CCM kuendelea kujimilikisha nchi kiharamu mwisho umefika. Hatutakubali tena

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Hata mtoto mdogo wa miaka miwili anaelewa fika kabisa CCM kwa sasa wanajimilikisha kiharamu. Hawana uhalali wowote kutoka kwa Mungu wala kwa wapiga kura ndio maana wamekatalia wamebakia kutumia nguvu kuwabambikia kesi wapinzani na kuwateka na kuwapoteza.Hata siku hakuna mabavu yaliyowahi kushinda haki, hakuna giza lililowahi kushinda nuru.

MADAI YA KATIBA MPYA
Madai ya katiba mpya ni msumari wa moto CCM kwa sababu wanaelewa fika kabisa kwamba katiba mbovu iliyopo ndiyo inayowapa uhalali wa kusalia madarakani. Katiba mbovu yenye vyeo vya wakuu wa wilaya na mikoa ambao kazi yao kuu ni kuhakikisha kua CCM inasalia madarakani ndio maana maagizo mengi ya Polisi kutumia nguvu yanatoka kwao kushinikiza wapinzani wakamatwe.

Tunahitaji katiba mpya isiyowatambua wakuu wa Wilaya na mikoa ambao hata ya Warioba iliwakataza na badala ya yake tawala za mikoa na wilaya zibaki chini ya Makatibu tawala na Wakurugenzi ambao kimsingi ndio watumishi wa umma na siyo wajumbe wa kamati za siasa za CCM. Huwezi kuvaa nembo ya chama halafu ukahudumia rais wote na wale wasiokua na nembo ya chama chako.

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI IWE HURA NA YA HAKI
Hakuna asiyefahamu kua Makada wa ccm ndio waliopewa wajibu mkubwa wa kusimamia uchaguzi, mfano ni huyu mkurugenzi wa NEC ambaye kimsingi ni kada wa CCM hakuna asiyejua, huyu ni Agent wa ccm halafu leo hii useme tuna tume huru ya uchaguzi? Lini atasimamia haki?

Kuwepo na tume ya kijaji itakayosimamia mchakato wa kuwapata viongozi wa NEC kuanzia ngazi ya mwenyekiti hati wakurugenzi wake. Wilayani na mikoani kuwepo na Makamishna wa NEC ambao wataomba kazi za kuajiriwa na kupitia usaili badala ya kutumia wakurugenzi wa Halmashauri ambao wana kazi nyingi na wengi wao kwanza hawana taaluma za fani za kusimamia haki za kisiasa kama vile wanasheria na wenye taaluma za sayansi ya siasa.

JE, NI KWELI WAPINZANI WANAWEZA KUONGOZA NCHI?
Hili ni swali la kitoto kabisa ambalo CCM wamekua wakiwaaminisha wananchi eti wapinzani bado hawana uwezo wa kuongoza nchi wakati huo huo kwenye teuzi wakuu wa wilaya na mikoa wamejaza wapinzani ambao wengi wao walilelewa upinzani. Maana yake kama upinzani umejazwa serikalini tayari Opposition ndani ya CCM itakua ni kubwa maana hawa walifuata vyeo na siyo itikadi ya chama, mtu ameingia CCM leo halafu kesho mkuu wa wilaya,ameisomalini itikadi na falsafa ya chama?

Kwahiyo mpaka hapa CCM kikae kikitambua kua muda wowote kinaweza kuumana. Upinzani unaweza kuongoza na kutawala nchi hii na ukaiendesha kwa amani na si kwa maigizo wanayoyafanya wao. Kama hawaamini wapinzani mbona wengi wao ni wakuu wa wilaya na mikoa? Au kwa vile wanamiliki kadi za CCM? Nyoyoni mwao ni wanaccm kweli?
Hawa wote nina uhakika siku upinzani ukichukua nchi watarudi wote, trust me!

CCM KIACHE MAZOEA WAKIAMINI DOLA ITAWALINDA MILELE
Naomba kuhitimisha kwa kusema dola hii ni CHADEMA,CUF,ACT,NCCR na vyama viingine kama ilivyo kwa CCM. Dola hii hii ndani yake imeajiri vijana ambao wazazi wao na ndugu zao ni wapinzani, si wote wanaofurahia unyanyasaji unaofanywa na baadhi ya viongozi wao dhidi ya wapinzani.

Dola hii hii kesho na kesho kutwa itakua chini ya upinzani na inatambua hilo, haiwezi kuibeba CCM kiazi kama wanavyofikiri na zaidi wanafanya Viongozi wao wa juu ambao wanalinda maslahi yao na wanajua kesho wanaostaafu na hawatakutana na utawala wa wapinzani.

Muwe na weekend njema!
CCM iache sikio la kufa!
Maendeleo hayana chama!
 
Mimi najiuliza suali moja:- Ikiwa ccm hawaitaki katiba mpya hivi kweli watakubali mpinzani ashinde?

Lunatic
 
Nje ya tume huru ya uchaguzi na katiba mpya ccm kamwe haiwezi kuwepo kabisa piga ua!

Ni sawa na mgonjwa aliyeharibika mapafu nje ya oxygen ni kifo tu.
 
Kwa Upinzani huu dhaifu uliopo nchini Tanzania ni kheri CCM itawale Tanzania mpaka pale Yesu Kristo na Mtume Mohammed SAW watakapokuja Kutukomboa na kutupeleka Mbinguni kwa Mungu Baba.

Cc: Prof Koboko
... udhaifu wa upinzani ni upi? Fafanua.
 
Kwa Upinzani huu dhaifu uliopo nchini Tanzania ni kheri CCM itawale Tanzania mpaka pale Yesu Kristo na Mtume Mohammed SAW watakapokuja Kutukomboa na kutupeleka Mbinguni kwa Mungu Baba.

Cc: Prof Koboko
Upinzani ungekuwa dhaifu msingewapiga viongozi wao risasi 16 mwilini na kuwafungulia makesi nchi nzima. Imagine mtu ni dhaifu dhohofulhal unamtesa wanini? Unambambikia kesi wanini unampiga risasi 16 mtu dhaifu ili iweje? Basi nyie ni mashetani mnaopiga risasi kuwateka kuwabambika kesi watu dhaifu.
 
Hawana AGENDA ya pamoja kwa Maslahi mapana ya Tanzania na Ustawi wake na kumejaa Matapeli wa Kisiasa na Demokrasia.
Kwanini kuwaunganisha wote kwenye kapu moja? Watakuwaje na ajenda ya pamoja wakati mamluki wamo na hata CCM inatumia vyombo vyote vya dola kuhakikisha hilo halitokei?

Vyama vilivyotangaza waziwazi kuunga mkono chama tawala vinaweza vipi kuwa kapu moja na vingine visivyounga mkono CCM? Si hata Katiba hairuhusu vyama kuungana? CCM inaweka mazingira magumu makusudi kwa kutumia dola halafu inavikebehi vyama kushindwa ku-overcome hayo mazingira!
 
Kuitoa CCM madarakani sio rahisi japo inawezekana kwa kuwa na watu wenye weredi na kusimama kwenye ajenda moja na ya msingi.viongozi wa upinzani wa sasa hawapo seriously bado wanapima kina cha maji,wakiona kina kirefu wanakimbia nchi.
 
Kuitoa CCM madarakani sio rahisi japo inawezekana kwa kuwa na watu wenye weredi na kusimama kwenye ajenda moja na ya msingi.viongozi wa upinzani wa sasa hawapo seriously bado wanapima kina cha maji,wakiona kina kirefu wanakimbia nchi.
Hakuna aliyekimbia nchi Bali ni chama Chao kimeamua kuwapeleka uhamishoni kwa lengo la kubadili mbinu za kivita. Rejea shabulio la M Lissu. Mazingira ya hapa nchini sio salama ktk kudai haki.
 
Madai ni yapi?Katiba mpya?
Au Ccm wako kiharam?..

Manake katika wanaodai katiba mpya wapo pia Wana CCM wengi..
 
Siilaum ccm nalaum system(inner state)kwanini wanashindwa kuweka mfumo imara ya nchi kwa niaba ya maendeleo indelevu bla kujal makundi(ccm.nk sababu lengo n kusonga kwannini mpaka tuongozwe na chama kimoja chenye mlengo mmoja kwn chadema wanatoka madagascar??????et
 
Hakuna aliyekimbia nchi Bali ni chama Chao kimeamua kuwapeleka uhamishoni kwa lengo la kubadili mbinu za kivita. Rejea shabulio la M Lissu. Mazingira ya hapa nchini sio salama ktk kudai haki.
Eti chama kimewapeleka.acha uongo,hivi kuna nani asiyejua Lisu na Lema wanaishi kama wakimbizi,Lema akupewa hifadhi ya ukimbizi Kenya alipokimbilia awali?
Moyo mgumu anao Mbowe tu pekeyake ndo maana yeye yupo jela wangine wametulia,akauna tena harakati mpaka yeye atoke jela.
 
Mbowe yupo jela wewe umelala una chati,alafu unataka kuitoa madarakani CCM wewe,watu hawapo tayari kwenye mabadiliko hii nchi,BBC,CNN,AL JAZEERA sahivi wangekuwa hapa Bongo wanaripoti habari ya kinuko.na CCM wenyewe wanajua fika hawa wapinzani bado sana.
Tatizo mnacheka na washindi wa kura feki ,mnashindwa kuwavuta hata kucha ,ilikuwa akishinda na kura zake feki basi ahame mji ahamie Dar kama wabunge wa CCM wanaoshinda kule Pemba,akishatangazwa mshindi hukodi nyumba akaishi dodoma lakini Pemba huja usiku usiku akiondoka usiku usiku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom