Elections 2010 CCM kubadili sheria ya uchaguzi 2010 kujinufaisha?

Paparazi Muwazi

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
310
79
CCM yaizidi kete CHADEMA, yabuni mbinu ya kupunguza wabunge wa upinzani

CCM imebuni kete mpya ya kuizidi CHADEMA na kupunguza nguvu ya upinzani bungeni. Katika mkakati huo mpya ambao umeshapata baraka ya kamati kuu ya chama hicho ukisubiri kupitishwa na NEC hivi karibuni, katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho kuweza kutekeleza mkakati huo. Chini ya marekebisho hayo, wabunge wa viti maalum hawatapatikana kwa kuteuliwa na vyama bali watagombea kupitia wilaya ambazo ndizo zitakazo kuwa majimbo ya wanawake pekee. Chini ya mfumo huo mpya, patakuwa na majimbo ya kawaida 232 ambayo yatagombewa na watu wote kwa kama ilivyo utaratibu wa sasa. Kwa upande mwingine viti maalum vya wanawake pekee 75 vitaondolewa na badala yake wanawake watagombea wenyewe kwenye wilaya 130 za Tanzania. Kwa hali hiyo, kutakuwa na ongezeko la wabunge ambalo litalazimisha taifa kupanua tena ukumbi wa bunge na pia bajeti ya matumizi ya wabunge ya mishahara na posho itabidi iongeze kwa zaidi ya bilioni 50. Kwa idadi hiyo ya wabunge, Tanzania itaingia katika kundi la nchi zenye wabunge wengi zaidi.

Mkakati huo umebuniwa kupunguza nguvu za kambi ya upinzani hususani CHADEMA ambayo imepata kutokana na kupata wabunge wengi wa viti maalum kutokana na idadi ya kura ambazo chama hicho na vingine vya upinzani vimeokoteza nchi nzima.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 CHADEMA ilipata wabunge watano tu wa kuchaguliwa lakini ikapata wabunge wa viti maalum sita kutokana na kura ambazo chama hicho kilipata katika uchaguzi. Kama viti maalum vingetolewa kwa idadi ya viti ambavyo chama kimepata chama hicho kingepata kiti maalum kimoja au viwili tu.

“Unajua tumeweka sheria inayoisaidia CHADEMA, hawa chini ya Operesheni Sangara hata kama tukitumia nguvu kushinda majimbo bado watapata zaidi ya asilimia 20-40 ya kura katika majimbo mbalimbali hali itayofanya wapate kati ya wabunge 15 mpaka 30 wa viti maalum mwaka 2010. Lazima tutafute njia ya kuwadhibiti mapema kwa kubadili sheria”, alinukuliwa mmoja wa wajumbe wa Kamati kuu ya chama hicho.

Timu ya kuandaa mpango huo iliundwa miezi michache iliyopita baada ya kujitokeza fursa ya marekebisho hayo kutokana na Rais Kikwete kutoa ahadi kupitia hotuba yake ya kuongeza uwakilishi wa wanawake bungeni kuwa 50 kwa 50.

Timu hiyo ilifanikiwa kushawishi wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho kuweka pembeni mapendekezo mengine ya Kamati ya Dr Ghalib Billal ambayo iliundwa baadaye kuchambua kuhusu suala hilo.

Kamati hiyo ilikuja na mapendekezo mbalimbali ikiwemo kupanua idadi ya wanawake katika uwakilishi wa uwiano kuwa na orodha yenye uwiano wa majina kijinsia. Aidha pendekezo lingine la kamati hiyo lilitaka uchaguzi uhusishe wagombea wawili mwanamke na mwanaume katika majimbo ya uchaguzi na kupunguza majimbo ya sasa.

Mfumo huu mpya unatarajiwa kupata upinzani mkali toka kwa makundi ya kijamii mathalani walemavu na asasi za kiraia.

“Unajua mfumo wa sasa wa viti maalum, unatoa fursa ya uwakilishi wa makundi maalum ya wanawake. Kwa mfano, mimi nimechaguliwa kuwakilisha kundi la walemavu. Lakini kwa marekebisho hayo yanayopendekezwa, nitatakiwa nikagombee katika jimbo la uchaguzi. Tunaweza tukapoteza kabisa uwakilishi wa makundi mbalimbali bungeni”, alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Chini ya mfumo mpya hakutakuwa na viti maalum vya makundi kama vijana, walemavu, wawikilishi wa elimu ya juu na mashirika yasiyo ya kiserikali ambavyo vimekuwa vikitengwa na vyama kutokana na uwingi wa viti ambavyo chama kimepata.

