CCM kubalini kuwa mlikosea sana, Yaachieni tu majimbo ya upinzani yarudi upinzani kwa amani. Hamtapoteza kitu!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
CCM kubalini kua mlishashindwa hata kabla ya uchaguzi kurejelewa, kitendo chenu cha kuteua watu ambao waliyaachia majimbo kwa hiyari zao wenyewe bila hata ya kohombezwa na mtu halafu baada ya muda mfupi tu mnawalazimisha kurudi kuomba kura warudi tena kuyawakilisha majimbo hayo sio vyema hata kidogo. Hii haiingiu akili, wananchi hawawezi kuwaelewa kubalini kua mlishapoteza. Wananchi hawawezi kua wajinga kiasi hicho.

Mnawarudisha watu waliokataa ubunge waliopewa na wananchi, mmeambiwa wanchi wanawahitaji tena?

Majimbo mnayarudisha upinzani ninyi wenyewe na wala sio wananchi. Ni imani yangu kwamba hata kura za maoni zingefanyika kama zilivyo taratibu za kawaida kwenye chama, Dr Moleli na Maulidi Mtulia wasingepita wallah nawaambieni. Msiwalazimishe wananchi kufanya dhambi wasiyoipenda kwani maamuzi ni yao na wako huru kuamua nani awaongoze.

Sio tatizo kwani Majimbo ya Siha na Kinondoni yakirudi upinzani hamtapoteza kitu bungeni, upinzani utarudisha majimbo yao na CCM ridhikeni na lile jimbo la Longido mliloachiwa bure na yale mengine mliorudisha kule Singida Kaskazini na Songea.

Naomba amani itawale kwenye kwenye chaguzi hizi, acheni wananchi waamue mwenyewe.
 
Wananchi wanawapenda sana ndio maana wamerudishwa kugombea ni wachapa kazi

Ukiwa arsenal au liverpool lazima akili igande huchukua muda kuhama eneo ulilopo.



NB.

hii post haina mahusiano na ulichokiandika hapo juu
 
Kila siku zinavyokwenda,chadema wanaishiwa nguvu kuhusu kinondoni
Mmepeleka mgombea atakaeshindwa hata kujipigia kura yake,huu ni mzaha wa karne
 
Hawa jamaa walioruka ukuta halafu wamegombea tena...inataka ujasiri kweli kweli.
 
Mkuu MAHANJU itakuwa ni aibu kubwa sana kwa Sizonje kwa juhudi zake za kutumia rushwa ya pesa na vyeo kugonga ukuta. Hivyo ujue fika watu wanaweza kabisa kupoteza maisha ili wahuni wa CCM wapore ushindi mwingine kwa gharama yoyote ile.
 
CCM wanataka ushindi wa kishindo,sawa sawa na Germany alivyotwaa baadhi nchi za Ulaya kwa parade tu.
Labda tuseme lengo lao ni mmoja kila pembe ya nchi wanataka wabunge na madiwani kijani tu,na shida ipo hapo.Lakini yanini kuzunguka sana,si waseme tu wamevifuta vyama vinavyopinga CCM?
 
Ngoja team lumumba waje na mapovu ila kiukweli kwa mm mtu wa field ninaezurula sehemu mbalimbali CCM imebaki kuzikwa tu ila ndio hivyo tena tatzo NEC
 
Back
Top Bottom