Elections 2010 CCM kubadili sheria ya uchaguzi 2010 kujinufaisha?

...mimi hadi sasa sijaona changamoto yoyote imayoletwa na hawa wabunge wa viti maalum ..nadhani njia ya kuwapata si ya ushindani wa kutsha kiasi wanakuwa wengine wapo below standard....kiukweli bora wabunge wa viti maalum wa upinzani kwa kuwa wapo wachache na tunawafahamu.............lakini in reality ccm yenyewe kuna wabunge wa viti maalum wengi sana ambao hawajapata kuuliza swali hata moja bungeni...its like walitupiwa tu kazi ambayo wala hawaiwezi...

mimi nadhani utaratibu uliopo uendelee kila chama kirafute wabunge wake..lakini hizo chaguzi za kuwapata zisimamiwe na MKURUGENZI WA UCHAGUZI.....ili haki itendeke na ionekane imetendeka...tusinyonge demokrasia kwa kuleta utaratibu mpya kandamizi...

LINGINE ni zile NAFASI KUMI ZA RAIS ...NDUGU WAJUMBE NAOMBA TUPIGANIE ILI KILA KIONGOZI ANAYEGOMBEA URAIS NA KUPATA ANGALAU ASILIMIA 5% NA KUENDELEA ...BASI MOJA KWA MOJA APEWE UBUNGE ........KUPATA ASILIMIA 5% TU KWENYE NCHI KUBWA HII SIO RAHISI ..TUSIKUBALI KUPOTEZA MAWAZO YA MTU KAMA HUYU.....MARA NYINGINE TUTAWEZA KUMLEA NA AKAKUWA ZAIDI KUJA KUFANYA VYEMA BAADAYE.....KWA WAZO KAMA HILI BUNGE HILI WATU KAMA :-

PROF . LIPUMBA IBRAHIM NA JUMA DUNI HAJI
NDG; FREEMAN MBOWE ,.na MAULIDA ANNA KOMU.

IKIWEZEKANA NA WAGOMBEA WENZA WAO ...HAO WALIPATA ZAIDI YA ASILIMIA 5%.......MCHANGO WAO BUNGENI UNGEKUWA NA CHANGAMOTO KUBWA....SASA HIVI MTU AKIGOMBEA...NI KAMA ANAPOTEA TENA ..HANA JUKWAA..ANASUBIRI UCHAGUZI UJAO ..BILA WANANCHI KUMSIKIA KWENYE JUKWAA RASMI.........

MWAKA 1995..WALIOPATA ZAIDI YA 5% NI:-

JOHN CHEYO MAPESA
IBRAHIM LIPUMBA
AUGUSTINE MREMA ....

TUMESHUHUDIA KILA ANAYEGOMBE ...UCHAGUZI UNAOFUATA HUSHUKA ZAIDI ..NADHANI KUNA TATIZO,,,,,,....

KAMA HII IKIKUBALIWA ..HAITAGARIMU ZAIDI YA NAFASI NNE KATI YA KUMI ZA RAIS....AMABAZO MARA NYINGINE HUWA HAZITUMII ZOTE.....

KIMSINGI WAZO LA KUPANUA BUNGE SASA NO..TUNAHITAJI KUFANYA UTAFITI KUJUA MCHANGO WA BUNGE KWA SASA ...KAMA KWA IDADI YA SAA WANAFIKIA MALENGO NA MATARAJIO YETU ,..NDIO TUPANUE,,SIO KUPANUA KISIASA...
 
Niliandika barua hii mwezi Mei 2006. Nikaandika tena mwezi Septemba 2007 barua yenye maudhui haya haya lakini bora zaidi. Ninaamini njia bora zaidi ya kuiimarisha demokrasia yetu ni kkuboresha mfumo wetu wa uchaguzi na kuwa na mfumo wa mchanyato wa wengi wape na uwakilishi wa uwiano. Utaimarisha Taasisi za Demokrasia na utahakikisha kila kura ina thamani na kuhesabiwa (every vote counts)

Tabora,
31 Mei 2006

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Ikulu,
Dar es Salaam.

Ndugu Rais,

MAAMUZI YA MAHAKAMA KUHUSU WAGOMBEA BINAFSI
NA UMUHIMU WA KUBADILI MFUMO WETU WA UCHAGUZI

Kwanza naomba nikupe pongezi kwa kuchaguliwa kwako kuwa Kiongozi wa nchi yetu. Inawezekana kuwa tayari nimeshakupa hongera tulipokutana pale Dodoma siku uliyomwapisha Waziri Mkuu Ndg. Edward Lowassa au vile vile tayari umekwisha pongezwa na Mwenyekiti wangu wa chama cha CHADEMA ndg. Freeman Mbowe pale Diamond Jubilee. Hata hivyo, kwa kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kuwasiliana na wewe kama Rais kwa barua, nimeona ni bora nikupe hongera zangu tena.

Vile vile nikutie moyo kwa kazi unayofanya. Umeanza kazi kwa kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya ili kuleta Mabadiliko ya kweli na Uhuru wa kweli kwa jamii ya Watanzania.

Kwamba timu yako nzima ya uongozi inafanya kama wewe ni suala la mjadala mwingine. Sina shaka hata kidogo kuwa Waziri Mkuu na Spika wa Bunge letu tukufu wanaendana na ari yako. Ninaamini watakusaidia vya kutosha. Nina imani kubwa sana na viongozi hawa licha ya changamoto kadhaa ambazo ninaamini ni matatizo ya kimfumo (systematic inherent problems) tu ambayo hata sisi tungefanikiwa kupata ridhaa ya Watanzania na kuongoza taifa letu tungekutana na changamoto hizo. Nikisema sisi, ndugu Rais, nina maana CHADEMA.

Ndugu Rais, barua hii ni yangu binafsi kama kijana mwenye kulipenda taifa langu na bara langu la Afrika. Kwa kuwa nina ofisi ya kitaifa, kama Mbunge, nakuomba uchukulie barua hii kama inatoka kwa Mbunge kwenda Rais wa nchi ambae ni sehemu ya pili ya Bunge.

Barua hii ina mawazo ya kujaribu kusaidia kutokana na changamoto iliyopo mbele yetu kufuatia hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu kuruhusu wagombea binafsi wa uongozi wa nchi yetu. Wagombea binafsi maana yake ni wagombea wasio na vyama vya siasa. Wanaweza kuwa ni wanachama wa vyama, lakini hawana dhamana ya vyama vyao wanapogombea na kisha kuchaguliwa kuwa viongozi.

Ndugu Rais, kuwa na mgombea binafsi haina maana kuwa mgombea huyu hatakuwa na udhamini wa aina fulani. Mfano, Kikundi cha Wafanya biashara wa zao fulani (mfano Tumbaku kule Urambo) wanaweza kudhamini watu kadhaa, wakagombea udiwani, wakashika “majority” ya Halmashauri ya Wilaya. Maana yake ni kuwa maamuzi yote ya Halmashauri ya Wilaya Urambo yatakuwa chini ya kundi hili. Hii inawezekana. Inawezekana pia hata kwa ngazi ya Ubunge. Sina uhakika katika ngazi ya Urais. Lakini sina haja ya kukuhadithia alichofanya Rais Bingu wa Mutharika wa Malawi.

Ndugu Rais, Vyama vya siasa vimewekewa masharti ya kuandikishwa. Kuna sheria inayopelekea vyama kusajiliwa na kuna ofisi ya Msajili wa vyama anaeratibu vyama vyote ikiwemo chama chako, CCM. Hata kama mmoja wa wajumbe wa secretariat ya chama chako alinukuliwa akisema Msajili wa vyama ni karani tu, lakini ofisi hii ina majukumu makubwa sana ya kuhakikisha taifa halimeguki kisiasa. Ingawa nina mawazo tofauti, kwamba ofisi hii ingeweza kuwekwa chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi badala ya muundo wa sasa. Lakini hii sio hoja kwa sasa.

Kiufupi ni kwamba vyama vinaratibiwa. Katiba zao na hata kanuni zao za uteuzi wa wagombea wa nafasi zote zipo kwa Msajili. Msajili aweza kufuatilia kuona kama chama kinafuata taratibu zake na anao uwezo wa kuonya.

Ndugu Rais, nchi haiwezi kuwa na ofisi ya kuratibu wagombea binafsi. Nidhamu yao Bungeni na hata katika Mabaraza ya madiwani haitaweza kushughulikiwa na vyama. Hawa hawana vyama!

Ndugu Rais, sio nia yangu hata kidogo kushauri kuwa tusiruhusu wagombea binafsi. Hii itakuwa ni kuzuia uhuru wa Mtanzania kushiriki katika uongozi wa nchi. Mahakama imesema ni kinyume na Katiba. Katiba ambayo sote tumeapa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea. Kiapo tulichokula ni kikubwa sana na lazima tuheshimu kiapo. Hata hivyo, suala hili ni lazima tuliangalie kwa mapana yake.

Mara baada ya mahakama kutoa hukumu nilinukuliwa na magazeti ya hapa nyumbani na moja na Ghuba (Gulf Times) na lingine na Marekani (The Herald Tribune). Nilisema kuwa maamuzi ya mahakama yanatutaka tufanye mabadiliko makubwa ya mfumo wetu wa siasa. Maamuzi ya mahakama yanaweza kuudhoofisha mfumo wa vyama nchini kwetu.

Uzoefu wangu unaonesha kuwa Watanzania hawapendi vyama. Sio manazi wa vyama vya siasa. Hawaoni kama vyama vinawawakilisha. Wanaona vyama kama vikundi tu vya watu wenye madhumuni ya kutawala. Hawaoni vyama kama Asasi muhimu za kujenga demokrasia na kutoa sera mbadala. Ndio maana kati ya Watanzania milioni 16 waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2005, ni Watanzania milioni tano tu ndio wanachama wa vyama. Hata wewe ndugu Rais, umechaguliwa na Watanzania milioni 9 wakati chama chako kina wanachama milioni tatu tu!

Kwa hali hii ya udhoofu wa vyama kutokukonga nyoyo za Watanzania, wagombea binafsi wanaweza kuvuruga kabisa mfumo wa vyama. Hii ni hatari ninayoiona. Ni hatari kweli kweli. Ni hatari kwa sababu, nchi inaweza kukatika kwa matamshi tu ya mtu ambae hana chombo cha kumdhibiti. Vyama vinadhibiti wanachama wake.

Ndugu Rais, mimi binafsi nina maoni yafuatayo ili kuimarisha Demokrasia katika nchi yetu kufuatia hukumu ya mahakama kuu. Mapendekezo yangu haya yanaweza kuwa sehemu ya mjadala wa kitaifa uliouahidi wakati ulipolihutubia Bunge mwishoni mwa Disemba 2005.

Serikali ikubaliane na maamuzi ya Mahakama:
Mabadiliko ya Katiba yapelekwe Bungeni na kuondoa vizuizi vya Watanzania kugombea uongozi kwa kudhaminiwa na vyama. Sheria ya Uchaguzi ifanyiwe marekebisho na kuweka masharti kadhaa ya kufuata kwa mgombea binafsi. Mfano, mgombea mtarajiwa kupata wadhamini 50 kutoka kila kata iliyopo katika Jimbo, kama anagombea Ubunge na wadhamini 20 kutoka kila Mtaa/Kijiji katika Kata kama anagombea Udiwani. Kama anagombea Urais, apate wadhamini 1000 kutoka kila Mkoa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mfumo wa Uchaguzi urekebishwe na kuruhusu mfumo mchanyato wa uwiano wa kura na mfumo wa “first-past-the-post”:
Ndugu Rais, mfumo wetu wa uchaguzi unataka Wabunge na Madiwani kupatikana kutoka katika majimbo na kata tu. Wabunge wanawake hupatikana kwa uwiano wa kura za Wabunge nchi nzima na Madiwani wa wanawake kutokana na uwiano wa viti vya udiwani ambao kila chama kimepata.

Lakini Wabunge Wanawake hawana mamlaka ya kisheria kwa eneo maalumu. Kwa sasa ni rahisi kusema kuwa wanatoka mikoani, lakini hii ni kwa sababu tuna chama kimoja kikubwa na hivyo kupata kura za kuenea mikoa yote. Huko mbele, tena na hawa wagombea binafsi, itatokea mikoa ambayo haitapata wabunge wanawake kwa sababu kura hazitotosha kwa chama kimoja kugawa wabunge kila mkoa. Umefikia wakati sasa kufanya mabadiliko makubwa ya mfumo wa uchaguzi ili kuingiza uwakilishi wa uwiano.

Napendekeza kama nchi tutafakari mambo yafuatayo yanayohusu mabadiliko ya mfumo wa kisiasa wa nchi yetu:
Wabunge wa kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi watokane na Halmashauri za Wilaya za sasa. Mfano, badala ya Wilaya ya Manispaa ya Kinondoni kuwa na Wabunge watatu, iwe na Mbunge mmoja tu. Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji ndio iwe Jimbo la Uchaguzi. Katika ngazi hii wagombea wasio na vyama waruhusiwe pamoja na wale wenye vyama.

Kwa hali ya sasa tutapata Wabunge 119 kutoka kundi hili. Idadi yao itaongezeka kutokana na kuongezeka kwa Halmashauri zitakazoundwa pindi mahitaji yanapotokea. Haitakuwa tena kazi ya Tume za Uchaguzi kuunda Majimbo ya uchaguzi bali vile vigezo vya kuunda Halmashauri (Baraza la Madiwani) vilivyopo kisheria (Local Government Authorities Acts) ndio vitatumika.

