CCM Kubadili Jina ili Kupata Mvuto.

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,713
12,063
Habari za ndani za na za kiintelijensia nilizozipata zinasema, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinampango wa kubadili jina hilo, ili kukiletea mvuto wake wa asili kwa wananchi.
Habari hizo zinazidi kudai kuwa, mchakato utawakilishwa katika siku ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, na mipango ya kutoa mapendekezo ya jina mbadala litakalotumiwa utaanza rasmi ili ikiwezekana litumike katika uchaguzi ujao.

Hali hiyo inatokana na CCM kupoteza umaarufu hivyo kutishia uwezekano wa kupotea katika ulimwengu wa kisiasa ifikapo mwaka 2025.

Hivi sasa CCM inadai kutumia nguvu na rasilimali nyingi katikai kuuza sera zake kwa wananchi, kitu ambacho ni tofauti na chama kikuu cha upinzani CHADEMA.
 
Hata wakijiita FUTUHI moto uko palepale.
 
Hata wakibadili jina, what about the change of orientation? mwenendo wao wataubadili? Kwa hali ilivyo sasa kila mwananchi anataka aishi kwa ujanja, you try to live straight, mambo hayaendi! Wajaribu kurejesha hali ya haki katika kipato....na mengine watazidishiwa!
 
Habari za ndani za na za kiintelijensia nilizozipata zinasema, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinampango wa kubadili jina hilo, ili kukiletea mvuto wake wa asili kwa wananchi.
Habari hizo zinazidi kudai kuwa, mchakato utawakilishwa katika siku ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, na mipango ya kutoa mapendekezo ya jina mbadala litakalotumiwa utaanza rasmi ili ikiwezekana litumike katika uchaguzi ujao.

Hali hiyo inatokana na CCM kupoteza umaarufu hivyo kutishia uwezekano wa kupotea katika ulimwengu wa kisiasa ifikapo mwaka 2025.

Hivi sasa CCM inadai kutumia nguvu na rasilimali nyingi katikai kuuza sera zake kwa wananchi, kitu ambacho ni tofauti na chama kikuu cha upinzani CHADEMA.
Shetani kubadili jina na kujiita malaika hakufanyi ushetani wake kuisha.
 
mmmmh,vpi kuhusu rangi nayo wabadili?,maana siku hzi nguo zenye rangi ya njano na kijani hazinunuliki kabisa hata kama si ya magamba!.
 
Good idea mie nawashauri wakiite CHAMA CHA MAJAMBAZI WAKUU (CCMW). Au CHAMA CHA WACHAKACHUAJI (CCW). Au wakiite kabisa CHAMA CHA VIGOGO NA WATOTO WAO NA MAJAMBAZI WENGINE (CCVWWMW). Hahaha hata wabadili vp chama kishakufa hicho.
 
Hata wajiite Marehemu, eti kwa sababu jina hilo linapotajwa kwa mfu hufuta Mabaya yake, bado wao wataendelea kuwa Magamba tu. Watangulie kuzimu salama.
 
Hapo kwenye red, CCM wanatakiwa waheshimu umma wa Tanzania. Tunaadhimia miaka 50 ya uhuru na si CCM hivyo wasi-hijack hii siku kwa ajili ya siasa zao za uchwara.

Habari hizo zinazidi kudai kuwa, mchakato utawakilishwa katika siku ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru
 
Ila unaweza kuwa mkakati unaowafaa baadhi ya watu. Nakumbuka enzi za ujana wangu kule kijijini mtu mmoja alinyweshwa sumu kijinga hivi hivi. Chupa imeandikwa "sumu ya panya" na jamaa akamwambia kuwa anaweza kubadilisha sumu akibadiilsha label. Na kweli mbele ya macho yake akabadilisha label na kuondoa hiyo ya "sumu ya panya" na kuandika "Maziwa Bora". Kwa vile vyote vilivyopo mle ndani vilikuwa vya rangi nyeupe jamaa - msiniulize kwanini - aliamini kuwa sumu imekuwa maziwa. Akanywa masaa machache baadaye watu walianza kutoa rambirambi.

Wapo watu wanaoweza kuamini kabisa kuwa kubadilisha label kunaweza kubadili kilichomo kama watu vile wapo wanaoamini kuwa kiumbe kinaweza kujivua gamba halafu kikageuka kuwa kiumbe kingine.

So please, hii iwe ni burudani nzuri tu kwa siku ya Ijumaa. TGIF!
 
Yaani wanataka glass mpya lakini mvinyo iwe ile ile? kwa akili zao CCM kweli wanaweza badili jina wakiamini kuwa italeta unafuu wa tuhuma za ufisadi wakiwa wanaendelea na mafisadi wao, MKJJ na watu wengine wamewapa ushauri mzuri tu CCM lakini wao hawasikii na hawabadiliki, hawaangalii alama zilizo ukutani, hata wakiona hizo alama hawachukui hatua yoyote...

Tusubiri mwisho wa siku wanainchi ndio watakaoamua mstakabari wao/CCM na si dola au katiba wanayolingia hivi sasa, Angalia mfano jana mtu mzima Mukama na akili zake anadai eti Chadema imeingiza makamandoo Igunga kutoka Pakistan etc ..upuuzi mtupu unatoka mdomoni mwa baba aliye na wajukuu,mtu mzima hana aibu kuongea uongo, utafikiri anaongea na wajukuu wake?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom