CCM Kimeumana, sasa Ubungo, Babati, Mbeya na Tabora kurudia Uchaguzi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg Daniel Chongolo amewaagiza makatibu wa Wilaya zilizobainika kuwa na kasoro kwenye mchakato wa uchukuaji wa fomu katika uchaguzi ngazi ya shina kurudia uchukuaji huo maramoja,


Aidha, ameyataja baadhi ya maeneo yaliyobainika kuwa na changamoto hiyo kuwa ni pamoja na Wilaya ya Ubungo, Babati, Mbeya, na Tabora,


Katibu mkuu huyo amesema ni lazima haki itendeke ndani ya Chama kwa wanachama wote bila ubaguzi wa aina yeyote,


Maagizo hayo ameyatoa Aprili, 20, 2022 Dar es Salaam alipokuwa kwenye Mkutano wa Halmashauri ya CCM ya Wilaya ya Ubungo na Kinondoni,

Bila kuwawajibisha waliovuruga zoezi ni dhahiri kutakuwa na facilitation toka juu
 
Huwa ninacheka vibaya sana, ili ccm ijipe matumaini hewa, inabidi iwe inawataja cdm kwenye kila vikao vyao ili kujifariji kuwa cdm haipo. Ikifika uchaguzi inategemea vyombo vya dola kutangazwa washindi!
Aaaaaiiiseee 😀😀😀😀😀😀😀
 
Hongera Sana Ccm-tanzania, ingekuwa wale wenzetu wa zidumu fikra za Mwenyekiti ndio ingekuwa basi tena,

CCM bado ni Chama bora kabisa duania na Africa cha kupigiwa mfano,

Viva CCM, VIVA, VIVA SAMIA VIVA
Wazidumu fikra za Mwenyekiti si ndiyo hao hao unaowapa hongera ....!!

Unahamisha magoli .....!!?
 
Ukiona kuna kuumana kuna watu wanafikiria UBUNGE hivyo wanawapanga watu wa kuwapigia kura za maoni ili wapite hatua za mwanzo za ubunge.
 
Hongera Sana Ccm-tanzania, ingekuwa wale wenzetu wa zidumu fikra za Mwenyekiti ndio ingekuwa basi tena,

CCM bado ni Chama bora kabisa duania na Africa cha kupigiwa mfano,

Viva CCM, VIVA, VIVA SAMIA VIVA
Tunaibiana kura kama tunavyowaibia wapinzani?
 
Back
Top Bottom