Wabunge 231 watokane na kura za uwiano. Vyama vya siasa vitapata viti kutokana na uwiano wa kura ambao kila chama kimepata katika Mkoa. Chama cha siasa ni lazima kiwe kimepata kwanza asilimia tano ya kura zote zilizopigwa katika Mkoa husika ili kigawiwe viti. Kwa hiyo kila chama kitatengeneza orodha ya wagombea wake kwa kila Mkoa na kuipeleka Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Orodha hii iwe katika hali ambayo kama jina la kwanza ni Mwanaume la pili awe Mwanamke, hali kadhalika kama jina la kwanza ni Mwanamke katika orodha la pili liwe la mwanaume. Mikoa itapata idadi ya Wabunge kutokana na vigezo maalumu, mfano idadi ya watu n.k. Jambo la kuzingatia tu ni kwamba idadi ya sasa ya Wabunge katika mikoa isishuke baada ya mabadiliko haya (no region shall be left worse off).

Mfano Mkoa wa Kigoma una Jumla ya Wabunge saba wa Majimbo. Iwapo tukibadili mfumo kama ninavyopendekeza hapa, kutakuwa na wabunge wanne wa kuchaguliwa, kutoka Halmashauri za Wilaya Kasulu, Kibondo na Kigoma na Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji. Hivyo wabunge watatu watagawiwa kwa vyama kutokana na uwiano wa kura ambao kila chama kitapata.

Kwa mapendekezo haya tuna uhakika wa kuwa na Wabunge wanawake zaidi ya theluthi moja katika Bunge. Lakini pia tutakuwa na uhakika kwamba kila Mkoa utakuwa na Mbunge au Wabunge wanawake.

Ndugu Rais, mabadiliko haya ya mfumo wetu wa Uchaguzi yana faida nyingi sana. Moja ya faida ni kuvigeuza vyama vyetu vya siasa kutoka katika kushindanisha watu tu, bali pia kushindanisha sera. Kwa sababu wananchi watakuwa wanapiga kura mbili. Kura moja ya chama na kura nyingine ya ama diwani au Mbunge na Rais. Kura ya chama ndio itatufanya kupata wabunge wa uwiano. Wala hatutatumia mfumo mmoja kuzalisha mfumo mwingine. Bali kila mfumo utazalisha Wabunge kuunda Bunge letu.

Vyama vikianza kushindanisha sera tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana kama nchi katika kuimarisha mfumo wa demokrasia na kwa kweli hatutokuwa na wasiwasi wa vyama kudhoofika kutokana na wagombea Binafsi kuruhusiwa.

Demokrasia ndani ya vyama itaimarika kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi itahakikisha vyama vinapata wawakilishi wake katika Orodha ya Mikoa kidemokrasia. Pia pale Bungeni uliahidi kutengenezwa kwa “code of conduct” ambazo zitakuwa binding kwa kila chama ili kuimarisha demokrasia ndani ya vyama.

Ndugu Rais, najua una majukumu mengi ya Kitaifa. Sitaki nikuchoshe na barua yangu hii.

Hata hivyo, sisi hatutokuwa wa kwanza kufuata mfumo huu wa uwiano. Ndugu zetu wa Msumbiji wanafanya hivi. Pia Afrika ya Kusini, Ujerumani, Uswidi na hata India.

Mfumo huu, pia unaweza kumaliza matatizo ya kisiasa ya Zanzibar kwani kila kura itakuwa na thamani. Wawakilishi wa Zanzibar watatokana na kura za kila chama. Kura za Wapemba walio CCM na za Waunguja walio CUF zitahesabika. Hivyo, ile hali ya Pemba yote kutoa Wawakilishi au Wabunge wa CUF tu au Unguja yote kutoa Wawakilishi au Wabunge wa CCM tu itaondoka. Hali hii pia inaweza pelekea kupatikana kwa vyama vingine vyenye wawakilishi au Wabunge kutoka Zanzibar, kwani ushindani utakuwa ni wa sera za vyama na sio watu.

Ndugu Rais, naomba utafakari mawazo yangu haya. Ninaamini kuwa ni muhimu kufanya mabadiliko ya mfumo wa siasa. Kesi ya Mtikila sio sababu pekee ya mabadiliko, bali tunakokwenda hatuwezi kukwepa mabadiliko kwa faida ya demokrasia ya nchi yetu.

Kwa leo naomba niishie hapa. Nakutakia kila la kheri katika kazi.

Kwa ruhusa yako nina nakili barua hii kwa Spika wa Bunge letu Tukufu na pia kwa wasaidizi wako muhimu. Pia nina nakili barua hii kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ambae pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala.

Wako mtiifu,

Zitto Z. Kabwe (Mb)

Kigoma Kaskazini.
 
Niliandika barua hii mwezi Mei 2006. Nikaandika tena mwezi Septemba 2007 barua yenye maudhui haya haya lakini bora zaidi. Ninaamini njia bora zaidi ya kuiimarisha demokrasia yetu ni kkuboresha mfumo wetu wa uchaguzi na kuwa na mfumo wa mchanyato wa wengi wape na uwakilishi wa uwiano. Utaimarisha Taasisi za Demokrasia na utahakikisha kila kura ina thamani na kuhesabiwa (every vote counts)

.

Safi sana. Kuna makala ilitoka Tanzania Daima Jumapili ambayo niliiandika na kuunganisha maudhui yaliyojadiliwa kwenye mjadala huu, na ya kwenye hii barua yako kwa Rais nikirejea mada ambayo niliwahi kuandika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005: Uzoefu kuhusu Uendeshwaji wa Uchaguzi Tanzania

Naungana mkono hoja ya kuwa na Mfumo mchanyato. Chini ya mfumo huo natarajia pia makundi mengine ya kijamii mathalani walemavu, wanawake, vijana nk yatawakilishwa vizuri zaidi. Chini ya mfumo huo hata hiyo hoja ya Phillimon michael kuhusu Wagombea Urais waliofanya vizuri kuungia bungeni inaweza kuingizwa kirahisi zaidi badala ya kusubiria uteuzi wa viti kumi vya Rais.

Huu ni mjadala muhimu na hatua za haraka inabidi zichukuliwe.

BTW: Uchaguzi wa Serikali za Mtaa ni 2009; naona serikali imeshikilia msimamo kuwa uchaguzi huo uendelee kuendeshwa na serikali yenyewe badala ya Tume ya Uchaguzi. Ni nafasi ya uchaguzi huo katika muktadha wa mjadala wa mfumo wa mchanyato?

JJ
 
Safi sana. Kuna makala ilitoka Tanzania Daima Jumapili ambayo niliiandika na kuunganisha maudhui yaliyojadiliwa kwenye mjadala huu, na ya kwenye hii barua yako kwa Rais nikirejea mada ambayo niliwahi kuandika baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005: Uzoefu kuhusu Uendeshwaji wa Uchaguzi Tanzania

BTW: Uchaguzi wa Serikali za Mtaa ni 2009; naona serikali imeshikilia msimamo kuwa uchaguzi huo uendelee kuendeshwa na serikali yenyewe badala ya Tume ya Uchaguzi. Ni nafasi ya uchaguzi huo katika muktadha wa mjadala wa mfumo wa mchanyato?

JJ

Uchaguzi wa serikali za Mitaa kuendelea kuendeshwa na TAMISEMI kwa mfumo wa sasa ni tatizo na serikali inataka hivyo ili kuiba uchaguzi huu kama ilivyofanya mwaka 2004.

Tume nayo kuendesha uchaguzi ni tatizo kwani credibility yao ni ndogo sana. Uchaguzi huu ni wa kijamii, tunachagua viongozi ambao kwa kweli sio wa kisiasa ukiangalia kazi zao za kila siku katika vijiji vyetu, kazi zao ni za kijamii zaidi. Mawazo yangu binafsi ni kuufanya uchaguzi huu usiwe wa vyama vya siasa. Uwe uchaguzi huru kabisa kwa kila raia pale kijijini au mtaani na kitongojini. Vyama viwe nje ya uchaguzi huu. Hata hivyo hili kwa sasa haliwezekani.

Then, uchaguzi huu uendeshwe na Kamati za Uchaguzi kila Mkoa. Kamati hizi ziwe na uwakilishi wa vyama vya siasa vilivyopo katika mkoa husika na mwenyekiti wa Kamati awe Hakimu Mkazi na katibu awe RAS. Wasimamizi wa uchaguzi wawe mahakimu wa mahakama za mwanzo huko vijijini na DED asiwemo kabisa katika mchakato wa uchaguzi.

These are just raw ideas, nadhani we have to think out of the box regarding these communal elections/civic elections.
 
Last edited:
...LINGINE ni zile NAFASI KUMI ZA RAIS ...NDUGU WAJUMBE NAOMBA TUPIGANIE ILI KILA KIONGOZI ANAYEGOMBEA URAIS NA KUPATA ANGALAU ASILIMIA 5% NA KUENDELEA ...BASI MOJA KWA MOJA APEWE UBUNGE ........TUSIKUBALI KUPOTEZA MAWAZO YA MTU KAMA HUYU.....MARA NYINGINE TUTAWEZA KUMLEA NA AKAKUWA ZAIDI KUJA KUFANYA VYEMA BAADAYE.....KWA WAZO KAMA HILI BUNGE HILI WATU KAMA :-

PROF . LIPUMBA IBRAHIM NA JUMA DUNI HAJI
NDG; FREEMAN MBOWE ,.na MAULIDA ANNA KOMU.

IKIWEZEKANA NA WAGOMBEA WENZA WAO ...HAO WALIPATA ZAIDI YA ASILIMIA 5%.......MCHANGO WAO BUNGENI UNGEKUWA NA CHANGAMOTO KUBWA....SASA HIVI MTU AKIGOMBEA...NI KAMA ANAPOTEA TENA ..HANA JUKWAA..ANASUBIRI UCHAGUZI UJAO ..BILA WANANCHI KUMSIKIA KWENYE JUKWAA RASMI.........

MWAKA 1995..WALIOPATA ZAIDI YA 5% NI:-

JOHN CHEYO MAPESA
IBRAHIM LIPUMBA
AUGUSTINE MREMA ....

TUMESHUHUDIA KILA ANAYEGOMBE ...UCHAGUZI UNAOFUATA HUSHUKA ZAIDI ..NADHANI KUNA TATIZO,,,,,,....

KAMA HII IKIKUBALIWA ..HAITAGARIMU ZAIDI YA NAFASI NNE KATI YA KUMI ZA RAIS.......

Mkuu Philemon, umegusa yale ambayo nimekuwa nikiyawaza muda mrefu. Ni hazina kubwa ambayo tumekuwa tukiitupa jalalani kila kipindi cha uchaguzi kinapokwisha. Naunga mkono kuwa sheria iangaliwe na hawa wagombea wa urais wanapopate kura zaidi ya asilimia fulani na ambapo hawakuushinda urais, moja kwa moja basi wawe WABUNGE. Vinginevyo, basi waruhusiwe kugombea ubunge, na endapo wakishinda urais, basi kuwe na uchaguzi mdogo kujaza nafasi itakayo kuwa wazi (Ila utaratibu wa kwanza wa asilimia ya kura za urais ni nzuri zaidi). NINGEOMBA UIANZISHE KAMA THREAD INAYOJITEGEMEA ILIIPATE NGUVU NA IJADILIWE YENYEWE.
 
Wanabodi,
Swala la viti maalum bungeni kwa wanawake ni swala la WANAWAKE sio vyama ama sisi wanaume kuwapangia kwa kutumia maguvu yetu ya kiume..Hata huo mpango uliopo sasa hivi binafsi sikubaliani nao kwa sababu hauleti Uwakishi wa Wanawake bungeni kwa haki zao isipokuwa kwa kutumia siasa za Chama...Na ndio maana kuna watu walishindwa kuelewa kuhusiana na Wabunge wa viti maalum wa Chadema kuwa hawa ni Wanawake kwanza na wanawakilisha wanawake sio swala la kabila zao, hivyo Uwakilishi wao unakwenda kwa Wanawake wote nchini na sio kabila zao..Siwezi kuamini kabisa kuwa Wanawake wanatakiwa kuwakilisha hoja zao kwa kutazama mrengo na siasa za vyama hata kidogo..

Wanawake wana haki zao, malengo yao na haijalishi yuko chama gani cha siasa..Ni sawa na kitengo cha Wanawake UN ambacho malengo yake yametazama haki na mahitaji ya Wanawake wote duniani bila kujali siasa za nchi hizo..
Kama alivyosema Mnyika hata kama kutakuwepo viti kwa ajili ya watoto walemavu, Yatima na kadhalika haitakiwi wawakilishi wao wafungwe ktk mrengo ama sera za vyama isipokuwa zao wao wenyewe kulingana na malengo na matakwa yao..
Uchaguzi wowote unahusu viti vya Wanawake ufanywe kwa kutumia wanawake wasiofungamana na siasa za chama chochote kwani wapo bungeni kuwakilisha wanawake WOTE TANZANIA, sio wanawake ndani ya vyama vya siasa...
 
CCM yataka kila wilaya kuwa Jimbo
Martha Mtangoo, Dodoma
Daily News; Monday,November 10, 2008 @21:15

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imeunda kamati teule ya kupitia mapendekezo kuhusu namna ya kuwapata wabunge na wawakilishi wanawake ambapo imependekeza kila wilaya kuwa jimbo litakaloongozwa na mwanamke na kufikia asilimia 50.