Makubaliano hayo ya Kamati Kuu yanatarajiwa kuzua mjadala mkali katika kikao cha NEC kutoka kwa wabunge wa majimbo kuhusu hadhi yao katika mfumo mpya.

“Inabidi tuelezwe wazi, kati ya wabunge wa wilaya, na wabunge wa majimbo. Ni nani watakuwa na hadhi na mamlaka zaidi chini ya marekebisho hayo”, alisema mbunge machachari wa kanda ya ziwa akitoa maoni yake kuhusu uamuzi wa NEC.

Chini ya mapendekezo hayo, mathalani wilaya kama Ilala yenye majimbo mawili ya Ukonga na Ilala itakuwa na wabunge watatu; Mbunge wa Wilaya ya Ilala ambaye atakuwa ni Mwanamke na Wabunge wawili wa majimbo ya Ilala na Ukonga ambao watakuwa ni wa jinsia yoyote.

Hata hivyo, ili kupunguza mjadala katika jamii kuhusu mkakati huo, tayari Mkuu wa Mawasiliano ikulu amekabidhiwa jukumu la kuundaa umma kukubaliana na marekebisho hayo kupitia propaganda za vyombo vya habari.

Kama sehemu ya propaganda hizo imekubaliwa kwamba habari maalum zitolewe na vyombo vya habari kabla zikieleza kwamba marekebisho hayo yanalenga kuundoa migogoro katika vyama vya siasa inayotokana na upendeleo katika uteuzi wa viti maalum kwa kuweka mfumo huu mpya ambao utafanya wanawake washindane wenyewe kwa wenyewe.

Habari hizo zitaeleza kwamba CHADEMA ni mfano dhahiri wa migogoro hiyo ya upendeleo wa viti maalum ambayo serikali ya CCM inalenga kuindoa kwa kufanya marekebisho hayo ya katiba ya nchi na sheria za uchaguzi katika upatikanaji wa wabunge wa viti maalum.

Changamoto kubwa kwa serikali inatabaki kutumiza ahadi ya kuwa na wabunge kwenye uwiano wa 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume, ahadi ambayo mfumo huu mpya hauwezi kuitekeleza badala yake mfumo huo umeondoa mfumo wa kuthamini kura ambao umekuwa ukitumika katika nchi mbalimbali.

PM
 
Last edited by a moderator:
Mhh kwa nchi masikini kama TZ ni hatari kidogo, mfano jiji kama Dar, kuna Meya wa Jiji, Meya wa Kila manispaa, Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Jiji,Wabunge wa Majimbo, na wawepo tena Wabunge kutoka wilayani wanawake. Ni ngumu kiasi fulani, nani anakuwa na madaraka kwa nani?. Hivi hizi gharama zote ni kwa kuwa wananchi wanatuona hatuna jinsi ama ni kiburi. Sasa kulipa wabunge wote hao, waliopo tu ni wengi na mishahara na marupurupu wapatayo. Kama hilo laja kuna kazi.
 
Kumbe.. nilisikia serikali wanataka kuongoza mabadiliko ya Katiba mwakani.. nilidhani kutokana na yale tunayoyazungumzia (urais, uwaziri mkuu n.k) kumbe wenzetu wanataka kuleta siasa tena kwenye Katiba..?
 
Waache CCM waendekeze mambo ya kipuuzi!

Kwa mtu mwenye akili, wakati wa mpito kama huu angeutumia kujenga misingi ya uongozi wa taifa ambayo haiyumbi. Na hiyo inawezekana tu kwa kuwa na KATIBA imara ambayo imepatikana kwa ridhaa ya makundi mbalimabli katika jamii. Sasa hii habari ya kuwindana, wajue siku wakikaa pembeni itawarudi! Wana nafasi ya kuleta mabadiliko ya maana kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu na watoto/wajukuu wetu ila wanag'ang'ania ulaji na ufisadi. Hii ni kutoa nafasi kwa kichaa yeyote ambaye anaweza kupata maradaka kutuharibia nchi. Laiti wangejua hili wakaamka na kuweka maslahi ya taifa kwanza!
 
Kwa CCM lolote la hovyo laweza kupangwa ili mradi tu liwe ni kwa lengo la kuwasaidia kushinda uchaguzi na kuishi madarakani bila kupata changamoto.

Lakini ole wetu Tanzania. Watoto wetu na wajukuu watakuja kufukua makaburi yetu waangalie tulikuwa na vichwa vya aina gani.
 
Hii sasa mpya.

Kazi tunayo kwa kweli. Wenzao wanajaribu kubuni mbinu za jinsi watakavyopunguza umaskini na kuongeza pato la serikali wao wanafikiri ni namna gani wataua upinzani na kutumia kale kakeki kadogo tulichonacho.

This is a shame for a "Poor" country like us. We need leaders with vision.
Kama hii habari inaukweli basi nachelea kusema CCM ya Leo haina "Viongozi wa wananchi" ila "Viunguzi (Burners) wa wananchi"

Aluta Kontinua
 
CCM yaizidi kete CHADEMA, yabuni mbinu ya kupunguza wabunge wa upinzani

CCM imebuni kete mpya ya kuizidi CHADEMA na kupunguza nguvu ya upinzani bungeni. Katika mkakati huo mpya ambao umeshapata baraka ya kamati kuu ya chama hicho ukisubiri kupitishwa na NEC hivi karibuni, katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho kuweza kutekeleza mkakati huo. Chini ya marekebisho hayo, wabunge wa viti maalum hawatapatikana kwa kuteuliwa na vyama bali watagombea kupitia wilaya ambazo ndizo zitakazo kuwa majimbo ya wanawake pekee. Chini ya mfumo huo mpya, patakuwa na majimbo ya kawaida 232 ambayo yatagombewa na watu wote kwa kama ilivyo utaratibu wa sasa. Kwa upande mwingine viti maalum vya wanawake pekee 75 vitaondolewa na badala yake wanawake watagombea wenyewe kwenye wilaya 130 za Tanzania. Kwa hali hiyo, kutakuwa na ongezeko la wabunge ambalo litalazimisha taifa kupanua tena ukumbi wa bunge na pia bajeti ya matumizi ya wabunge ya mishahara na posho itabidi iongeze kwa zaidi ya bilioni 50. Kwa idadi hiyo ya wabunge, Tanzania itaingia katika kundi la nchi zenye wabunge wengi zaidi.

Mkakati huo umebuniwa kupunguza nguvu za kambi ya upinzani hususani CHADEMA ambayo imepata kutokana na kupata wabunge wengi wa viti maalum kutokana na idadi ya kura ambazo chama hicho na vingine vya upinzani vimeokoteza nchi nzima.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 CHADEMA ilipata wabunge watano tu wa kuchaguliwa lakini ikapata wabunge wa viti maalum sita kutokana na kura ambazo chama hicho kilipata katika uchaguzi. Kama viti maalum vingetolewa kwa idadi ya viti ambavyo chama kimepata chama hicho kingepata kiti maalum kimoja au viwili tu.

“Unajua tumeweka sheria inayoisaidia CHADEMA, hawa chini ya Operesheni Sangara hata kama tukitumia nguvu kushinda majimbo bado watapata zaidi ya asilimia 20-40 ya kura katika majimbo mbalimbali hali itayofanya wapate kati ya wabunge 15 mpaka 30 wa viti maalum mwaka 2010. Lazima tutafute njia ya kuwadhibiti mapema kwa kubadili sheria”, alinukuliwa mmoja wa wajumbe wa Kamati kuu ya chama hicho.

Timu ya kuandaa mpango huo iliundwa miezi michache iliyopita baada ya kujitokeza fursa ya marekebisho hayo kutokana na Rais Kikwete kutoa ahadi kupitia hotuba yake ya kuongeza uwakilishi wa wanawake bungeni kuwa 50 kwa 50.

Timu hiyo ilifanikiwa kushawishi wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho kuweka pembeni mapendekezo mengine ya Kamati ya Dr Ghalib Billal ambayo iliundwa baadaye kuchambua kuhusu suala hilo.

Kamati hiyo ilikuja na mapendekezo mbalimbali ikiwemo kupanua idadi ya wanawake katika uwakilishi wa uwiano kuwa na orodha yenye uwiano wa majina kijinsia. Aidha pendekezo lingine la kamati hiyo lilitaka uchaguzi uhusishe wagombea wawili mwanamke na mwanaume katika majimbo ya uchaguzi na kupunguza majimbo ya sasa.

Mfumo huu mpya unatarajiwa kupata upinzani mkali toka kwa makundi ya kijamii mathalani walemavu na asasi za kiraia.

