CCM kama nyie ni wapenda haki, naomba mfute matokeo ya chaguzi zenu zote za mwaka huu kwasababu zimejaa rushwa 100%

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,535
99.9999% ya wote walioshinda, wameshindwa kwa nguvu kubwa ya rushwa(kuhonga) kwa wajumbe na siyo nguvu ya kura za wajumbe makini.

Rais Mstaafu Kikwete ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa kiongozi wa uangalizi wa uchaguzi mkuu nchini Kenya na huku nyumbani mimi GENTAMYCINE niliamua kujiteua mwenyewe kufuatilia hizi chaguzi za CCM (za matawi, shina na kata). Nilichokiona huko ni rushwa kutembezwa tena wazi wazi bila aibu kwa wajumbe(Wapiga kura) waliokuwepo.

CCM tafadhali kwa maslahi mapana ya chama chenu na mkiwa kama mfano wa kuigwa Tanzania, Afrika na kwa marafiki zenu wachina upesi sana tengueni matokeo na sitisheni kwa sasa chaguzi hizi mpaka huu ugonjwa sugu wa rushwa mlionao mtakapoupatia tiba ya kudumu na wote kupona.​
 
Chama kikikaa madarakani muda mrefu madarakani kwa shuruti, uongozi hugeuka kuwa fursa na sio utumishi kwa umma. Iwapo viongozi wanapatikana ndani ya chama chao kwa rushwa, tegemea wizi mkubwa wa kura kwenye uchaguzi wa nchi ili wakae madarakani.

Kwa bahati mbaya mfumo wa uchaguzi hapa nchini na deep state nao ni sehemu ya hiyo rushwa, hivyo ni lazima waulinde mfumo huo wa rushwa ili waendelee na ulaji.

Namna pekee ya kubadili huu mfumo mkongwe wa rushwa, ni kutokea machafuko, au nchi kupinduliwa ili mifumo ya utawala ianze upya.
 
Sikujua, kumbe refugees wanaruhusiwa kutoa ushauri wa kisiasa ndani ya jamuhuri nyingine baada ya kukaribishwa kwa hifadhi., Ooh sawa sawa hili ni jambo jema sana, sawa sawa mkimbizi toka Kitwe Rwanda ulikua unasema kwamba ?
 
Itoshe kusema haiwezekani. Itoshe kusema hawawezi kufanya hivyo.
Kuna baadhi ya maeneo viongozi wa wilaya wamewaita walioshindwa ngazi ya Kata nà kuwapiga mkwara wasikate rufaa vinginevyo watakutana na rungu la Chama.
 
Naipongeza ccm kwa kudumisha mila, rushwa na ccm ni kama uji na mgonjwa.

Ukiona mtu analalamikia rushwa ndani ya ccm ujuwe wajumbe wameshampiga spana sasa analeta umbea wake JF.

Wasiokubaliana na upumbavu wa ccm walishajitenga na chama hicho muda mrefu tu.

Tatizo ka wasomi koko sasa hivi ajira hawana wameona fursa ni kugombea chaguzi za ccm, subirini mpigwe spana mpaka mtie akili na umbea wenu bakini nao hukohuko msije kutupigia kelele huku.

Hakuna asiyetowa rushwa ccm, wanachozidiana ni viwango tu, wewe ukitowa elfu 20 kwa kila mjumbe mwenzako anatowa elfu 40 kwa kila mjumbe, mjumbe anakunja mishiko yake kwa wingi wanampigia aliyepanda dau kubwa.

Kwa kifupi ccm ni gulio la ulanguzi wa kura, anayepanda dau ndio mshindi, sasa mtulie dawa iwaingie mpambane kulipa madeni mliokopa kufanyia kampeni zenu chafu za chama cha kuzimu.
 
Tuendelee tu na ujinga wa kupakana matope na kusifia ujinga muone kama kuna siku tutakuja kufanya chaguzi zenye uhalali. Kila siku tutakuwa tuñapata viongozi wahuni, wezi na washenzi kwasabb tume siyo huru na hatutaki kupambana ili tupate katiba mpya.

Yaani tunataka CCM ambayo inafurahia hii katiba mbovu ijikaange kwa kutengeneza katiba itakayoweka mazingira magumu kwao kushinda chaguzi kwa hila.
 
Kila sekta nchi hii unaifahamu...huyu ndo genta ninayemfahamu mimi
Kwenye siasa yupo,michezo yupo,serikali yupo kwenye umbea yupo pia
 
Chama kikikaa madarakani muda mrefu madarakani kwa shuruti, uongozi hugeuka kuwa fursa na sio utumishi kwa umma. Iwapo viongozi wanapatikana ndani ya chama chao kwa rushwa, tegemea wizi mkubwa wa kura kwenye uchaguzi wa nchi ili wakae madarakani.

Kwa bahati mbaya mfumo wa uchaguzi hapa nchini na deep state nao ni sehemu ya hiyo rushwa, hivyo ni lazima waulinde mfumo huo wa rushwa ili waendelee na ulaji.

Namna pekee ya kubadili huu mfumo mkongwe wa rushwa, ni kutokea machafuko, au nchi kupinduliwa ili mifumo ya utawala ianze upya.
Kupata uongozi ni rushwa, kupata kazi serikalini rushwa na upendeleo. Viongozi na watumishi waliojaa rushwa nchi itaendaje sasa.
 
Chama kikikaa madarakani muda mrefu madarakani kwa shuruti, uongozi hugeuka kuwa fursa na sio utumishi kwa umma. Iwapo viongozi wanapatikana ndani ya chama chao kwa rushwa, tegemea wizi mkubwa wa kura kwenye uchaguzi wa nchi ili wakae madarakani.

Kwa bahati mbaya mfumo wa uchaguzi hapa nchini na deep state nao ni sehemu ya hiyo rushwa, hivyo ni lazima waulinde mfumo huo wa rushwa ili waendelee na ulaji.

Namna pekee ya kubadili huu mfumo mkongwe wa rushwa, ni kutokea machafuko, au nchi kupinduliwa ili mifumo ya utawala ianze upya.
Kwa bahati mbaya mfumo wa uchaguzi hapa nchini na deep state nao ni sehemu ya hiyo rushwa, hivyo ni lazima waulinde mfumo huo wa rushwa ili waendelee na ulaji.
 
99.9999% ya wote walioshinda, wameshindwa kwa nguvu kubwa ya rushwa(kuhonga) kwa wajumbe na siyo nguvu ya kura za wajumbe makini.

Rais Mstaafu Kikwete ameteuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa kiongozi wa uangalizi wa uchaguzi mkuu nchini Kenya na huku nyumbani mimi GENTAMYCINE niliamua kujiteua mwenyewe kufuatilia hizi chaguzi za CCM (za matawi, shina na kata). Nilichokiona huko ni rushwa kutembezwa tena wazi wazi bila aibu kwa wajumbe(Wapiga kura) waliokuwepo.

CCM tafadhali kwa maslahi mapana ya chama chenu na mkiwa kama mfano wa kuigwa Tanzania, Afrika na kwa marafiki zenu wachina upesi sana tengueni matokeo na sitisheni kwa sasa chaguzi hizi mpaka huu ugonjwa sugu wa rushwa mlionao mtakapoupatia tiba ya kudumu na wote kupona.​
Hii ndio ccm bhana
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom