CCM komaeni mafisadi yatawatoa Ikulu na si CHADEMA

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,404
Wananchi wakikosa huduma bora, wakikosa haki watakilaumu chama tawala. Lakini ukitizama kwa haraka haraka wanaowakosesha huduma wananchi si wana ccm ni watu baki tu tena wasiokuwa na chembe ya ushawishi wa kisiasa.

Hebu ona majipu haya yanayotumbuliwa ukiondoa wabunge njaa wachache wengine wote hawana uhusiano na chama tawala. Ona madaktari wananyanyasa wagonjwa wala hawana itikadi zozote za kisiasa. Ona watu wanapiga hela za umma kuanzia mashirika ya umma hadi bandarini hawana itikadi zozote za kisiasa ni majizi na mashenzi tu ya mtaani.

Ukifika wakati wa uchaguzi ni wana ccm kutwanzima na usiku kucha wanahangaika kubeba spika na kubandika matangazo, makoo yanawakauka kujitetea kwa wananchi kwanini hakuna maendeleo wakati wanaowakosesha wananchi maendeleo wako majumbani na maofisini wametulia muda mwingine wanawaoneni majuha jinsi mishipa inavyowatoka kutetea uozo wa wazi.

Kama mzee Kinana alivyokuwa anahutubia kwa wananchi niwakati sasa wa ccm kuisimamia serikali watu waliopewa dhamana na chama wanapaswa kujieleza ni vipi wamewaletea maendeleo wananchi walioiweka madarakani ccm.

Mtumishi aliyemdhulumu kiwanja kikongwe wala hana uhusiano na ccm lakini yule bibi lazima alie na ccm kwa kuwa ndicho chama alichokichagua kitetee maslahi yake. Kijana anayehangaika kupata mafao yake huku akisoma magazetini watu wamevuta hela za kufa mtu utamshawishije aichague ccm?

Niwakati sasa CCM iweke madawati ya malalamiko watu waweze kujieleza shida zao na chama kiweze kuchukua hatua stahiki.
 
Kama kubwa la mafisadi likisaidiwa na UKAWA lilishindwa kuitoa CCM madarakani itakuwa hawa virambasi?
 
Kama kubwa la mafisadi likisaidiwa na UKAWA lilishindwa kuitoa CCM madarakani itakuwa hawa virambasi?
Itafika wakati wananchi watachoka wataamua liwalo na liwe, hebu fikiria 52% ya watanzania ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35, hawa sawa na 18m kati ya hawa wenye nguvu za kufanyakazi ni 15m wengine ni wanafunzi wagonjwa. kati ya hao ni laki saba tu ndio walioajiriwa.

Kote duniani vijana wengi huajiriwa viwandani, kwa taarifa ya repoa tanzania ina viwanda 50,776. kwa maana nyingine kwa wastani kila kiwanda kimeajiri vijana wasiozidi kumi, hivi ni viashiria kuwa tunakokwenda sio salama.
 
Back
Top Bottom