CCM kabla hamjahoji ya Zitto, tuambieni nini kilimpata Kolimba

Status
Not open for further replies.

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
Habari wakuu,

Tangu naibu katibu mkuu wa CHADEMA,Zitto Kabwe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho,ndugu Kitilla Mkumbo kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya chama,wana -CCM wengi wameibuka wakipinga hatua hiyo na kufikia hatua ya kuhoji Demokrasia ndani ya chama.

Mbali na madai ya kuhoji Demokrasia,wamefikia hatua ya kusema eti mh.Zitto amevuliwa madaraka kwasababu pia amehoji kuhusu ukaguzi wa fedha za ruzuku za chama chake(CHADEMA).

Anyway,tuseme hio ni moja ya sababu ya Zitto kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama.Kama wana-CCM wameona ilikuwa si kosa kwa Zitto kuhoji kuhusu ukaguzi huo wa fedha za ruzuku,je,wana -CCM hawa watuambie kauli ya marehemu Horace Kolimba kuwa CCM imepoteza dira ilihalalisha kilichompata mareheme Kolimba?

Adhabu atayoipata Zitto(kama itatolewa) na adhabu aliyopewa marehemu Kolimba ni ipi isiyo ya kidemokrasia na pengine ni ipi ya kikatili zaidi?

Naomba majibu kutoka kwa wana- CCM.

CCM mnatambuka kuwa charity begins at home?

Mods naomba msiondoe huu uzi.
 
​kolimba ndo nini.....

Kilichoandikwa ni Kolimba we unaandika kolimba. Huoni tofauti?

Kama hujui ni nini, yaonekana hujapitia darasani'. Rudi shule ya msingi na Kati ya darasa la tatu na sita, utakuwa umefundishwa zaidi ya Hilo swali lako.
 
Rafiki pole siku zote kuna ule msemo wa Kiswahili usemao ..."Nyani haoni....."ndiyo sababu kuu CCM kuwapigia kelele nyingi CDM.
 
Ukiwakumbusha suala la Kolimba wanaishia mitini! wanajua walichokifanya Maccm. Wengine wanajifanya hawamjue Kolimba eti wanauliza ndiyo nani? Sisi wa Manda bado tunamkumbuka na nipigo kwetu. Walipokuja kwenye mazishi walihaidi kujenga kipande fulani cha barabara kuwatuliza wamanda na baada ya kumaliza walitokomea na kumsahau kabisa Kiongozi huyu. RIP Kolimba!
 
Rafiki pole siku zote kuna ule msemo wa Kiswahili usemao ..."Nyani haoni....."ndiyo sababu kuu CCM kuwapigia kelele nyingi CDM.
Wanafikiri tumesahau ya marehemu Kolimba!

Hawa ni wanafiki tu!
 
​kolimba ndo nini.....

Kilichoandikwa ni Kolimba we unaandika kolimba. Huoni tofauti?

Kama hujui ni nini, yaonekana hujapitia darasani'. Rudi shule ya msingi na Kati ya darasa la tatu na sita, utakuwa umefundishwa zaidi ya Hilo swali lako.
 
Nani wapo nyuma ya mauaji ya Dr. Senkondo Mvungi? CCM tuambieni, hasa Mwigulu na Nchimbi!
 
inasemekana aliitwa Dodoma akaulizwa umesema nini wewe
chama hakina dira wala mwelekeo???
alie muuliza wapo wote huko walipo
ndio ukawa mwisho wake..
hao CCM sio wasafi wanadhani kila mtu mdhambi kama wao
walishavuana gamba? mbona Kinana hawamkamati na kumtimua kwa tuhuma za kumaliza tembo wetu?
mafisadi wanawalea.
Yule mama alietoka huko UN anaandamana na Kinana badala ya kufundisha chuo na kuwa mshauri wa masuala ya kimataifa amegeuka kipeperushi cha chama,nina wasiwasi kule UN alishindwa kuperform wakamnyima mkataba mwingine.
shame on her.
CCM muda umeisha maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi??
 
Watu tumekereka na Ukanda wenu,Waraka tumeuona,mumefukuza,na fastafasta mumetangaza Uchaguzi,Watu wa sasa hivi wanadadisi na wachambuzi.Wajanja wachache tulijuwa nyinyi ni Wabaguzi.
 
Status
Not open for further replies.
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom