CCM Kitendo walichomfanyia Sitta si cha kiungwana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Kitendo walichomfanyia Sitta si cha kiungwana

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FUSO, Nov 19, 2010.

 1. F

  FUSO JF-Expert Member

  #1
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  JF,

  Kila nikifikiria kitendo walichomfanyika mwana siasa mkongwe Sitta si cha ki ungwana kabisa, Sitta amekulia CCM na amefanya mengi sana kuifikisha CCM hapo ilipo, leo hii CCM ina ubavu kweli wa kumwondoa kwa mizengwe kiasi kile?

  Hutakiwi kutumia akili nyingi sana kuelewa kwamba huo ulikuwa mpango mahsusi uliondaliwa ingawa waandaaji hawakutumia logic kiasi sisi watanzania tusijue kilichojiri ndani ya chama hiki kikongwe kabisa.

  Wote mtakubaliana na mimi kwamba kosa kubwa sana alilolifanya Sitta ni kuruhusu hoja muhimu za kifisadi ziendelee bungeni pamoja na kubariki uundwaji wa Tume huru ya Bunge kuchunguza ufisadi wa Richmood ambapo matokeo yalifanya Waziri Mkuu wa wakati huo aliachia ngazi.


  Nani asiyejua kwamba sasa CCM imegawanyika makundi mawili? kundi moja likiasisiwa na mafisadi kwenye pesa za ajabu, mbaya zaidi kundi hili lina mizizi mizito hadi kwenye Kamati kuu ya Chama. Mkumbuke kikao cha kumwengua Sita kilikuwa na wajumbe 37 tu.

  CCM wanajaribu kulificha bomu chini ya meza wakidhani halitalipuka, Kitendo cha kuwafanya wana CCM kuwa waoga hata kusimama na kutoa hoja za msingi ni hatari kwa taifa letu.

  Nani asiyejua kwamba CCM sasa ni ka genge ka watu wafisadi ambao wamejificha juu kabisa ya CCM huku wanachama wengine wakiwa chini wanashangilia. hivi unahitaji akili nyingi kweli kujua kwamba Rostam na Lowassa ndiyo vinara wa dili la kumkaanga Sitta?

  Poleni wabunge wa CCM, kwa mlio wachache wenye akili za kuchambua mambo mtakubaliana na mimi kwamba chama chenu hakina nia yoyote ya kumkomboa mwananchi maskini aliye kijijini bali ni kuwatunishia mifuko matajiri wachache ambao wanakula kwa mgogo wa chama chenu.

  nisiwachoshe, ila kumbukeni Bomu MMELIKALIA hilo.
   
Loading...