CCM: Jembe na Nyundo ni alama sahihi kwa nyakati?

kipusy

JF-Expert Member
May 7, 2010
639
321
Zile alama zinazua mjadala mitaani kua, Kua Nyundo inamaanisha kumpiga mtanzania nyundo ya utosi na Lile Jembe ni kwenda kumchimbia kaburi na kumfukia.... Lakini walisahau kwamba ile nyundo maanake ni mfanyakazi, na lile jembe ni Mkulima...

Lakini inabidi sasa Wadau wa chama husika waangalie jinsi ya kubadilisha hizo alama maana hata kama lile jembe linamaanisha mkulima, inamaana watanzania hawawezi kubadilika watatumia kilimo duni cha jembe la mkono mpaka mwisho wa dunia, na ile dhana ya kilimo kwanza haipo tena..... itabaki porojo la vijiwe vya kahawa...WAWEKE HATA PICHA YA TREKTA, ikishindikana kabisa waweke hata NG'OMBE.

na Wafanyakazi hicho chama sio chao kama alivyo address JK... nyundo inafanya nini pale?

Changieni wana Jamii....:confused2:
 
Ni wakati muafaka wa kubadilisha hizo alama hasa ukizingatia wamekiri hadharani kuwa CCM sio chama cha Wafanyakzi.
 
Labda sasa waweke nembo inayoonyesha mafisadi wakikwapua manoti ya wananchi -- iwapo itawezekana kupata mchoro wa namna hiyo. lakini hii ikiwekwa kwenye zabuni, artist atapatikana tu!
 
ALAMA YA JEMBE NA NYUNDO CCM KUFUTWA HIVI KARIBUNI?

CCM kimezaliwa kutokana na TANU na lengo la Waasisi ilikuwa Kiwe ni Chama cha Kuunganisha watu wote na zikachaguliwa alama mbili kuwakilisha Wakulima na Wafanyakazi Ambapo alama zilizotumika ambazo zinatumika pia leo ni Jembe likiwakilisha kundi la Wakulima na Nyundo Wafanyakazi na Wafanya Biashara wakiwa Huko Pia.

Lakini Hivi Sasa Chama Kimekuwa cha wenye Pesa na Mafisadi wala Rushwa Watupu Mpaka wakaipatia umaarufu Takukuru wakati wa mchakato wao wa Kuwapata wagombea.

Tunapendekeza watafute Alama zingine za Kuwakilisha Chama cha Wenye Mapesa, Wala Ruswa na Mafisadi ili Kiache kutuaibisha sisi wakulima na wafanya kazi kwani sisi hatufanyi uchafu huo
 
CCM si chama cha wakulima na wafanyakazi tena bali wenye pesa zao na mafisadi na ndiyo maana mchakato wake ulionekana kujawa na rushwa kuliko vyama vingine vyote
 
Tutumie takwimu za TAKUKURU kupima na kuchagua vyama vyenye watu waadilifu nadhani CCm ni cha mwisho kabisa kwa maadili mema
 
Walimchezea sana rafu mzee Philipo Mangula kwenye uchaguzi wa chama ati kwa vile hakuwa mwanamtandao
 
wanajamii poleni kwa kuchukua hatua hasa ya kupinga ufisadi.
Naleta kwenu changamoto hii,hivi ni kweli jembe na nyundo katika alama za ccm zina maana chama cha wakulima na wafanyakazi ,au zinawakilisha mambo mengine ?
Isije ikawa alama zilezile kwa maana na imani tofauti k.v jembe alama ya kuzika wapinzani baada ya kuwabonda na nyundo ? naomba maoni
 
Rubbish... you have time & PC it doesn't mean you can post any non sense , karibu JF by the way:eyeroll2:
 
Hivi kuna wakulima na wafanyakazi Tanzania wenye shilingi milioni 60 za kuchezea?
 
Jembe na nyundo ni vya kuwalima na kuwabonda watanzania wote - na sio wapinzani tu.
 
Jembe na nyundo inaonesha jinsi ccm inavyoponda vichwa vya watz na kuwauwa kwa kuwazika kwa kutumia jembe la mkono..............
 
NYUNDO = ponda wapinzani, ( sio wafanyakazi tena manake hataki kura zetu)

JEMBE = negative kilimo kwanza.
 
Nauliza...Alama ya Jembe na Nyundo kwenye bendera ya CCM kumaa...nisha nini??








nimegundua janja yako hapo penkundu.
 
I always wondered what meaning these CCM chaps have entailed over years. With all the good reasons they have and looking on what is happening on the ground I think this what it means:

JEMBE: Tutawatumia wakulima kutuweka madarakani, watake watatuchagua wasitake watatuchagua maana Jembe ni lao milele.

NYUNDO: Tutawatwanga wafanyakazi ili wasifurukute, tumia nyundo kugonga fikra zao maana siku wakiungana hatima yetu itakuwa mashakani


What do you think?
 
nyundo ni kwa ajili ya kutengenezea jeneza la wadanganyika na jembe ni la kuchimbia kaburi la wadanganyika
 
NYUNDO inakupiga kichwa na kukuacha ukiwa maiti.
JEMBE linachimba kaburi lako.
Halafu unaambia Chama kimeshika hatamu.
Zidumu fikra sahihi za mwenyekiti
 
Back
Top Bottom