CCM jifunzeni Kenya upatikanaji na utendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi, msione aibu

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Wakati umefika kwa chama kikongwe Afrika kubadilika. Ni miaka 61 TANU/CCM kipo madarakani huku ikitumia mifumo ya chama kimoja cha siasa wakati nchi ipo kwenye Mfumo wa Vyama Vingi.

CCM na Serikali yake imekuwa ikiendesha nchi kwa kutumia Katiba ya Chama Kimoja kwa Vyama Vingu vya Upinzani na kupelekea ukandamizaji mkubwa kwa Vyama vya Upinzani katika Chaguzi.

Katiba iliyopo inampa uwezo Mwenyekiti wa CCM ambaye ndiye Rais kuteua viongozi wa kuongoza chombo muhimu kiuchaguzi ambacho ni Tume ya Uchaguzi na Mwenyekiti huyo huyo ni Mgombea Uongozi katika chaguzi zinazosimamiwa na Tume aliyoiteua. Je haki itatendeka kwa Wapinzani?

Ni busara kwa CCM na Serikali yake kwenda nchi ya Jirani Kenya ili kujifunza jinsi Tume yao Huru ya Uchaguzi ilivyopatikana na inavyofanya kazi kwa Haki ili kuondoa utata katika chaguzi za Kenya.

CCM isione aibu kujifunza, mbona nchi jirani zinakuja kujifunza mambo mazuri Tanzania kwa manufaa ya watu wao na nchi kwa ujumla? Vivyo hivyo na CCM na Serikali nendeni Kenya kujifunza ili kuondoa malalamiko ya Vyama vya Upinzani juu ya Tume isiyo Huru na isiyotenda Haki iliyopo.

Tanzania ni yetu sote, tumepewa na Mungu wetu sote.
 
Sijui shida ya hawa jamaa nini. Mi nadhani shida sio ccm. Ni the so called deep state/sijui kama ipo kwanza au ni myth tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom