CCM kapuni; Mchicha umegeuka kuwa mbuyu

Wakati wa kampeni za Urais 2015 yaliongelewa mengi. Mfano "Hakuna mwenye nguvu kuliko chama". Nikijaribu kuangalia kwa undani naona Mgfl ana nguvu mara kumi kuliko chama chenyewe. Wengine wamebaki kujipendekeza tu. Hata siamini kama ni CCM ileile iliyotusadikisha kwa miaka mingi kuwa mambo yao yanaamuliwa na vikao halali vya chama chao. Duu
 
Ndugu wanaJF, naamini wengi mnakumbuka Magufuli alipokabidhiwa rungu la Urais na Kikwete, wana-CCM wakaanza yao ya kichama chama mara Magufuli mchanga kwenye CCM, hajawahi hata kuwa mwenyekiti wa mkoa wala mjumbe wa NEC, sio mwanasiasa bali mtendaji.

Leo hii najiuuliza maswali sipewi majbu wale wenye CCM yao wako wapi mbona kimya, sauti zao ziko wapi kama CCM wakongwe.

Juzi kati Nape kang'olewa mchana kweupe, kakosa hata mwanaCCM mmoja wakumtetea au hata kulaani tu udhalilishaji huo mbele ya Media kwa mtu kama Nape ambaye kila mtu anajua mchango wake ndani ya chama.

Waliojidai wao ndo wajenzi wa CCM leo wako wapi? Mbona hatuwasikii? Waliojidai wananguvu CCM wako wapi?

Hii yote inaonesha CCM imefungiwa kwenye chupa!Hii yote inaonyesha wale wote waliokuwa wanajidai ni wajenzi wa CCM na wenye nguvu sio wasafi ni wezi tu, wala rushwa wakubwa, majangili ya wanyama pori, wauza unga wakubwa ndio maana kimyaaaaaaa!

Aliyebaki msafi mh Nape wa kupaza sauti mbele ya umma kang'olewa meno na fox. Waliojidai ndio wamiliki wa CCM kumbe wachafu sasa kimyaaa! Wamefcha mikia!

Namshauri Magufuli akifute kabsa hiki chama kipotee kwenye ramani ya Tanzania aanzishe chama chake kipya kinachoendana na speed ya akili yake!

Uliona wapi sauti ya serikali ndio hiyo hiyo iwe sauti ya chama?(Hii inaitwa nani anabisha).

UVCCM nawashauri waachane na siasa badala yake wakalime viazi na matikiti maji,
Ofisi zote za CCM ningependa baada ya mwaka mmoja ziwe maduka ya matikiti maji na viazi mviringo.
Chadema utawajua tuu. Mnashabikia CCM kuvurugika? Mbona imeimarika pamoja na Lowasa kutoka. Aliyekwambieni CCM ni mtu nani? CCM Ni jeshi kubwa hata wakifanyakazi Askari 1000 kwa mpigo linaendelea kuimarika. Mwacheni Magufuli afanyekazi. Kumuona Nape amejisahau kuwa ni msemaji wa Serikali NA kufunga a na wanaoiponda Serikali . Alijisahau na mwenyewe kusema Nape. Mwacheni Nape apumzike. Mnampandisha jazba . Mnataka ahamie kwenu Chadema? Mbona huko ni worse?
 
Back
Top Bottom