Uchaguzi 2020 CCM kama mnaipenda Tanzania amueni kiume 2020

Ngomile

Member
Mar 18, 2018
18
14
Kwa hali ilivyo sasa inaonesha ule utamaduni wa makundi ya kuwania urais 2020 yameshajipanga na yako mkao wa kuelekea kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu ujao.

hivi karibuni tumeona kumekuwepo majibizano ya kisiasq kati ya wanasiasa wawili hasimu kutoka ndani ya ccm bwana Benard Membe na Rostam Azizi. Hali hii ilianza punde tu baada ya Bwana Rostam Aziz kuibuka na kile alichokiita kumtaka Bwana Membe aachane na watu wanomshawishishawishi kuhusiana na kumokea kijiti kupitia michakato ya ndani ya chama mh Rais John Pombe Magufuli.

Hivi karibuni kwa mara kadhaa Membe amegonga vichwa vya habari katika mitando ya kijamji na vyombo vya habri akitajwa kama mwenye nia ya kuuwania urais wa JMT 2020.

Sasa kwa maoni yangu huku tukizingatia utrendaji na rekodi ya magufuli katika kipindi hiki cha miaka minne nawasihi CCM kuwa wanapaswa kuwaonea wanchi huruma kabisa. Yapo mengi amefanya Magufuli katika kipindi hiki kifupi cha muhula huu wa kwanza ambayo yanaiweke Tz katika rekodi ya nchi ya nchi yenye rekodi mbaya kuhusu

1. Kuporomoka kwa hali za uchumi wa wananchi kwa kisingizi cha miradi mikubwa
2. Hali mbaya za watumishi waumma kwa rekodi ya miaka minne mfululizo bila nyongezaa ya mishahara
3. Kuporomoka kwa uhuru wa vyombo vya habari na uhuri wa kujieleza
4.Mahussano mabovu ya tanzania na jamii ya kimataifa
5.Kufungwa kwa biashara nyingi na wawekezaji kuondoka na kupelekea watu kupoteza ajira zao

Kwa hayo machache na mengine mengi tunaiomba ccm ifikirie jambo kutuwekea huyu bwana kando twende na mtu mwingine anayeweza kututkwamua kutoka hapa tulipokwama jamani hali ni ngumu sana huku mitaani kila kada inalia kivyake.

Ikiwa kweli mko kwa maslahi ya umma huu wa watanzania tunaomba mfanye jambo ka kweli.
Tukisema tunaitwa wapiga dili lkn ukweli wa mambo ni tafrani tupu huku mitaani. Mie sina imani na chama chochote zaidi ya CCM kulingana na mifumo yetu ya uchaguzi mtakaempitisha ndio ataekuwa Rais.
Chondechonde ccm pinduenio meza jamani mtupe ahuenio yamambo.
 
Back
Top Bottom