CCM kugeuka kuwa Chama Dola ni kujichimbia shimo

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,325
29,112
Chama cha siasa ni lazima kitumie ushawishi ili kukubalika. Endapo chama kipo madarakani kitawashawishi wafuasi na wapigakura wake kwa kutekeleza ahadi au ilani yake ya uchaguzi. Pia kitaisimamia serikali kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi.

Chama kikikengeuka na kujiona kina hakimiliki ya dola, basi kitatumia vitisho na zawadi kujenga kukubalika. Ninaposema dola namaanisha vitisho vitisho na operesheni za kukandamiza watu waogope kuacha kukiamini.

CCM yangu ambayo leo wale wananaharakati waliokonga nyoyo za watanzania kwa kusimamia ukweli hapo hawali, ndiyo wamepewa nafasi za juu kwenye chama hiki lakini kwa mshangao mkubwa wamegeuka hata ile misimamo yao ya awali.

Kipimo cha uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 kimeshaonesha CCM ni aina gani ya chama. Duniani katika maongozi ya nchi kuna aina tatu za vyama
1. Vyama vya siasa
2. Vyama vya harakati za siasa
3. Vyama dola

Chama changu CCM kimeangukia kwenye hiyo maana ya tatu. Nje ya dola hakitaweza kupumua na kuwa hai.

NINI KIFANYIKE

CCM inahitaji retreat. Inahitaji kubadilika ili kwenda na wakati tulio nao. Baada ya kuwabania upinzani wasifanye siasa na CCM kuendelea na mikutano nchi nzima hiyo inashawishi kuamini kuwa tumekuwa chama kinachoamini kwenye kukandamiza wapinzani wake ili tuendelee kuwepo wepo.

CCM iwatumie wastaafu wake hazina ya wazee kwenye Chama ili kutengeneza mustakabali huku ikishirikisha na kuingiza mawazo mapya.

CCM inapaswa kusimamia misingi yake ya kusimamia na siyo kutamalaki. Chama kisitumike kama daraja la wapenda madaraka na vyeo.

CCM itumie mafanikio ya utekelezaji wa ilani yake kama hoja kwenye ushindani wa kisiasa na siyo kutumia nguvu za dola kushika dola.

Mimi ni MwanaCCM na nitaendelea kusema kweli kwa sababu milango ya kuwafikia walengwa ni mingi. Unaweza kuwafikia ukiwa unatweta kumalizia pumzi kutokana na chujio za kuwafikia kuwa ngumu kupenya.

Msanii
 
Kweli kabisa.

Kinahitaji kuboreshwa na kutoenda nje ya misingi take

CCM ina wajibu wa kulea na kuikuza demokrasia nchini jukumu ambalo ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa.

Tuwe mfano
Ccm ndio chama cha kuwaondolea watanzania shida walizonazo


State agent
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom