CCM katika hali mbaya Arusha; kigogo mwingine (Bananga) atimkia CHADEMA

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. TAARIFA KWA VYA HABARI


"Mficha maradhi kifo humfichuwa "

Ni muda mrefu nimeitafakari dhamira yangu na sasa ni wakati muafaka kufikia maamuzi magumu, Nimeamua kuachia nyadhifa zangu zote ndani ya CCM ambazo ni, MJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM TAIFA, MJUMBE WA BARAZA LA MKOA UVCCM, NA M/KITI WA KAMATI YA MAHUSIANO YA UVCCM MKOA ARUSHA.

Yaliyonisukuma ni mwelekeo mbaya wa CCM kwa sasa ambao umejiondoa kuwa Chama cha wanyonge na wakulima na sasa ni chama cha kundi la watu wachache na watoto wao ndio sababu yanayoendelea sasa ndani ya CCM yanasikitisha sana.

Usaliti na makundi ndani ya CCM yanatishia kabisa uhai wa chama na tayari yamekwisha angamiza Taifa letu, hata hivyo nafasi ya wa watoto wa wanyonge ndani ya CCM inazidi kuwa finyu, aidha ujipendekeze kwa wakubwa ili upate nafasi ya kutumikia jamii au Chama, wakati nafsi yangu haiko tiyari kusimamia uovu huu sasa nimeamua kusimamia ninachokiamini bila uoga wala unafiki, na mfano Tazameni yanoyoendelea ndani ya UVCCM ARUSHA mikono ya mtoto wa mkubwa unaumaliza umoja huo mkoani hapa.

Lakini pia uzito wa serikali ya CCM kushidwa kuwawajibisha wabadhirifu na wanaotumia vibaya madaraka waliyopewa angalia ubadhirifu mkubwa hivi karibuni uliofanywa na Mawaziri na Watumishi wengine wa Umma, Angalia jinsi Serikali imelichukulia suala la Jairo kwa mzaha, ni hatari kwa Nchi yetu kwamba wakati watoto hawana madawati wako viongozi wakubwa ambao wanashindwa kuchukuliwa hatua kwa wizi wa mabilioni ya fedha.

Sababu ni nyingi sana za kwanini nimeamua kutoka CCM, nikisema niandike zote pengine itanipasa kuandika kitabu hata hivyo ninaamini kuwa nitakuwa na fursa ya kueleza mambo mengi sana kwenye mikutano ya hadhara nitakayofanya na Chama cha kipya CHADEMA.

CHADEMA, nawashukuru kwa kunipokea nawahaidi utumishi na kazi iliyotukuka, nitajifunza kwenu na pia naamini mtajifunza kwangu ili tuweze kwa pamoja kuleta matumaini kwa wanyonge.

Kwa marafiki zangu na wanachama wa CCM, msihuzunike sana kwani ninatangulia kwenda kuwaandalia makao kwani ninajua nanyi pia mko njiani mnakuja, hata hivyo sikuwahi kuwa mwema kama malaika tulipokuwa pamoja CCM naamini kuna mahali niliwakosea kama binadamu naomba msamaha kwenu na undugu wetu ubaki, lakini kama maamuzi yangu ya kwenda Chadema yatakuwa yamewauzunisha poleni sana na muendelee kuchukia kwani hatuwezi kuukwaza utu na faraja ya Mwanadamu kwa kufurahisha nafsi za watu wachache.

Asanteni sana karibuni Chadema.


Ally Bananga.
……………………
27/4/2012.
 
Nimeupenda sana ujumbe wake huyu bwana. Kwa hakika kama trend itakuwa hivi tunaweza kujikuta hadi kufikia 2014 tunatakiwa kurudia uchaguzi wa madiwani na wabunge wengi sana kwa kuwa wengi wao watakuwa wameshahamia CHADEMA. Kwa hili tutapaswa kumshukuru na kumpongeza Kikwete kwa kusaidia kuindoa CCM madarakani.
 
Kwa marafiki zangu na wanachama wa CCM , msihuzunike sana kwani ninatangulia kwenda kuwaandalia makao kwani ninajua nanyi pia mko njiani mnakuja ,hata hivyo sikuwahi kuwa mwema kama malaika tulipokuwa pamoja CCM naamini kuna mahali niliwakosea kama binadamu naomba msamaha kwenu na undugu wetu ubaki , lakini kama maamuzi yangu ya kwenda Chadema yatakuwa yamewauzunisha poleni sana na muendelee kuchukia kwani hatuwezi kuukwaza utu na faraja ya Mwanadamu kwa kufurahisha nafsi za watu wachache.

Asanteni sana karibuni Chadema.

Ally Bananga.
……………………
27/4/2012.
Karibu sana Bananga nimependa paragraph yako ya mwisho kwa jinsi ulivyowaaga CCM.
Tunamsubiri Abdallah Mpokwa aliyekuwa katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha nasikia amehamishiwa makao makuu Dar.
 
Ally Bananga mfuasi mwingine wa EL sina imani na na wewe kabisa CCM we na Millya mlikuwa mnatumikia EL na mtoto wake ""Cadet" Fred Lowassa anyway karibu CDM but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa

Wametubu dhambi zao hatuna budi kuwarudisha maana nia yetu ni kurudisha wale waliopotea pia.
 
Kwa marafiki zangu na wanachama wa CCM, msihuzunike sana kwani ninatangulia kwenda kuwaandalia makao kwani ninajua nanyi pia mko njiani mnakuja hata hivyo sikuwahi kuwa mwema kama malaika tulipokuwa pamoja CCM naamini kuna mahali niliwakosea kama binadamu naomba msamaha kwenu na undugu wetu ubaki, lakini kama maamuzi yangu ya kwenda Chadema yatakuwa yamewahuzunisha poleni sana na muendelee kuchukia kwani hatuwezi kuukwaza utu na faraja ya Mwanadamu kwa kufurahisha nafsi za watu wachache.

Ujumbe wa maana sana huu!
 
CHADEMA nawashukuru kwa kunipokea na wahaidi utumishi na kazi iliyotukuka, nitajifunza kwenu na pia naamini mtajifunza kwangu ili tuweze kwa pamoja kuleta matumaini kwa wanyonge.

Kwa marafiki zangu na wanachama wa CCM, msihuzunike sana kwani ninatangulia kwenda kuwaandalia makao kwani ninajua nanyi pia mko njiani mnakuja, hata hivyo sikuwahi kuwa mwema kama malaika tulipokuwa pamoja CCM naamini kuna mahali niliwakosea kama binadamu naomba msamaha kwenu na undugu wetu ubaki, lakini kama maamuzi yangu ya kwenda Chadema yatakuwa yamewauzunisha poleni sana na muendelee kuchukia kwani hatuwezi kuukwaza utu na faraja ya Mwanadamu kwa kufurahisha nafsi za watu wachache.


Ally Bananga.
……………………
27/4/2012.

Ninamashaka kama hii ndiyo nakala halisi.
But hiyo BLUE paragraph imenivutia sana. Hongera kwa kuiona ile kweli na kuheshimu dhamira yako kwa vitendo
 
Ally Bananga mfuasi mwingine wa EL sina imani na na wewe kabisa CCM we na Millya mlikuwa mnatumikia EL na mtoto wake ""Cadet" Fred Lowassa anyway karibu CDM but tutakaa na nyie kwa tahadhari kubwa

siyo kila jambo una weza kukubali kwa kulazimishwa kwasababu alikuwa mfuasi wa EL NO kwani wenzako wanaona mabadiliko ni sasa siyo mbali kama wengi waonavyo ndiyo maana wameona niwakati wawao kuwahi kabla SAFINA HAIJAFUNGWA
 
Back
Top Bottom