jamii bila kuwashirikisha kupata maoni yao jamii imeona kuwa ni mifumo kandamizi hivyo jamii imejitoa dhidi mifumo ya aina hiyo. Ukitaka kipimo tizama nchi za kiarabu na mabadiliko yanayoendelea kwenye UMMA kuchukua madaraka toka mikononi mwa watawala.

  Naamini kuna baadhi ya viongozi wanalitambua hilo lakini kuna baadhi wamekua ni kikwazo na kuamini katika mifumo hiyo iliyopitwa na wakati.Haswa wazee wenye umri mkubwa ndani ya madaraka ya nchi.Wanaamini wao ndio wenye mamlaka ya kuamua nini kifanyike na kwa manufaa ya nani,na si vinginevyo.Lakini mwitikio wa wananchi dhidi ya matakwa ya viongozi wa aina hiyo ndio umekifikisha chama cha mapinduzi hapo kilipo.Wakati wowote chama hicho chaweza kuwa chama cha upinzani kama tu kitaendelea kukumbatia viongozi wasiomini na kutoa mabadiliko ambayo wananchi wanataka kuyaona yakitendeka katika sura nzima ya UTWALA NA USTAWI WA JAMII NA MAENDELEO YA NCHI NZIMA.
   
Loading...