CCM Kila wakiharibu wanadai ni Maoni binafsi ya Kiongozi hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Kila wakiharibu wanadai ni Maoni binafsi ya Kiongozi hii imekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Jan 11, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Toka kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu kumekuwa na mambo ambayo yanakera sana pale unapokuta kiongozi tena mtendaji wa chama iwe katibu au mwenyekiti wa chama utasikia HAYO YALIKUWA MAONI BINAFSI NA SI TAMKO LA CHAMA, sasa mimi najiuliza kwenye vikao vya CCM waandishi wa habari hawaingii ndani na Kiongozi akizungumza na waandishi na ikaonekana ilikuwa pumba, utasikia halikuwa tamko la chama.

  Hivi majuzi Lowasa alikiri arusha kuna tatizo lazima litatutuliwe, tukasikia CCM haihusiki na hayo ni maoni yake bimafsi.

  Tena akaja huyu mwendawazimu chitanda amewakejeli maaskofu wakati huo makamba anachakachua ili ionekane ni mgogoro wa kidini, chatanda anawaambia maaskofu wavue majoho waje kwenye majukwaa ya siasa ile hali maaskofu wanakemea watu kuuawa.

  Juzi akaibuka Mzee Katapila eti anadai Huyu binti kafanya makosa na CCM inatakiwa kuomab Radhi, nakubaliana naye kiasi. Lakini cha kushangaza leo anakuja makamba eti ile ni maoni binafsi wakati katibu ndio anayetoa tamko la chama.

  Hii imekaaje Great Thinkers?
   
 2. e

  emalau JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Iti iz disoganizeshen !!!!!
   
 3. Mbwiga_Plus

  Mbwiga_Plus Senior Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kupoteza dira na mwelekeo kama alivyopata kutamka Mzee(rip) Kolimba.

  Sasa tutatofautishaje maoni binafsi ya mtu na ya chama?...

  Mi nilijua mtu akiwa madarakani na analipwa mshahara na oganaizesheni fulani anakuwa muda wote anawakilisha maoni ya taasisi hiyo...
  Aidha hawezi kuongea kitu ambacho kwa namna yoyote kinakinzana na sera ya taasisi yake!

  Lakini hawa wenzetu wanasoma kauli za wakubwa wao sana...Nadhani hata JK alipoongelea katiba mpya watakuwa walisema kuwa hayo ni maoni yake binafsi!..hahahaaa...itafikia wakati mkuu anahutubia taifa na wasemaji wake wakasema amehutubia maoni yake binafsi!..
  Kukosa msimamo ni hatari sana !...hasa mwongeaji anapokuwa Makamba au Tambwe Hiza!...Gadem!

   
 4. P

  Proud Patriot JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 220
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wanaf--a
   
 5. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mtaalamu wa mambo ya siasa Vernon Bogdanor kwenye article yake "The rise and fall of the political party" ameandika hivi, In an era where individualism, not collectivism, has become the leitmotif, the mass party is dying on its feet.

  hiki ndicho kwa uwazi kabisa tunachokiona CCM. kwanza sauti na heshima ya watu na utu ambazo ni nguzo kuu za uanzishwaji wa chama hiki (cha wakulima na wafanyakazi) tayari zimekwisha kubomoka.

  Sasa hivi ni kila mtu na lwake, aseme lake...sawa...atwae lake...sawa, maadamu tu haingili ulaji wa wakuu.

  Kimsingi msigano huu wa kimantiki na kifikra, huku kila mtu akiwa dume la nyani mwenye uwezo wa kutamka lolote lile kisha kesho akasema tena lolote lile analotaka, ndio kichocheo kizuri cha kifo cha CCM

  Angalia wakati mfupi tu hapo nyuma, magazeti ya wanaofahamika
  "wakijani" yalikuwa yenye muelekeo mmoja. Leo soma utagundua ule msemo wa "Mwamba Ngoma" umeanza kufanya kazi. Kila mtu na lwake, ni ku-Chukua Chako Mapema, ukizubaa wenzako wakikuzidi ujanja, funga domo........piga kimya

  CCM is now dying on its feet.
  Wanadhani wako salama, but keep my words, you will seekama hawatajirudi na kurudi kwenye misingi yake,Chama cha wafanyakazi na wakulima na sio majambazi
   
Loading...