Emmanuel J. Buyamba
JF-Expert Member
- May 24, 2013
- 1,167
- 651
Ni kupitia Star tv habari usiku huu saa mbili.M/kiti wa kundi la Tanzania kwanza (nje ya bunge) linaloundwa na CCM ndg Matefu kasema wamepanga kuandamana ili kumshinikiza balozi wa Ujerumani nchini kuzikemea taasisi za kijerumani wanazozihisi kwamba zinavuruga mchakato wa katiba mpya nchini.MY TAKE;Kweli nchi hii ni kichwa cha mwendawazimu. Wapinzani wanaandamana dhidi ya serikali,serikali nayo kupitia chama chake inapanga kuandamana badala ya kuchukua hatua.Sijui ile kauli ya watawala kuwa maandamano yanavuruga amani imeishia wapi.Kila la kheri CCM ila mjihadhari na vitu vya ncha kali.