CCM Kilolo wampa makavu Waziri

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,597
94,666
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa Bwana Kiliani Myenzi leo amemueleza Waziri wa Viwanda kuwa, Asilimia zaidi ya 80% ama 90% ya Wananchi wa Kilolo mahitaji yao ni Kiwanda cha Chai kufunguliwa na sio Ununuzi wa Ndege ama Ujenzi wa Reli kwani hata hiyo Reli hawaijui, wala hizo ndege hawana uwezo wa kuzipanda.

Naye Waziri wa Viwanda Innocent Bashungwa akitoa ufafanuzi kuhusu kauli hiyo ya Mwenyekiti, amemuonya Mwenyekiti huyo huku akimtaka awe sehemu ya kutangaza Miradi mikubwa inayofanywa na seriakali ya ccm.

Naona sasa somo limeanza kueleweka hata kwa wenye chama chao. Pole pole ndiyo mwendo tutafika tu na shule zetu za kata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuwezi kuwa na wana ccm wasaliti ndani ya chama haiwezekani kama mwenyekiti hajui umuhimu wa ndege na reli huyo uenyekiti haumfai kabisaaa aondoke zake akiache chama salama
 
Huyo mwenyekiti aache ushamba , kama anataka viwanda atoe wazo lake kwa staha, ili lifanyiwe kazi , ndege , reli na vitu vingine vyenye sura pana ya kitaifa na yakimataifa, ni muhimu zaidi kwa maslahi mapana zaidi kwa taifa kwa ujumla wake , hivyo viwanda bila usafiri wa uhakika na miundimbinu madhubuti na ya kisasazaidi bidhaa zitasafirishwaje kumfikia mlaji ? Au malighafi zitafikaje kiwandani ?
 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa Bwana Kiliani Myenzi leo amemueleza Waziri wa Viwanda kuwa, Asilimia zaidi ya 80% ama 90% ya Wananchi wa Kilolo mahitaji yao ni Kiwanda cha Chai kufunguliwa na sio Ununuzi wa Ndege ama Ujenzi wa Reli kwani hata hiyo Reli hawaijui, wala hizo ndege hawana uwezo wa kuzipanda.

Naye Waziri wa Viwanda Innocent Bashungwa akitoa ufafanuzi kuhusu kauli hiyo ya Mwenyekiti, amemuonya Mwenyekiti huyo huku akimtaka awe sehemu ya kutangaza Miradi mikubwa inayofanywa na seriakali ya ccm.

Naona sasa somo limeanza kueleweka hata kwa wenye chama chao. Pole pole ndiyo mwendo tutafika tu na shule zetu za kata.

Sent using Jamii Forums mobile app

Anamuonya mtu kwa kusema ukweli? sasa hiyo miradi mikubwa kama haina manufaa nao kwa nini iwe dhambi kusema wanacho kihitaji?
 
Hatuwezi kuwa na wana ccm wasaliti ndani ya chama haiwezekani kama mwenyekiti hajui umuhimu wa ndege na reli huyo uenyekiti haumfai kabisaaa aondoke zake akiache chama salama
Iko wapi dhana na dhima ya demokrasia mnayoihubiri ccm kwenye bandiko lako? Au mwenyekiti hakutakiwa kuyazungumzia mnahitaji ya waliomchagua? Na huyo waziri wa viwonder naye no Kati ya praisers waliokubuhu ambao hawajui kuwa demokrasia Ina dirisha la kuwasikiliza na kuwapa wachache badala ya wengi! Kweli namamini leo kuwa ccm ni chama Cha kifalme kisichohojiwa!
 
Katinka.selikali.hii.ukisema.ukweli2.ww.tayari.umeshakua.niaduyao
1579699573260.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu anahujumu uchumi na lazima ametumwa na mabeberu huku akijivika ngozi safi ya wanaccm , wanyonge tuwe makini kwani hawa ndio wanasababisha tuonekane sisi ni maskini wakati sisi tupo uchumi wa kati na soon tutakua donour country
 
Iko wapi dhana na dhima ya demokrasia mnayoihubiri ccm kwenye bandiko lako? Au mwenyekiti hakutakiwa kuyazungumzia mnahitaji ya waliomchagua? Na huyo waziri wa viwonder naye no Kati ya praisers waliokubuhu ambao hawajui kuwa demokrasia Ina dirisha la kuwasikiliza na kuwapa wachache badala ya wengi! Kweli namamini leo kuwa ccm ni chama Cha kifalme kisichohojiwa!
Kuzungumzia mahitaji yake ni jambo moja na kukejeli yale yalio mahitaji kwa wengine hata kama yeye hayaja mgusa ni jambo jingine

Kwani aliye mwambia ndege na reli ni lazima kila mtanzania apande nani?

Kuna wanao pata direct advantage kupitia ndege na reli na wengine wanapata indirect advantage hivyo wale wanao panda ndege ndio hao wanao pata direct advantage na malipo wanayo lipa hao wapanda ndege na treni yatawafikia hao wengine indirectly kama kupewa elimu bure na huduma za afya pamoja na madawa

Sikutegemea hata siku moja mawazo kma hayo ya mwenyekiti huyo yatoke kwa mwana ccm ameonesha ujinga wa hali ya juu sana napendekeza aondolewe huo uenyekiti haraka sana hatufai.
 
Aina ya mwenyekiti huyo inaakisi aina ya wanachama wengi wa ccm ambao inawaringia kuwa nao! Kama kumfukuza yeye Basi jiandaeni kuwafukuza wanachama wenu wengi ambao mliwanyima elimu makusudi ili muwamiliki na Sasa yanawatokea piano mnamlalamikia! Lakini, huo no mwanzo tu wa baadhi ya wanaccm kujitambua na kuwaalart kuwa hawakubaliani na mnayoyatenda!
 
Hatuwezi kuwa na wana ccm wasaliti ndani ya chama haiwezekani kama mwenyekiti hajui umuhimu wa ndege na reli huyo uenyekiti haumfai kabisaaa aondoke zake akiache chama salama
Lakini ataondokaje wakati kachaguliwa na wanachama? Unadhani huyu ni wakupachikwa kama huyo jamaa wa 100% kwa 100%?
 
M/kiti katoa maoni yake kulingana na geografia aliyopo lakini watu wanamwelewa Kama mealiti🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🤣🤣🤣🤣
 
Aina ya mwenyekiti huyo inaakisi aina ya wanachama wengi wa ccm ambao inawaringia kuwa nao! Kama kumfukuza yeye Basi jiandaeni kuwafukuza wanachama wenu wengi ambao mliwanyima elimu makusudi ili muwamiliki na Sasa yanawatokea piano mnamlalamikia! Lakini, huo no mwanzo tu wa baadhi ya wanaccm kujitambua na kuwaalart kuwa hawakubaliani na mnayoyatenda!
Kama unaamini huyo kajitambua basi tanzania ina hali mbaya sana sana sana.
 
Ndani ya wana lumumba ukiwa una tabia ya kuhoji basi wewe ni msaliti
Iko wapi dhana na dhima ya demokrasia mnayoihubiri ccm kwenye bandiko lako? Au mwenyekiti hakutakiwa kuyazungumzia mnahitaji ya waliomchagua? Na huyo waziri wa viwonder naye no Kati ya praisers waliokubuhu ambao hawajui kuwa demokrasia Ina dirisha la kuwasikiliza na kuwapa wachache badala ya wengi! Kweli namamini leo kuwa ccm ni chama Cha kifalme kisichohojiwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom