Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Habari wakuu,
Tangu naibu katibu mkuu wa CHADEMA,Zitto Kabwe na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho,ndugu Kitilla Mkumbo kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya chama,wana -CCM wengi wameibuka wakipinga hatua hiyo na kufikia hatua ya kuhoji Demokrasia ndani ya chama.
Mbali na madai ya kuhoji Demokrasia,wamefikia hatua ya kusema eti mh.Zitto amevuliwa madaraka kwasababu pia amehoji kuhusu ukaguzi wa fedha za ruzuku za chama chake(CHADEMA).
Anyway,tuseme hio ni moja ya sababu ya Zitto kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama.Kama wana-CCM wameona ilikuwa si kosa kwa Zitto kuhoji kuhusu ukaguzi huo wa fedha za ruzuku,je,wana -CCM hawa watuambie kauli ya marehemu Horace Kolimba kuwa CCM imepoteza dira ilihalalisha kilichompata mareheme Kolimba?
Adhabu atayoipata Zitto(kama itatolewa) na adhabu aliyopewa marehemu Kolimba ni ipi isiyo ya kidemokrasia na pengine ni ipi ya kikatili zaidi?
Naomba majibu kutoka kwa wana- CCM.
CCM mnatambuka kuwa charity begins at home?
Mods naomba msiondoe huu uzi.