CCM Kila wakiharibu wanadai na Maoni binafsi ya Kiongozi hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Kila wakiharibu wanadai na Maoni binafsi ya Kiongozi hii imekaaje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Jan 11, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Toka kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu kumekuwa na mambo ambayo yanakera sana pale unapokuta kiongozi tena mtendaji wa chama iwe katibu au mwenyekiti wa chama utasikia HAYO YALIKUWA MAONI BINAFSI NA SI TAMKO LA CHAMA, sasa mimi najiuliza kwenye vikao vya CCM waandishi wa habari hawaingii ndani na Kiongozi akizungumza na waandishi na ikaonekana ilikuwa pumba, utasikia halikuwa tamko la chama.

  Hivi majuzi Lowasa alikiri arusha kuna tatizo lazima litatutuliwe, tukasikia CCM haihusiki na hayo ni maoni yake bimafsi.

  Tena akaja huyu mwendawazimu chitanda amewakejeli maaskofu wakati huo makamba anachakachua ili ionekane ni mgogoro wa kidini, chatanda anawaambia maaskofu wavue majoho waje kwenye majukwaa ya siasa ile hali maaskofu wanakemea watu kuuawa.

  Juzi akaibuka Mzee Katapila eti anadai Huyu binti kafanya makosa na CCM inatakiwa kuomab Radhi, nakubaliana naye kiasi. Lakini cha kushangaza leo anakuja makamba eti ile ni maoni binafsi wakati katibu ndio anayetoa tamko la chama.

  Hii imekaaje Great Thinkers?
   
Loading...