CCM kichwa kigumu haitaki kusikia ukweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM kichwa kigumu haitaki kusikia ukweli!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kessy kyomo, Aug 27, 2012.

 1. kessy kyomo

  kessy kyomo Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Ya Igunga, CCM na jeuri ya madaraka!

  Na Mashaka Mgeta, 26th August 2012

  Waliokuwa wajanja, walishiriki kikamilifu kukionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika hatua za awali za kampeni zake kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge, jimbo la Igunga mkoani Tabora uliofanyika mwaka jana. Waliionya CCM kupitia viongozi na makada wao, kwamba kutokana na kauli na vitendo vya hovyo, vilivyojikita katika taswira ya jeuri ya kuwepo madarakani, wanazidi kuuchukiza umma.

  Vitendo kama vilivyohusu utoaji misaada hasa ya chakula, vitisho vya kuikosesha jamii haki za msingi ikiwa watamchagua mgombea asiyetokana na CCM, kutembea na kuonyesha hadharani bastola, ni miongoni mwa yaliyotajwa kutokukistahili chama tawala.
  Yalisemwa mambo mengi katika kuionya CCM, hata sasa bado yanasemwa mengi pale ukiukwaji wa haki za raia unapofanywa, lakini kwa jeuri na dharau, miongoni mwa wasiostahili kuvishiriki vitendo hivyo, wanatenda.

  Yaliandikwa mambo mengi na mengine kutangazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, badala ya kujifunza ili wayaepuke, CCM wakayaendeleza, wakayachochea na kuyafanya kuwa ‘mambo ya kawaida' kwao. Pole kwa aliyetangazwa mshindi wa Igunga kupitia CCM, Dk Peter Kafumu, kwa maana alish iriki kampeni kwa njia za kistaarabu, lakini akachafuliwa. Wanaoshindwa kuuona mwanga wa mabadiliko unaolimulika taifa hili, wakajikita katika ‘kuzivuruga' kampeni za Dk Kafumu, hatimaye mahakama imeutengua ushindi wake.

  Yapo mambo ya kujifunza kutokana na hatua ya mahakama kutengua ushindi wa Dk Kafumu, mtaalamu wa madini ambaye pasipo shaka, uwepo wake bungeni ulikuwa na maana pana kwa nchi na watu wake. Pasipo kujadili msukumo na shinikizo za kisiasa, bali ukweli unabaki kuwa mtaalamu wa madini, sekta inayopigiwa kelele kila kukicha, anapokuwa ndani ya chombo cha maamuzi kama Bunge, inasaidia zaidi hasa anapokuwa miongoni mwa wanaojali maslahi ya umma.

  Ingawa ni hivyo, watawala kupitia CCM wanapaswa kutambua kwamba kuwepo madarakani ni dhamana inayotokana na umma, hivyo kitendo cha aina yoyote kinacholenga kuudhalilisha, kuufedhehesha, kuulaghai na kuutisha (umma) lazima `uzale' adhabu inayotokana na umma.

  Ninatambua dhahiri kwamba wapo watu miongoni mwa watawala, wanaotambua na kutenda ipasavyo, wakitimiza wajibu wao pasipo kuathiriwa na jeuri, kiburi ama majigambo ya kisiasa, kwamba kwa sababu wanatawala, wanaweza kufanya lolote lile. Kwa siku za hivi karibuni CCM imejipambanua kwa kukosa viongozi na makada wenye uwezo wa kupanda jukwaani, wakihutubia na kuushawishi umma ili pasipo hila, ghiliba na vitisho, kiendelee kukubalika na kutawala. CCM imejikuta ikiwa na wanasiasa walio mfano wa ‘waigizaji', kwamba hata wanapokuwa kwenye majukwaa ya siasa, si rahisi kukubali mara moja kwamba wanaistahili sifa na heshima ya kuwa watawala. Pengine wangebaki ‘vijiweni' kuongoza mijadala inayohusu hali ya siasa nchini.

  Lakini wasiokuwa na uwezo wa kuushawishi umma ndani ya CCM, wameotesha mizizi, wameunda mitandao na kushiriki fitina zinazowafanya wateuliwe na hatimaye kuchaguliwa kuwa viongozi wa umma. Badala ya kuutumikia umma, wakaudhalilisha umma.
  Mathalani, CCM ilishafanya tathimini kubaini gharama zilizotumika kuwasafirisha viongozi wa serikali kwenda Igunga, ikalinganisha gharama hizo na thamani ya kujieneza kwake ili kikubalike zaidi kwa umma?

