CCM jifunzeni Kwa CHADEMA

Masanilo

Platinum Member
Oct 2, 2007
22,286
4,493
WanaJF,

Siungi Mkono moja kwa moja alichoongea Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mh.Lukuvi Bungeni jioni hii.

Kwanza,Wametoa tuhuma hizi wakati Zitto akiwa hayupo ndani ya Bunge

Pili,Hatuwezi kumuhukumu Zitto moja kwa moja bila kumpa fursa ya kumsikiliza

Napinga tabia hii ya wanaCCM kumdhalilisha Zitto Bungeni na kumnyima fursa ya kujitetea na wengine kuanzisha thread humu.

Tatu,Ni jambo la kusitisha kuwa Chama tawala kina viongozi na makada wanaoweza kuminya haki wazi wazi hasa pale wanapoona kuwa maslahi ya viongozi na wanachama wao yanahatarishwa.Mh.Zitto anayo majina na sio busara kumshambulia kama alivyofanyiwa ili tu kuwanusuru wanasiasa na makada wa CCM waliolimbikiza fedha nje

Nne,Naomba Wanachama na viongozi wa CCM,Wabunge na Viongozi wa Bunge waige mfano bora wa CHADEMA kwa kumpa nafasi ya kujitetea.Natural justice ni jambo la msingi.Tuimarishe misingi ya uwazi katika suala linalohusu maslahi ya nchi.

Namshauri pia Mh.Zitto aweka wazi suala hili hasa suala la kutaja majina ya wamiliki na kama hawezi anaweza kumpatia majina haya Mhe.Lema ayataje.

Kama task Force ya Bunge iliweza kuvujisha majina ya waliochunguzwa,ni kitu gani kinamshinda yeye kuvujisha majina kwa Lema ambaye yupo tayari kutaja bila woga?

Tumpe nafasi badala ya kumzomea na kumshutumu jamani.
 
ki ukweli zitto kadhalilisha sana fans wake na watanzania kwa ujumla wapenda haki na mabadiliko. Mtu anayependa sifa na utulufu mi hatari sana

lakini nashukuru CHADEMA imeyaona haya mapema lakini akapewa nafasi ya kujirekebisha lakini wapi.

mbaya zaidi anafanya utetezi kwenye media, lol. Sijui huyu ataficha wapi sura yake

mnafiki ni mnafiki tu, hafai hafai. Ni sawa na kula nyama ya watu, uahitaji tena na tena
 
WanaJF,

Siungi Mkono moja kwa moja alichoongea Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mh.Lukuvi Bungeni jioni hii.

Kwanza,Wametoa tuhuma hizi wakati Zitto akiwa hayupo ndani ya Bunge

Pili,Hatuwezi kumuhukumu Zitto moja kwa moja bila kumpa fursa ya kumsikiliza

Napinga tabia hii ya wanaCCM kumdhalilisha Zitto Bungeni na kumnyima fursa ya kujitetea na wengine kuanzisha thread humu.

Tatu,Ni jambo la kusitisha kuwa Chama tawala kina viongozi na makada wanaoweza kuminya haki wazi wazi hasa pale wanapoona kuwa maslahi ya viongozi na wanachama wao yanahatarishwa.Mh.Zitto anayo majina na sio busara kumshambulia kama alivyofanyiwa ili tu kuwanusuru wanasiasa na makada wa CCM waliolimbikiza fedha nje

Nne,Naomba Wanachama na viongozi wa CCM,Wabunge na Viongozi wa Bunge waige mfano bora wa CHADEMA kwa kumpa nafasi ya kujitetea.Natural justice ni jambo la msingi.Tuimarishe misingi ya uwazi katika suala linalohusu maslahi ya nchi.

Namshauri pia Mh.Zitto aweka wazi suala hili hasa suala la kutaja majina ya wamiliki na kama hawezi anaweza kumpatia majina haya Mhe.Lema ayataje.

Kama task Force ya Bunge iliweza kuvujisha majina ya waliochunguzwa,ni kitu gani kinamshinda yeye kuvujisha majina kwa Lema ambaye yupo tayari kutaja bila woga?

Tumpe nafasi badala ya kumzomea na kumshutumu jamani.

Masanilo,

Naunga Mkono asilimia 98 ya hiki ulichoandika.
 
Last edited by a moderator:
Hivi CCM na Ag hawaoni haja ya kumsikiliza kabla ya kutoa hukumu?Hawa ni Opportunists.Naamini kesho Zitto ataibuka bungeni kuwaaibisha na kutaja majina hayo
 
Kama mtu amekiri mbele ya kiapo kwa hana majina ya walioficha fedha uswiss kwanini asiitwe kanjanja.. atuombe radhi watanzania... Hongereni chadema kumvua uongozi huyu kanjanja...
 
Hivi CCM na Ag hawaoni haja ya kumsikiliza kabla ya kutoa hukumu?Hawa ni Opportunists.Naamini kesho Zitto ataibuka bungeni kuwaaibisha na kutaja majina hayo

Akifanya hivyo atakuwa amejisafisha sana... Kama anayo kweli asiendelee kunyamaza, ayataje tu angalau watanzania watamwelewa
 
Lakini hebu turudi nyuma kidogo,

Huyu si alikubali kamati ya ucbunguzi iundwe? akakubali kutoa ushirkiano ikiwa ni pamoja na kusema ukweli kwa kula kiapo? tena fungu likatengwa na akawa anakwenda 'kutembea' huko uswizi kuhakiki akaunti na majina?

mimi nadhani AG ametufumbua macho ya kwamba huu ni mchezo wa kisanii maanake siamini kwamba mtu anaweza ku-bank kwenye cheap politics kama hizi

kwisha habari yake zitto
 
Lakini kama vp ampe majina hayo GODbles Lema kama yeye anaogopa.....

duuh ukanjanja ni shida tupu
 
Last edited by a moderator:
Hivi CCM na Ag hawaoni haja ya kumsikiliza kabla ya kutoa hukumu?Hawa ni Opportunists.Naamini kesho Zitto ataibuka bungeni kuwaaibisha na kutaja majina hayo

Zitto hana jina lolote! Lengo lake lilikuwa aseme Mbowe ananyumba Dubai ili mpango wao na akina Kitila ufanikiwe bahati mbaya akakuta imeorodheshwa kwenyed tume ya maadili! Sasa amevuliwa nguo, amebaki uchi wa mnyama! Hana jipya! ccm wamemtosa kama walivyomtosa Lamwai, Tambwe, Ngawaia na wengineo!
Sasa wanafuatia Shoza, Mwampamba, Habibu na Lukosi!
 
Last edited by a moderator:
Lakini kama vp ampe majina hayo GODbles Lema kama yeye anaogopa.....

duuh ukanjanja ni shida tupu
Lema huyu huyu ambaye muda wote ameongea bungeni akiwa ameinama tena ameshikilia meza kama zile picha alizokuwa anazisambaza yeye mwenyewe. Atawezaje kutaja majina ya watu wenye fedha? Si watamgodbless lema kwa mara nyingine?
 
Hivi kodi yetu iliyokuwa inampeleka ulaya kufuatilia huu uongo atazilipaje? Kwa hili watanzania tunatakiwa kushika mawe kuponda si tu zitto ni pamoja na waliokuwa wanampa hizo hela. Wanachezea hela yetu. Upuuzi mtupu
Naunga mkono hoja ya Masanilo.
 
Zitto hana jina lolote! Lengo lake lilikuwa aseme Mbowe ananyumba Dubai ili mpango wao na akina Kitila ufanikiwe bahati mbaya akakuta imeorodheshwa kwenyed tume ya maadili! Sasa amevuliwa nguo, amebaki uchi wa mnyama! Hana jipya! ccm wamemtosa kama walivyomtosa Lamwai, Tambwe, Ngawaia na wengineo!
Sasa wanafuatia Shoza, Mwampamba, Habibu na Lukosi!
Mkuu, ccm hatakiwi mtu mnafiki
 
Back
Top Bottom