“Unajua mfumo wa sasa wa viti maalum, unatoa fursa ya uwakilishi wa makundi maalum ya wanawake. Kwa mfano, mimi nimechaguliwa kuwakilisha kundi la walemavu. Lakini kwa marekebisho hayo yanayopendekezwa, nitatakiwa nikagombee katika jimbo la uchaguzi. Tunaweza tukapoteza kabisa uwakilishi wa makundi mbalimbali bungeni”, alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Chini ya mfumo mpya hakutakuwa na viti maalum vya makundi kama vijana, walemavu, wawikilishi wa elimu ya juu na mashirika yasiyo ya kiserikali ambavyo vimekuwa vikitengwa na vyama kutokana na uwingi wa viti ambavyo chama kimepata.

Makubaliano hayo ya Kamati Kuu yanatarajiwa kuzua mjadala mkali katika kikao cha NEC kutoka kwa wabunge wa majimbo kuhusu hadhi yao katika mfumo mpya.

“Inabidi tuelezwe wazi, kati ya wabunge wa wilaya, na wabunge wa majimbo. Ni nani watakuwa na hadhi na mamlaka zaidi chini ya marekebisho hayo”, alisema mbunge machachari wa kanda ya ziwa akitoa maoni yake kuhusu uamuzi wa NEC.

Chini ya mapendekezo hayo, mathalani wilaya kama Ilala yenye majimbo mawili ya Ukonga na Ilala itakuwa na wabunge watatu; Mbunge wa Wilaya ya Ilala ambaye atakuwa ni Mwanamke na Wabunge wawili wa majimbo ya Ilala na Ukonga ambao watakuwa ni wa jinsia yoyote.

Hata hivyo, ili kupunguza mjadala katika jamii kuhusu mkakati huo, tayari Mkuu wa Mawasiliano ikulu amekabidhiwa jukumu la kuundaa umma kukubaliana na marekebisho hayo kupitia propaganda za vyombo vya habari.

Kama sehemu ya propaganda hizo imekubaliwa kwamba habari maalum zitolewe na vyombo vya habari kabla zikieleza kwamba marekebisho hayo yanalenga kuundoa migogoro katika vyama vya siasa inayotokana na upendeleo katika uteuzi wa viti maalum kwa kuweka mfumo huu mpya ambao utafanya wanawake washindane wenyewe kwa wenyewe.

Habari hizo zitaeleza kwamba CHADEMA ni mfano dhahiri wa migogoro hiyo ya upendeleo wa viti maalum ambayo serikali ya CCM inalenga kuindoa kwa kufanya marekebisho hayo ya katiba ya nchi na sheria za uchaguzi katika upatikanaji wa wabunge wa viti maalum.

Changamoto kubwa kwa serikali inatabaki kutumiza ahadi ya kuwa na wabunge kwenye uwiano wa 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume, ahadi ambayo mfumo huu mpya hauwezi kuitekeleza badala yake mfumo huo umeondoa mfumo wa kuthamini kura ambao umekuwa ukitumika katika nchi mbalimbali.

PM

Lipo Kabila moja hapa nchini wana msemo unasema kwamba unapomuombea kifo mama yako wa kambo, hapo ndipo mama yako anapokufa. Sijui utasemaje na utajisikiaje. Pole sisiemu.
 
huo ndio mwanzo wa mwisho wao.Yani mizigo yote hii wanayo bebesha wananchi bado tu hawashtuki?? waache waendelee kutuchosha ili tupate hasira za kutosha kuwa kataa milele....
 
Huu ni upuuzi mtupu yaani changamoto zote hizi ambazo nchi inazikabili kwa sasa cha maana wanachoweza kufanya ni hiki? Yaani wao lengo lao wao siku zote ni uchaguzi. Zipo sheria nyingi zilizopitwa na wakati kama ile ya vyombo vya habari, udhaifu wa tume ya uchaguzi,uchaguzi wa serekali za mitaa kusimamiwa na Tamisemi chini ya mfumo wa vyama vingi?!! Lakini cha maana wanchoweza kufiliria wao ni namna ya kuidhibiti CHADEMA wanainajisi na kuipindisha katiba wanavyotaka ili waweza kutimiza malengo yao yaliojaa uoga!

CCM wafanya mchezo wa kihuni na utaendelea kulifukarisha taifa letu. Uamuzi wowote wa kuitumia katiba kama nyezo ya kisiasa usikubalike! Upinzani unakuwa kila siku watabadili mangapi ili waudhibiti? hofu kama hizi hazipaswi kuvumuliwa! Katiba ni nyaraka ya kitaifa na si ya kichama kwa kuichezaa namna hii ili iweze kukidhi mahitaji ya chama. Wakiendelea hivyo, na ndivyo watakavyofanya watakuwa wamefanikiwa kulisambaratisha kabisa taifa kwa maana katiba itaonekana kama nyaraka ya CCM na si muongozo wa kitaifa kama inavyopaswa kuwa!

Wanaliingiza taifa katika gharama zisizo za lazima, hata wafanyaje watatoka tu ila kwa kuwa tu wanatoka wasifanye maamuzi ya kijinga kwa kuharibu kila kitu vikiwemo vinavyotuunganisha kama taifa! Wanaelekea kubaya
 
Wewe Mchungaji hayo kasemee huko huko usione kuwa wenzio wamesinzia mbinu hususan za kisiasa haziishi - mapambano kila kukicha.
 
CCM yaizidi kete CHADEMA, yabuni mbinu ya kupunguza wabunge wa upinzani

CCM imebuni kete mpya ya kuizidi CHADEMA na kupunguza nguvu ya upinzani bungeni. Katika mkakati huo mpya ambao umeshapata baraka ya kamati kuu ya chama hicho ukisubiri kupitishwa na NEC hivi karibuni, katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho kuweza kutekeleza mkakati huo. Chini ya marekebisho hayo, wabunge wa viti maalum hawatapatikana kwa kuteuliwa na vyama bali watagombea kupitia wilaya ambazo ndizo zitakazo kuwa majimbo ya wanawake pekee. Chini ya mfumo huo mpya, patakuwa na majimbo ya kawaida 232 ambayo yatagombewa na watu wote kwa kama ilivyo utaratibu wa sasa. Kwa upande mwingine viti maalum vya wanawake pekee 75 vitaondolewa na badala yake wanawake watagombea wenyewe kwenye wilaya 130 za Tanzania. Kwa hali hiyo, kutakuwa na ongezeko la wabunge ambalo litalazimisha taifa kupanua tena ukumbi wa bunge na pia bajeti ya matumizi ya wabunge ya mishahara na posho itabidi iongeze kwa zaidi ya bilioni 50. Kwa idadi hiyo ya wabunge, Tanzania itaingia katika kundi la nchi zenye wabunge wengi zaidi.

Mkakati huo umebuniwa kupunguza nguvu za kambi ya upinzani hususani CHADEMA ambayo imepata kutokana na kupata wabunge wengi wa viti maalum kutokana na idadi ya kura ambazo chama hicho na vingine vya upinzani vimeokoteza nchi nzima.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 CHADEMA ilipata wabunge watano tu wa kuchaguliwa lakini ikapata wabunge wa viti maalum sita kutokana na kura ambazo chama hicho kilipata katika uchaguzi. Kama viti maalum vingetolewa kwa idadi ya viti ambavyo chama kimepata chama hicho kingepata kiti maalum kimoja au viwili tu.

“Unajua tumeweka sheria inayoisaidia CHADEMA, hawa chini ya Operesheni Sangara hata kama tukitumia nguvu kushinda majimbo bado watapata zaidi ya asilimia 20-40 ya kura katika majimbo mbalimbali hali itayofanya wapate kati ya wabunge 15 mpaka 30 wa viti maalum mwaka 2010. Lazima tutafute njia ya kuwadhibiti mapema kwa kubadili sheria”, alinukuliwa mmoja wa wajumbe wa Kamati kuu ya chama hicho.

Timu ya kuandaa mpango huo iliundwa miezi michache iliyopita baada ya kujitokeza fursa ya marekebisho hayo kutokana na Rais Kikwete kutoa ahadi kupitia hotuba yake ya kuongeza uwakilishi wa wanawake bungeni kuwa 50 kwa 50.

Timu hiyo ilifanikiwa kushawishi wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho kuweka pembeni mapendekezo mengine ya Kamati ya Dr Ghalib Billal ambayo iliundwa baadaye kuchambua kuhusu suala hilo.

Kamati hiyo ilikuja na mapendekezo mbalimbali ikiwemo kupanua idadi ya wanawake katika uwakilishi wa uwiano kuwa na orodha yenye uwiano wa majina kijinsia. Aidha pendekezo lingine la kamati hiyo lilitaka uchaguzi uhusishe wagombea wawili mwanamke na mwanaume katika majimbo ya uchaguzi na kupunguza majimbo ya sasa.

Mfumo huu mpya unatarajiwa kupata upinzani mkali toka kwa makundi ya kijamii mathalani walemavu na asasi za kiraia.

“Unajua mfumo wa sasa wa viti maalum, unatoa fursa ya uwakilishi wa makundi maalum ya wanawake. Kwa mfano, mimi nimechaguliwa kuwakilisha kundi la walemavu. Lakini kwa marekebisho hayo yanayopendekezwa, nitatakiwa nikagombee katika jimbo la uchaguzi. Tunaweza tukapoteza kabisa uwakilishi wa makundi mbalimbali bungeni”, alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Chini ya mfumo mpya hakutakuwa na viti maalum vya makundi kama vijana, walemavu, wawikilishi wa elimu ya juu na mashirika yasiyo ya kiserikali ambavyo vimekuwa vikitengwa na vyama kutokana na uwingi wa viti ambavyo chama kimepata.

Makubaliano hayo ya Kamati Kuu yanatarajiwa kuzua mjadala mkali katika kikao cha NEC kutoka kwa wabunge wa majimbo kuhusu hadhi yao katika mfumo mpya.

“Inabidi tuelezwe wazi, kati ya wabunge wa wilaya, na wabunge wa majimbo. Ni nani watakuwa na hadhi na mamlaka zaidi chini ya marekebisho hayo”, alisema mbunge machachari wa kanda ya ziwa akitoa maoni yake kuhusu uamuzi wa NEC.

Chini ya mapendekezo hayo, mathalani wilaya kama Ilala yenye majimbo mawili ya Ukonga na Ilala itakuwa na wabunge watatu; Mbunge wa Wilaya ya Ilala ambaye atakuwa ni Mwanamke na Wabunge wawili wa majimbo ya Ilala na Ukonga ambao watakuwa ni wa jinsia yoyote.

Hata hivyo, ili kupunguza mjadala katika jamii kuhusu mkakati huo, tayari Mkuu wa Mawasiliano ikulu amekabidhiwa jukumu la kuundaa umma kukubaliana na marekebisho hayo kupitia propaganda za vyombo vya habari.

Kama sehemu ya propaganda hizo imekubaliwa kwamba habari maalum zitolewe na vyombo vya habari kabla zikieleza kwamba marekebisho hayo yanalenga kuundoa migogoro katika vyama vya siasa inayotokana na upendeleo katika uteuzi wa viti maalum kwa kuweka mfumo huu mpya ambao utafanya wanawake washindane wenyewe kwa wenyewe.

Habari hizo zitaeleza kwamba CHADEMA ni mfano dhahiri wa migogoro hiyo ya upendeleo wa viti maalum ambayo serikali ya CCM inalenga kuindoa kwa kufanya marekebisho hayo ya katiba ya nchi na sheria za uchaguzi katika upatikanaji wa wabunge wa viti maalum.

Changamoto kubwa kwa serikali inatabaki kutumiza ahadi ya kuwa na wabunge kwenye uwiano wa 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume, ahadi ambayo mfumo huu mpya hauwezi kuitekeleza badala yake mfumo huo umeondoa mfumo wa kuthamini kura ambao umekuwa ukitumika katika nchi mbalimbali.

PM

Asant sana kwa post hii. Nimewahi kusema katika mikutano yangu mbalimbali kuwa CCM ipo tayari kufanya lolote ili kubakia madarakani. Lolote lile. Hii ya kubadili katiba na kuweka Majimbo ya Wanawake haiimarishi demokrasia hata kidogo. Kuna umuhimu mkubwa wa kuingiza katika mfumo wetu wa uchaguzi aina fulani ya uwakilishi wa uwiano (Proportionality) ili kuhakikisha kuwa kura hazipotei. Kila kura ina thamani ni vema kuithaminisha kwa viti Bungeni. Uwakilishi wa uwiano ukiwa na viti vya kutosha utatoa fursa ya kuruhusu wagombea binafsi katika majimbo. CCM inashagaza sana kutaka kubadili katiba kwa sababu tu ya kuiogopa CHADEMA
 
Kaka,
usiwashangae CCM,hawa watu wameshafanya mengi kuua upinzani!!!this time badala ya kuwashangaa, inabidi kuwakemea na kuipinga kwa nguvu kazi hii ya kishetani!!!!!nyie ndo wabunge mpo wachache lakini mkisema hopefully jamii itatuelewa
 
Hili suala sio la kuwaachia upinzani peke yake. Sio suala la kuwaachia akina Zitto na Hamad. Ni suala la watanzania wote. Suala la uwakilishi kwa uwiano wa kura ni suala la msingi linalogusa makundi yote ya watanzania. Kila chama kiwe na uwakilishiwi kulingana na idadi ya kura zilizopigwa. Watanzania tuamke na kukemea mkakati huu utakaodumaza demokrasia hapa nchini na kuliongezea taifa mzigo mkubwa wa kuwalipa watu ambao hawana tija katika maendeleo ya taifa hili.
 
Paparazi asante sana kwa hili .Umenifanya nisinyae kwa kweli na sina la kusema.Yaani CCM kweli wanataka kufanya hili na kuongeza walaji wengine Bungeni ? Nilitegemea hata waje na wazo la kuwapunguza watu kule jumbani lakini ndiyo wanaamua kuua kabisa ? Jamani hii si hujuma kwa Nchi kama EPA na Richmond ? JK hizi ndizo busara zake ?
 
CCM yaizidi kete CHADEMA, yabuni mbinu ya kupunguza wabunge wa upinzani

CCM imebuni kete mpya ya kuizidi CHADEMA na kupunguza nguvu ya upinzani bungeni. Katika mkakati huo mpya ambao umeshapata baraka ya kamati kuu ya chama hicho ukisubiri kupitishwa na NEC hivi karibuni, katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho kuweza kutekeleza mkakati huo. Chini ya marekebisho hayo, wabunge wa viti maalum hawatapatikana kwa kuteuliwa na vyama bali watagombea kupitia wilaya ambazo ndizo zitakazo kuwa majimbo ya wanawake pekee. Chini ya mfumo huo mpya, patakuwa na majimbo ya kawaida 232 ambayo yatagombewa na watu wote kwa kama ilivyo utaratibu wa sasa. Kwa upande mwingine viti maalum vya wanawake pekee 75 vitaondolewa na badala yake wanawake watagombea wenyewe kwenye wilaya 130 za Tanzania. Kwa hali hiyo, kutakuwa na ongezeko la wabunge ambalo litalazimisha taifa kupanua tena ukumbi wa bunge na pia bajeti ya matumizi ya wabunge ya mishahara na posho itabidi iongeze kwa zaidi ya bilioni 50. Kwa idadi hiyo ya wabunge, Tanzania itaingia katika kundi la nchi zenye wabunge wengi zaidi.

Mkakati huo umebuniwa kupunguza nguvu za kambi ya upinzani hususani CHADEMA ambayo imepata kutokana na kupata wabunge wengi wa viti maalum kutokana na idadi ya kura ambazo chama hicho na vingine vya upinzani vimeokoteza nchi nzima.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 CHADEMA ilipata wabunge watano tu wa kuchaguliwa lakini ikapata wabunge wa viti maalum sita kutokana na kura ambazo chama hicho kilipata katika uchaguzi. Kama viti maalum vingetolewa kwa idadi ya viti ambavyo chama kimepata chama hicho kingepata kiti maalum kimoja au viwili tu.

“Unajua tumeweka sheria inayoisaidia CHADEMA, hawa chini ya Operesheni Sangara hata kama tukitumia nguvu kushinda majimbo bado watapata zaidi ya asilimia 20-40 ya kura katika majimbo mbalimbali hali itayofanya wapate kati ya wabunge 15 mpaka 30 wa viti maalum mwaka 2010. Lazima tutafute njia ya kuwadhibiti mapema kwa kubadili sheria”, alinukuliwa mmoja wa wajumbe wa Kamati kuu ya chama hicho.

Timu ya kuandaa mpango huo iliundwa miezi michache iliyopita baada ya kujitokeza fursa ya marekebisho hayo kutokana na Rais Kikwete kutoa ahadi kupitia hotuba yake ya kuongeza uwakilishi wa wanawake bungeni kuwa 50 kwa 50.

Timu hiyo ilifanikiwa kushawishi wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho kuweka pembeni mapendekezo mengine ya Kamati ya Dr Ghalib Billal ambayo iliundwa baadaye kuchambua kuhusu suala hilo.

Kamati hiyo ilikuja na mapendekezo mbalimbali ikiwemo kupanua idadi ya wanawake katika uwakilishi wa uwiano kuwa na orodha yenye uwiano wa majina kijinsia. Aidha pendekezo lingine la kamati hiyo lilitaka uchaguzi uhusishe wagombea wawili mwanamke na mwanaume katika majimbo ya uchaguzi na kupunguza majimbo ya sasa.

Mfumo huu mpya unatarajiwa kupata upinzani mkali toka kwa makundi ya kijamii mathalani walemavu na asasi za kiraia.

“Unajua mfumo wa sasa wa viti maalum, unatoa fursa ya uwakilishi wa makundi maalum ya wanawake. Kwa mfano, mimi nimechaguliwa kuwakilisha kundi la walemavu. Lakini kwa marekebisho hayo yanayopendekezwa, nitatakiwa nikagombee katika jimbo la uchaguzi. Tunaweza tukapoteza kabisa uwakilishi wa makundi mbalimbali bungeni”, alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka kutajwa jina lake.

Chini ya mfumo mpya hakutakuwa na viti maalum vya makundi kama vijana, walemavu, wawikilishi wa elimu ya juu na mashirika yasiyo ya kiserikali ambavyo vimekuwa vikitengwa na vyama kutokana na uwingi wa viti ambavyo chama kimepata.

Makubaliano hayo ya Kamati Kuu yanatarajiwa kuzua mjadala mkali katika kikao cha NEC kutoka kwa wabunge wa majimbo kuhusu hadhi yao katika mfumo mpya.

“Inabidi tuelezwe wazi, kati ya wabunge wa wilaya, na wabunge wa majimbo. Ni nani watakuwa na hadhi na mamlaka zaidi chini ya marekebisho hayo”, alisema mbunge machachari wa kanda ya ziwa akitoa maoni yake kuhusu uamuzi wa NEC.

Chini ya mapendekezo hayo, mathalani wilaya kama Ilala yenye majimbo mawili ya Ukonga na Ilala itakuwa na wabunge watatu; Mbunge wa Wilaya ya Ilala ambaye atakuwa ni Mwanamke na Wabunge wawili wa majimbo ya Ilala na Ukonga ambao watakuwa ni wa jinsia yoyote.

Hata hivyo, ili kupunguza mjadala katika jamii kuhusu mkakati huo, tayari Mkuu wa Mawasiliano ikulu amekabidhiwa jukumu la kuundaa umma kukubaliana na marekebisho hayo kupitia propaganda za vyombo vya habari.

Kama sehemu ya propaganda hizo imekubaliwa kwamba habari maalum zitolewe na vyombo vya habari kabla zikieleza kwamba marekebisho hayo yanalenga kuundoa migogoro katika vyama vya siasa inayotokana na upendeleo katika uteuzi wa viti maalum kwa kuweka mfumo huu mpya ambao utafanya wanawake washindane wenyewe kwa wenyewe.

Habari hizo zitaeleza kwamba CHADEMA ni mfano dhahiri wa migogoro hiyo ya upendeleo wa viti maalum ambayo serikali ya CCM inalenga kuindoa kwa kufanya marekebisho hayo ya katiba ya nchi na sheria za uchaguzi katika upatikanaji wa wabunge wa viti maalum.

Changamoto kubwa kwa serikali inatabaki kutumiza ahadi ya kuwa na wabunge kwenye uwiano wa 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume, ahadi ambayo mfumo huu mpya hauwezi kuitekeleza badala yake mfumo huo umeondoa mfumo wa kuthamini kura ambao umekuwa ukitumika katika nchi mbalimbali.

PM

Mzee wa Data

Maamuzi gani yamefikiwa kuhusu pendekezo hili la kamati kuu?

PM
 
Ama kweli kazi ipo!
Hapa hoja ni vinatakiwa viti maalum kama wawakilishi wa wanawake Bungeni...
CCM wana Umoja wa wanawake (UWT) ktk kila mkoa na wilaya zake hivyo kuna urahisi kwao, wakati vyama vya Upizani hata ofisi ya chama tu wilayani imekuwa shida hii kweli inawezekana jamani?
Ama kweli CCM itaongoza milele!
 
Hizi ni dalili za kufilisika kwa CCM. Badala ya kuhakikisha nchi inakuwa na katiba thabiti inayolinda maslahi ya Watanzania wao wanataka kuhakikisha wanafanya mabadiliko ya katiba ili kulinda maslahi ya chama cha mafisadi. Shame on you CCM! :(
 
Back
Top Bottom