  Kama viongozi wakiwemo mawaziri wanatumia rasilimali za umma, kupitia dhamana walizokabidhiwa wanashindwa kuielezea itikadi ya CCM, dira ya CCM, mwelekeo wa CCM, ilani ya uchaguzi ya CCM, tena kwa kuwianisha na mipango na mikakati ya maendeleo.
  Badala yake wanashiriki kutoa kauli za vitisho, kuonyesha silaha hadharani na uozo mwingine unaokigharimu chama tawala hata kufikia ‘kupigwa chini' kwa Mbunge anayetokana na chama hicho, kuna manufaa gani. Mwishoni mwa wiki niliandika kwenye mtandao wa kijamii wa Wanabidii, nikachapisha utenzi huu ambao kwa ujumla, unahusiana na kadhia ya Igunga:

  Anguko la Kafumu na Mapinduzi ndani ya CCM

  Kafumu amevuliwa ubunge,
  Makosa Ya 'wahafidhina' wa CCM,
  Wale wasioyaona mabadiliko,
  Wasiotaka kuyaishi mabadiliko,
  Wasioyakubali mabadiliko.

  Wamefanya 'uvundo wa kisiasa',
  Wameukasirisha umma,
  Wameumbuliwa na Mahakama,
  Pole sana Kafumu!
  Pole sana mwana mawasiliano mwenzatu.
  Kwa jeuri na ulevi wa madaraka,
  Wasiostahili, wamekusababishia usichostahili.

  Hukumu imeshatoka,
  Taji la ubunge umevuliwa,
  Mjengoni hawatakuona,
  Pumzika, anza upya.

  Ole wako CCM,
  Ole kwa jeuri ya waliomo ndani yako,
  Wakitumia rasilimali za umma,
  Wanakiuka yaliyo ya umma.

  Wanajivisha jeuri ya kutoguswa,
  Wafanye wanalolitaka,
  Watishie pasipo soni,
  Wakiuke kwa matarajio,
  Kwamba watadumu siku zote.

  Amka enyi mlio wa CCM,
  Mapinduzi ya haki myaibue,
  Hasira zenu ziwaondoe wasioistahili jamii.
  Watoke, watoke kabla hamjatoka.

  Msibwete enyi wana wa CCM,
  Mkayaona mabaya na kuyaacha,
  Kwa vile yanatendwa na wenye majina,
  Mkashindwa kuwakemea, kuwatimua.

  Mtayaonja mauti ya kisiasa,
  Kwa uzembe wa wasio haki,
  Wakitisha na kukiuka,
  Ubunge wenu mkavuliwa.

  Kazi kwenu.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  sijakuelewa!
   
 3. m

  mnduoeye Senior Member

  #3
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Kessy usemayo ni sahihi kabisa lakini bahati mbaya sana walishaziba masikio siku nyingi wasisikie usemalo.
  Hawataamini na hawaamini kuwa mambo yanaenda mrama kwa sasa na watasimama mishipa ya shingo ikiwatoka pima na kusema wanaohama chama waache waende ni mzigo na kiko imara.Hebu tusiseme tena tuache upepo uwabebe kuwe na mabadiliko.MVINYO WA MADARAKA UMEWALEVYA WALA HAWAMKUMBUKI TENA ALIYEWAANDALIA MVINYO HUO(WANANCHI).
   
 4. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ni wiki hii ambapo CHADEMA inaelekea IRINGA na SONGEA, mtambo wa kurushia propaganda wa CCM, gazeti la SAUTI HURU likarusha propaganda ya kuwa CHADEMA inafadhiliwa na Kanisa Katoliki, kwa kujua au kutokujua propaganda hii inarushwa wakati CHADEMA inaelekea maeneo ambayo watu wengi katika maeneo hayo ni wakatoliki.

  Athari ya propaganda kama hizi anaathiri CCM yenyewe, kwani watu huko watajiunga wengi kwa kuwa chama hicho kimepata baraka kwa imani wanayo ishikilia. CCM ijue hili utoaji wa propaganda kiholela holela hakujengi chama bali kunabomoa.

  CCM inapaswa ijitathimini kuwa kama matumizi ya propaganda kama yanajenga chama au yanabomoa chama kuliko kuendelea kurusha propaganda kiholela holela bila kuangalia zinajenga vip Chama na taifa
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Mkuu ilitabiliwa mwisho wa ccm hata iweje ni lazima kife, kama walivyokufa cuf!
  Huko koote ni kutapatapa!
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu wanategemea kuku achinjwe aitapetape?
   
 7. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mmh, watajiunga tu kwa vile gazeti la Sauti limedai kwamba CDM ni chama cha wakatoliki?! Siamini sana kwa hili kwani wakatoliki si wajinga kiasi hicho. Kama watajiunga na chadema ni kwa sababu ya sera zake na siyo kwa sababu ya kufungamanishwa na ukatoliki.
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mimi mkatolic na nimwanachama wa ccm sijui wanasemaje sasa!
   
 9. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  sawa lakini kinachonishangaza mimi nikuona wanashindwa hata kuzipangilia propaganda zao kwa kushindwa kwenda na wakati wa hao adui zao, ni kweli pia propaganda zinatolewa na ccm hazikidhi viwango vya wajinga kuamini labda vitakidhi viwango vya wapumbavu tuu kwasasa,
   
 10. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  waraka wa TEC haujakufikia kwani au umeamua kuziba masikio?
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu kwani yoote haya unayoleta faida yake ni nini!?
   
Loading...