CCM Kuharibu Uchaguzi 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Kuharibu Uchaguzi 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kamende, Oct 28, 2010.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu habari za jioni

  NInawaletea habari zilizotua kwenye meza yangu kutoka kwenye source ya ndani kabisa ya CCM anayehusishwa mipango muhimu lakini asiyependa kutekelezwa kwa hila hizo za Chama Cha Mafisadi.

  CCM wameorodhesha mikoa ambayo hawawezi kushinda na tayari wamekwishapeleka vijana wa kazi katika mikoa hiyo. Vijana hawa ni wale waliopewa mafunzo kule Iringa na Msinga mkoani Kilimanjaro. Kazi yao ni pamoja na kuingia kwenye vituo vya kupigia kura wakijifanya viongozi wa Tume ya Uchaguzi.

  Mwanzoni watapita wakiuliza hali ya vituo na baadaye watakuja kutoa maagizo vituo hivyo vifungwe kwa sababu mbalimbali. Lengo la magizo haya ni kusababisha fujo ambayo itahalalisha kufungwa kwa vituo ukweli na hivyo kuharibu uchaguzi.

  NIna taarifa kuwa mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Kilimanjaro na Mwanza vijana hawa wamekwisha kufikishwa kwenye wilaya ambazo watafanya kazi. Mathalan katika mkoa wa Kilimanjaro vijana hawa wamekwishawasili katika majimbo ya Rombo, Mshi Mjini, Hai, Siha Same zote na Moshi Vijijini.

  Kama hawatadhibitiwa mapema kwa hakika uchaguzi utaharibika na Kikwete atanusurika kipigo cha aibu.

  Wajameni tutoe habari hii kwa umma ili kuivujisha isitekelezeke.

  CCM!!!
  TUACHIENI AMANI YETU!!!!!!!!!!!!
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Khe khe mfupa uliomshinda Fisi nani atauweza. Nchi hii walikuwepo wakoloni wakashindwa itakuwa mkwere?

   
 3. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naomba hili nalp liongezwe kwenye maswali ya kumuuliza yeye mwenyewe kesho
   
 4. K

  King kingo JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi naomba kuwaonya kabisa kwenye kituo changu wasije maana sitakubaliana nao, vijana wengi tunaotaka mabadiliko tumeshaamua tutakuwepo kituoni kuanzia kinafunguliwa mpaka majibu yatakapobandikwa kulinda kura zetu.
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  yup
   
 6. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  source pleeese!!!!!!!
  no source no comments!!!
   
 7. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  KAka Kamende,

  Yote hapo juu siwezi sema kitu maana everything s possible...Lakini hili la amani yenu ni ipi na mambo mnayoendeleza huko HAI na kwengineko? Vipi kaka sauti za kilio mapema, hali imegeuka nini?

  Kamende huna haki ya kuongelea kuvunjika kwa amani kwani nawe ni sehemu ya kuvunjika huko na unajua hilo.....
   
 8. Comrade Mpayukaji

  Comrade Mpayukaji Senior Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na amani ina anzia kwa mtu rohoni na wala si risasi. nani anataka mtutu? ila ikibidi kweny kulinda haki zetu pale tutakapoona tunaibiwa sauti ya umma inatosha kuwanyamazisha mafisadi! Hata mawe yatatuunga mkono na hawa majambazi wa thitiem!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kama habari hizi ni za kweli basi wahue kuwa NEC itakuwa imehalalisha uvunjivu wa amani ili kulinda maslahi ya CCM. Lakini naamini Nguvu ya Mungu itashinda na hao vibweka watashindwa kwa jina la Jehova.
   
Loading...