Ili kufikia asilimia 50, NEC hiyo ya CCM imetoa pendekezo la kuzifanya wilaya zote nchini kuwa majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya wagombea wanawake. Aidha, NEC imeomba serikali kuharakisha kutunga sheria ya uchaguzi itakayomtaka kila mgombea kueleza fedha anazotumia katika kampeni amezipata wapi na zimetumikaje, sheria ambayo sasa haipo.

Katibu wa NEC wa Itikadi na Uenezi, John Chiligati aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kuwa kwa utaratibu huo wa uwakilishi, utawezesha kupatikana kwa wabunge wanawake 137 kutoka wilaya 137 za Tanzania Bara sawa na asilimia 38 katika Bunge la Muungano.

Alisema kwa upande wa Baraza la Wawakilishi, wawakilishi wanawake 20 kutoka wilaya 10 za Zanzibar ambapo kila wilaya za Unguja na Pemba, watatoka wanawake wawili. Alisema pia wanawake wataendelea kugombea katika majimbo 232 yaliyopo hivi sasa katika Bunge la Muungano ambako asilimia 12 iliyobaki inaweza kupatikana ili kufikia asilimia 50.

Alisema Kamati hiyo teule chini ya aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Dk. Mohamed Gharib Bilal, imepewa jukumu la kuchambua kwa makini namna ya pendekezo hilo linavyoweza kutekelezwa. Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Makamu Mwenyekiti Anne Makinda; Dk. Maua Abeid Daftari, William Lukuvi, Jenista Mhagama, Machano Othman Said, Andrew Chenge, Mtumwa Kassim Idd na Dk. Milton Mahanga.

Chiligati alisema pia kamati hiyo itaangalia uwezekano wa kuundwa upya majimbo ya sasa kwa lengo la kuyapunguza ili kila jimbo liwe na wabunge na wawakilishi wawili, mmoja akiwa ni mwanamke na wa pili akiwa ni mwanamume ili idadi ya wabunge isizidi 360.

Alisema NEC imeipa kamati hiyo jukumu la kuona uwezekano wa Tanzania kutumia mfumo wa uwakilishi wa uwiano ambao vyama huandaa orodha ya wagombea wa ubunge na kuikabidhi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambapo baada ya uchaguzi, kila chama hupata idadi ya wabunge kulingana na wingi wa kura alizopata.

Aliitaja kazi nyingine ya kamati hiyo ni kuchambua utekelezaji wa pendekezo la namna ya kuwashirikisha wanaCCM matawini katika kupiga kura za maoni za kuwapata wagombea wa ubunge na uwakilishi. Alisema chini ya utaratibu huo, kura za maoni zitapigwa na wajumbe wa mkutano wa Jimbo tofauti na ilivyo sasa.

Alisema kamati hiyo imepewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha kazi hiyo, na mapendekezo hayo yatajadiliwa na kupitishwa katika kikao kijacho cha NEC na baadaye kufikishwa kwa wananchi kwa kujadiliwa na kupata mwafaka iwapo serikali pia itaridhia mapendekezo hayo.

Kuhusu uharakishaji wa kutunga sheria ya fedha za kampeni, Chiligati alisema ombi hilo limetolewa kutokana na baadhi ya wagombea katika uchaguzi mbalimbali na hasa uchaguzi mkuu kutumia fedha nyingi, jambo ambalo limedaiwa kuwa limekuwa linaigawa CCM.

Chiligati alisema NEC imejadili na kuomba sheria hiyo itungwe haraka ili ianze kutumika katika Uchaguzi Mkuu ujao ili kuziba mianya ya rushwa na hasa katika kipindi cha uchaguzi. Alisema sheria hiyo itakapotungwa na kuanza kutumika, itadhibiti vitendo vya rushwa ambapo kila mgombea atatakiwa kuelezea ni namna gani ametumia fedha katika uchaguzi na fedha hizo amezitoa wapi na pia sheria hii itaweka kiwango cha juu cha fedha ambazo zitatakiwa kutumika katika uchaguzi.

“Katika sheria hii, itamtaka kila mgombea kuelezea pesa anazofanyia kampeni amezitoa wapi na kwa akina nani na hao watu wataulizwa iwapo ni kweli na pia mgombea atatakiwa kuelezea pesa hizo amezitumiaje katika uchaguzi. Mgombea ndani ya chama kuwa na mapesa mengi anakigawa chama,” alisema Chiligati.

Kuhusu rufaa ya Nape Nnauye, Chiligati alisema NEC haikuijadili kutokana na rufaa hiyo kwenda moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Aidha, Chiligati alisema NEC haikuwa na ajenda ya kumjadili Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na kuongeza kuwa ajenda hiyo haikuwapo na haitakuwapo.

Alisema NEC ilipitisha majina ya wagombea wa nafasi mbalimbali wa Jumuiya; na kwa nafasi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa ni Suleiman Muhsun Haji, Hamad Masauni Yussuf na Adilla Hilai Vuai; wakati kwa Makamu Mwenyekiti ni Beno Malisa, Zainabu Rashid Kawawa na Hussein Bashe.

Kwa upande wa Umoja wa Wanawake (UWT), waliopitishwa ni Janet Kahama, Joyce Masunga, Sophia Simba kwa Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti ni Asha Bakari Makame. Kwa Uenyekiti wa Wazazi ni Alhaji Abdallah Bulembo, Athumani Mhina na Esther Nyawazwa huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Khamis Suleiman Dadi, Haidar Haji Abdallah na Dogo Iddi Mabrouk.
 
Busara isipotumika vizuri tunajiingiza kwenye matumizi mazito kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wanasiasa na siyo jamii. sidhani kama tunahitaji wabunge wengi bali tunahitaji huduma za kijamii ziongezeke. kuongeza idadi ya wabunge ni kuzidi kukigawa kidogo sana tulicho nacho.
 
Waheshimiwa,

Katika taarifa za vikao vya CC na NEC za CCM wametoa dhamira ya kubadili mfumo wa kuwapata wagombea nafasi mbalimbali kupitia CCM.

Inaelekea mwaka 2010, hakutakiwa na kuwakusanya wajumbe sehemu moja na kuchagua wawakilishi wao na badala yake itakuwa kama ile ya USA. Wote wanazunguka vijiji vyote na kura zinapigwa na wanachama wote.

Huu ndio utaratibu ulikuwepo hata hapo mwanzoni baadaye ukafutwa kwasababu ya kuogopa gharama.

Nini mawazo yenu kuhusu utaratibu huu mpya hasa kwenye mambo kama ya rushwa na pia gharama hasa kwa wagombea ambao hawatakuwa na uwezo mkubwa?

Huko nyuma wagombea wote walikuwa wanakuwa kwenye gari moja la chama na hivyo kupunguza gharama. Huenda sasa kila mtu ataendesha kampeni zake mwenyewe.

Binafsi nilikuwa sipendi utaratibu wa sasa ambao wajumbe walikuwa mpaka wanafichwa sehemu na kumwagiwa vyakula na pombe kama njia ya kuwarubuni kura. Naamini utaratibu wa 2010 huenda ukapunguza rushwa za kwenye uchaguzi maana utahonga watu wangapi?
 
They are upto no good.Whatever they come up with,is just to make sure their party remains stronger and powerfully as never!
 
Hi ni fursa chanya kwetu vijana ktk kuingia medani za siasa za ushindani, ni imani yangu kuona idadi kubwa ya vijana si watoto kuingia ktk siasa za ushindani ktk nchi yetu kupitia CCM.

Nami nafikiria pia kuingia ktk mchakato endapo hali ya hewa kisiasa itaruhusu kwa watu wa kipato cha kawaida kujitosa ktk siasa na kuipa fursa jamii ya kuiona tofauti ya CCM.
 
hawa ccm,sasa wanataka kuipeleka nchi ndiko siko,mimi sioni umuhimu wa kuwa na wabunge wengi bila sababu,hawa waliopo tu ni mzigo tosha kwa wananchi tena watuongezee wengine 137,kwa gharama za nani ?
kama kweli serikali ina pesa za kuwalipa hao wabunge wa nyongeza kwa miaka mitano,kwa nini tusijenge hospitali ya rufaa kila mkoa ?
 
Katibu,
Binafsi nashindwa kuelewa, hivi nchi haina dira na vipaumbee vyake??

Hivi nchi inaendeshwa tu kama genge, leo unaamua kuuza nyanya kesho vitumbua, keshokutwa maharage?

Hivi kweli vipaumbele vyetu watanzania ni kuwa na wabunge lukuki wanao tanua kwenye mashangigi eti wana wakilisha wananchi walio zama katika lindi la umasikini?

Sioni matinki ya jimbo moja kuwa na wawakilishi wawili, wanini? na mgawanyo wa majukumu yao utakuwa ni upi?

JAMENEI KUWENI WAUNGWANA, MASIKINI TULIO CHOKA NAMNA HII BADO MNAONA ZAWADI YETU NI KUTUTWISHA MZIGO WA BUNGE KUUBWA KWA AJILI YA KUFULFILL POLITICAL WILL YA MTU??

kuweni serious tujenge nchi, ni aibu RWanda na Burundi kutupiga bao Tanzania!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom