CCM Kimeumana, sasa Ubungo, Babati, Mbeya na Tabora kurudia Uchaguzi

ISRAEL JR

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
1,434
625

Chongolo: aagiza uchukuaji fomu za uchaguzi ndani ya CCM urudiwe​

chongolo pic

===

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg Daniel Chongolo amewaagiza makatibu wa Wilaya zilizobainika kuwa na kasoro kwenye mchakato wa uchukuaji wa fomu katika uchaguzi ngazi ya shina kurudia uchukuaji huo maramoja,

Aidha, ameyataja baadhi ya maeneo yaliyobainika kuwa na changamoto hiyo kuwa ni pamoja na Wilaya ya Ubungo, Babati, Mbeya, na Tabora,

Katibu mkuu huyo amesema ni lazima haki itendeke ndani ya Chama kwa wanachama wote bila ubaguzi wa aina yeyote,

Maagizo hayo ameyatoa Aprili, 20, 2022 Dar es Salaam alipokuwa kwenye Mkutano wa Halmashauri ya CCM ya Wilaya ya Ubungo na Kinondoni,

Ndg Chongolo amesisitiza kuwa a chama hicho si mali ya mtu binafsi bali cha wanachama wote bila kujali kabila wala rangi zao,

Nawaagiza Makatibu wa wilaya, Ubungo na wilaya zote nchini,

Pamoja na maeneo yote ambayo tumebaini yana changamoto ya watu kunyimwa kuchukua fomu za kugombea ndani ya chama.

"Tunarudisha utoaji wa fomu upya"

CCM tunataka wale wote wenye dhamira ya kuchukua fomu wachukue bila kuwekewa vizuizi,

Ndg Chongolo aliendelea kusisitiza kwa kusema,

Hiki sio chama cha mtu,

Hiki sio chama cha maslahi binafsi,

Hiki chama ni cha wanachama wote,

Amesema huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho hivyo viongozi wa chama ngazi zote wanapaswa kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho,

Crde Chongolo pia amewataka wanachama kuacha ubinafsi na kuchagua nani wa kuwania nafasi ndani ya chama,

Waache kila mwenye nia ashiriki na wanachama wachague wanayempenda kwa uwazi kabisa,

"Dhamana tulizonazo hazijatupa haki ya kufanya uamuzi kwa ubinafsi"

Maeneo ambayo tumegundua yana hiyo changamoto napiga marufuku kuwanyima fomu wanachama.

Kwanza, naagiza fomu ziendelee kutolewa kwa watu wote,

Pili, uchaguzi usitishwe, wanachama wote wenye nia wapate haki ya kuchukua fomu na kugombea," amesema

Wakati huo huo Katibu mkuu huyo amesema chama hicho hakitasita kusitisha uchaguzi huo kwa ngazi zote za chama,

Ndg Chongolo amewaagiza pia Makatibu wa wilaya nchi nzima kuhakikisha katika chaguzi hizo vitumike vitabu vilivyohakikiwa kupiga kura na sio vinginevyo.

Tunafuatilia na tukibaini kuna maeneo ambapo vitabu vilivyokuwa vimehakikiwa vimeongezwa majina ya watu wasiokuwemo kwenye utaratibu wa daftari la wanachama,

Wakurugenzi au Makatibu wa uchaguzi watawajibika, ameeleza kiongozi huyo,
 
Huwa ninacheka vibaya sana, ili ccm ijipe matumaini hewa, inabidi iwe inawataja cdm kwenye kila vikao vyao ili kujifariji kuwa cdm haipo. Ikifika uchaguzi inategemea vyombo vya dola kutangazwa washindi!
CDM ndio nini? Achana na CCM ni habari nyingine kabisa
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom