Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 79
CCM yaizidi kete CHADEMA, yabuni mbinu ya kupunguza wabunge wa upinzani
CCM imebuni kete mpya ya kuizidi CHADEMA na kupunguza nguvu ya upinzani bungeni. Katika mkakati huo mpya ambao umeshapata baraka ya kamati kuu ya chama hicho ukisubiri kupitishwa na NEC hivi karibuni, katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho kuweza kutekeleza mkakati huo. Chini ya marekebisho hayo, wabunge wa viti maalum hawatapatikana kwa kuteuliwa na vyama bali watagombea kupitia wilaya ambazo ndizo zitakazo kuwa majimbo ya wanawake pekee. Chini ya mfumo huo mpya, patakuwa na majimbo ya kawaida 232 ambayo yatagombewa na watu wote kwa kama ilivyo utaratibu wa sasa. Kwa upande mwingine viti maalum vya wanawake pekee 75 vitaondolewa na badala yake wanawake watagombea wenyewe kwenye wilaya 130 za Tanzania. Kwa hali hiyo, kutakuwa na ongezeko la wabunge ambalo litalazimisha taifa kupanua tena ukumbi wa bunge na pia bajeti ya matumizi ya wabunge ya mishahara na posho itabidi iongeze kwa zaidi ya bilioni 50. Kwa idadi hiyo ya wabunge, Tanzania itaingia katika kundi la nchi zenye wabunge wengi zaidi.
Mkakati huo umebuniwa kupunguza nguvu za kambi ya upinzani hususani CHADEMA ambayo imepata kutokana na kupata wabunge wengi wa viti maalum kutokana na idadi ya kura ambazo chama hicho na vingine vya upinzani vimeokoteza nchi nzima.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 CHADEMA ilipata wabunge watano tu wa kuchaguliwa lakini ikapata wabunge wa viti maalum sita kutokana na kura ambazo chama hicho kilipata katika uchaguzi. Kama viti maalum vingetolewa kwa idadi ya viti ambavyo chama kimepata chama hicho kingepata kiti maalum kimoja au viwili tu.
Unajua tumeweka sheria inayoisaidia CHADEMA, hawa chini ya Operesheni Sangara hata kama tukitumia nguvu kushinda majimbo bado watapata zaidi ya asilimia 20-40 ya kura katika majimbo mbalimbali hali itayofanya wapate kati ya wabunge 15 mpaka 30 wa viti maalum mwaka 2010. Lazima tutafute njia ya kuwadhibiti mapema kwa kubadili sheria, alinukuliwa mmoja wa wajumbe wa Kamati kuu ya chama hicho.
Timu ya kuandaa mpango huo iliundwa miezi michache iliyopita baada ya kujitokeza fursa ya marekebisho hayo kutokana na Rais Kikwete kutoa ahadi kupitia hotuba yake ya kuongeza uwakilishi wa wanawake bungeni kuwa 50 kwa 50.
Timu hiyo ilifanikiwa kushawishi wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho kuweka pembeni mapendekezo mengine ya Kamati ya Dr Ghalib Billal ambayo iliundwa baadaye kuchambua kuhusu suala hilo.
Kamati hiyo ilikuja na mapendekezo mbalimbali ikiwemo kupanua idadi ya wanawake katika uwakilishi wa uwiano kuwa na orodha yenye uwiano wa majina kijinsia. Aidha pendekezo lingine la kamati hiyo lilitaka uchaguzi uhusishe wagombea wawili mwanamke na mwanaume katika majimbo ya uchaguzi na kupunguza majimbo ya sasa.
Mfumo huu mpya unatarajiwa kupata upinzani mkali toka kwa makundi ya kijamii mathalani walemavu na asasi za kiraia.
Unajua mfumo wa sasa wa viti maalum, unatoa fursa ya uwakilishi wa makundi maalum ya wanawake. Kwa mfano, mimi nimechaguliwa kuwakilisha kundi la walemavu. Lakini kwa marekebisho hayo yanayopendekezwa, nitatakiwa nikagombee katika jimbo la uchaguzi. Tunaweza tukapoteza kabisa uwakilishi wa makundi mbalimbali bungeni, alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake.
Chini ya mfumo mpya hakutakuwa na viti maalum vya makundi kama vijana, walemavu, wawikilishi wa elimu ya juu na mashirika yasiyo ya kiserikali ambavyo vimekuwa vikitengwa na vyama kutokana na uwingi wa viti ambavyo chama kimepata.
Makubaliano hayo ya Kamati Kuu yanatarajiwa kuzua mjadala mkali katika kikao cha NEC kutoka kwa wabunge wa majimbo kuhusu hadhi yao katika mfumo mpya.
Inabidi tuelezwe wazi, kati ya wabunge wa wilaya, na wabunge wa majimbo. Ni nani watakuwa na hadhi na mamlaka zaidi chini ya marekebisho hayo, alisema mbunge machachari wa kanda ya ziwa akitoa maoni yake kuhusu uamuzi wa NEC.
Chini ya mapendekezo hayo, mathalani wilaya kama Ilala yenye majimbo mawili ya Ukonga na Ilala itakuwa na wabunge watatu; Mbunge wa Wilaya ya Ilala ambaye atakuwa ni Mwanamke na Wabunge wawili wa majimbo ya Ilala na Ukonga ambao watakuwa ni wa jinsia yoyote.
Hata hivyo, ili kupunguza mjadala katika jamii kuhusu mkakati huo, tayari Mkuu wa Mawasiliano ikulu amekabidhiwa jukumu la kuundaa umma kukubaliana na marekebisho hayo kupitia propaganda za vyombo vya habari.
Kama sehemu ya propaganda hizo imekubaliwa kwamba habari maalum zitolewe na vyombo vya habari kabla zikieleza kwamba marekebisho hayo yanalenga kuundoa migogoro katika vyama vya siasa inayotokana na upendeleo katika uteuzi wa viti maalum kwa kuweka mfumo huu mpya ambao utafanya wanawake washindane wenyewe kwa wenyewe.
Habari hizo zitaeleza kwamba CHADEMA ni mfano dhahiri wa migogoro hiyo ya upendeleo wa viti maalum ambayo serikali ya CCM inalenga kuindoa kwa kufanya marekebisho hayo ya katiba ya nchi na sheria za uchaguzi katika upatikanaji wa wabunge wa viti maalum.
Changamoto kubwa kwa serikali inatabaki kutumiza ahadi ya kuwa na wabunge kwenye uwiano wa 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume, ahadi ambayo mfumo huu mpya hauwezi kuitekeleza badala yake mfumo huo umeondoa mfumo wa kuthamini kura ambao umekuwa ukitumika katika nchi mbalimbali.
PM

Last edited by a moderator: