CCM: Je, bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM: Je, bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi?

Discussion in 'Great Thinkers' started by Rev. Kishoka, Aug 24, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Katika sehemu ya kwanza ya Katiba ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kifungu cha cha tatu, hitimisho la Azimio la kuunganisha TANU na ASP linasema hivi:
  Kisha katiba ya CCM inaendelea kwa kusema hili
  Halafu katika kifungu cha nne kinachozungumzia Imani ya CCM, katiba ya CCM inasema
  Kisha ukiendelea nakifungu cha tano kinachogusia malengo ya CCM utakuana na maneno mazito na yenye nguvu kama yafuatayo:
  Ukimaliza malengo na imani ya chama, kinachofuatilia ni Uanachama na wajibu wa Mwanachama wa CCM

  Mwishoni, Katba hii ya CCM toleo la mwaka 2007 linaweka Ahadi za Mwanachama wa CCM ambazo ni hizi
  Sasa ukishaisoma katiba ya CCM kisha ukasoma sehemu kadhaa za Muongozo wa CCM wa Mwaka 1981 hasa kifungu cha 36
  utabaini kuwa Chama cha Mapinduzi kama Chama cha Kisiasa, kwa Miongozo yake na Katiba zake, si chama kibovu, bali hali halisi ya sasa hivi ni kuwa kuna genge ama kundi la watu fulani ambao wamejiingiza ndani ya Chama na kushikilia madaraka na mamlaka ndani ya Chama na Serikali ambao ndio wanaokiharibia sifa CCM, ndio wanaolihujumu Taifa letu na kutumia kisingizi kuwa anayepiga vita Ufisadi na Uhujumu ni mhaini!

  Vikao viwili vikubwa vya CCM vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ambavyo vilanzia kule Butiama na hiki kilichoisha majuzi hapa Dodoma, vinaashiria wazi ni jinsi gani CCM iliyoundwa mwaka 1978 na malengo yake ya kimapinduzi katika kulijenga Taifa la Kijamaa na Kujitegemea, imetekwa nyara na kutumiwa kunufaisha wajanja wachache ambao ni watwana wa Wakoloni na Mabeberu, ni waroho, wavivu, wazembe, wasiowajibika na wanaojinufaisha kutumia hatamu ambazo CCM imepewa na Watanzania kuliongoza Taifa la Tanzania kwa manufaa yao binafsi.

  CCM ni chama cha Wakulima na Wafanyakazi, si cha Wanafiki, Mafisadi au Wazembe!

  CCM ni chama ambacho kilijijenga kwa Watanzania kwa ahadi za kulijenga Taifa letu liwe huru na lenye kujitegemea, liwe mfano wa kuigwa, na si Taifa dhaifu ambalo halina utashi wa kujiimarisha kwa kutumia Juhudi na Maarifa kupiga vita Ujinga, Umasikini na Maradhi!

  Wanaoongoza CCM ni dhaifu na ndio wanaokidhoofisha Chama na kukipa taswira mbaya ambayo inanuka kama kidonda kilichooza.

  Waliopewa dhamana ya kuongoza CCM katika ngazi zote anzia Mtaa, Kata, Kijiji, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa hawafai tena kuendelea kukiongoza Chama cha Mapinduzi au kunufaika kwa matunda ya Uimara wa CCM.

  Uimara wa CCM umebakia kuwa nadharia na maneno na si vitendo na ndio sababu kauli za kipuuzi na kijinga zilizosikika Butiama na juzi Dodoma, zinadhihirisha wazi kuwa maneno ya Marehemu Kolimba kuwa CCM imepoteza dira kuwa ni maneno sahihi na ni lazima yapatiwe ufumbuzi.

  Mimi nina jibu moja tena rahisi sana, nalo ni kuleta Mapinduzi ndani ya CCM kwa wale wote ambao wanasimama upande wa misingi ya awali na ya kweli ya kuundwa kwa CCM na wanaofuatilia masharti, wajibu, majukumu na dhamana ya kuwa Wana CCM, basi wao ndio walio warithi na wamiliki halisi wa CCM na si hawa wengine ambao wamegeuka na kuwa ndumilakuwili na kufikiria nafsi zao kwanza.

  Walioko madarakani CCM wanatia AIBU!

  Nasema tena kuwa CCM imetekwa nyara na mahaini na wahujumu ambao wanatumia kila nyenzo na nguvu za dola kujiimarisha kwa kutumia rushwa, wizi, uhujumu na kuvunja kabisa miiko ya uanachama na kupuuzia maagizo yote ya Chama ambayo bado hayajabadilika hata pamoja na kuwa tumeingia katika mfumo wa Vyama vingi na mfumo wa kiuchumi wa soko huria.

  Hivyo basi, kauli ya Mchungaji kwa WanaCCM imara ni simameni kidete na msione haya Ufisadi ulioko ndani ya Chama! Msionee haya viongozi wabuvu na wazembe ambao wameendelea kushindwa kuleta maendeleo ya kweli kwa Tanzania!

  Wapiganaji wa CCM, simameni imara msiyumbishwe na vitisho au mizenge. CCM ina wenyewe, na wenyewe ni Wakulima na Wafanyakazi na si Mafisadi na virabaka na makuwadi wao!

  Asiwatishe mtu kwa kutumia kikao chochote kile cha Chama au hata vitisho vya kuvuliwa uanachama. Hakuna haja ya Walio CCM wa kweli ambao ni watiifu na waaminifu kwa Katiba na Miongozo ya CCM kuwa leo waondoke wakaunde Chama kingine cha Kisiasa au kuhamia chama kingine.

  Jiungeni, mshikamane na mlete Mapinduzi ndani ya Chama, kwa maana wote hawa wanaotetea na kulinda ufisadi, wanaogopa kuondolewa madarakani na kuvuliwa uanachama, na hivyo wanaanza kuwatuhumu wale walio watiifu kwa Katiba ya CCM kuwa hawafuati maadili ya Chama na hawalindi maslahi ya Chama.

  Maslahi ya CCM ni kuongoza Tanzania na kujenga Taifa imara linalotumia rasilimali zake kwa manufaa ya Wananchi wake.

  Maslahi ya CCM ni kujenga Uongozi na kuwa na Siasa Safi ambazo lengo ni kumkomboa Mtanzania kutoka Unyonge wa kuwa Masikini, Mggonjwa na Mjinga.

  Maslahi ya CCM ni kuhakikisha kuwa Tanzania inajitegemea na kujitosheleza.

  Maslahi ya CCM ni kuhamasisha Uzalishaji mali, Utiifu wa Sheria, Haki, Utu na Uwajibikaji.

  Haya ndio maslahi ya CCM ya kweli ya Wakulima na Wafanyakazi walioko pande zote za Muungano toka Wete, Vikokotoni, Malagarasi, Songea na Manyara.

  Enyi mafisadi na vibaraka wenu, kiacheni CCM chama cha Wakulima na Wafanyakazi. Ondokeni mkaanzishe chama chenu kisicho na nidhamu wala dira!
   
 2. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nafikiri hata hiyo katiba ya SISIEMU inahitaji marekebisho....hata wakiongeza wafanyabishara na fisadiz kwenye huo mstari wa WAKULIMA na WAFANYAKAZI inaweza kuleta sense kuwa wameifanyia marekebisho. Ahha aaahaha teh teh teh..
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mchungaji Hiii ndio, tunaita great thinking na hii imefika mkuu.

  Respect.


  FMEs!
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Hapana, CCM ya leo siyo chama chama cha wakulima na wafanyakazi. Ni chama cha mafisadi (ghala) wanaotumia wakulima (jembe) na wafanyakazi (nyundo) kujinufaisha bila wao wenyewe kujionyesha hadharani.

  Nembo ya CCM inaonyesha nyundo na jembe bila kuonyesha ghala la mavuno yatokanayo na zana hizo mbili. Ghala hilo ndilo linalomiliki CCM. Kwa vile kwa kawaida ghala halitembei, basi mafisadi hawawezi kutemebea na kuondoka, ila wanaoweza kuondoka CCM ni wakulima na wafanyakazi wenyewe.
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  CCM kilijengwa kwa jasho la Wakulima na Wafanyakazi, hivyo mafisadi hawana haki yeyote kuwanyang'anya waliotoka jasho na damu kukiunda CCM.

  Kama wao walikuja huko baadaye na kukifadhili chama, ilikuwa si kwa ajili ya kulijenga Taifa au kukiimarisha Chama, bali ni kujiwekea mianya na njoa nyoofu ya kuweza kujitunishia mifuko yao kwa kutuhujumu kwa kutumia dola na upindishwaji wa Sheria na kanuni.

  Walichokifanya ni kwa manufaa yao na si manufaa ya Watanzania na wanachama ambao ni Wakulima na Wafanyakazi.

  Mafisadi na Ufisadi ni Wanyonyaji na wanaimarisha Unyonyaji, sawa na minyoo inayokaa tumboni mwa kiumbe na kujishibisha chakula cha kiumbe huyu, au kupe anayeng'angania ngozi na kufnyonza damu kama si kunguni anayejificha kwenye godoro naye akisubiri mwenye godoro alale ili ajishibishe!
   
 6. Sungi

  Sungi Senior Member

  #6
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huu ni mjadala mzuri Mch. Kishoka. Niliwahi kusema hapa wakati wa nyuma kwamba kinachotakiwa kwenye CCM ni "Nyerere revolution". CCM ni ya wanachama na sio hawa watu wachache walioteka chama kwa ajili ya maslahi yao binafsi, wamejilimbikizia fedha kwa njia zisizo halali na ndizo zinawafanya ku "call shots" na kuwa na makundi yanayowaunga mkono ndani ya chama, sio kwa sababu ni viongozi makini, bali ni kwa sababu wanafedha nyingi!

  Marekebisho yameanza hasa kwenye kura za maoni kwa wagombea wa ngazi za udiwani - urais. Wanaopiga kura sio wajumbe wachache bali wanachama wote wa CCM, pengine ni mwanzo kusaidia kupigana na mambo ya rushwa, maana kama utagawa fedha kwa watu wakupigie kura, itabidi uwahonge watu wengi zaidi, na sio wote watakuwa na fedha za kufanya hivyo, ingawa baadhi ya watu wachache walio na fedha nyingi bado wataweza. Ninatamani chama kirudi tena kuwa na maana halisi ambayo CCM ilisimamia na kuleta heshima kwa mtanzania.

  Tutaweza kuwavua uanachama wanachama ambao wanakiuka maadili ya chama na sio viongozi wa chama wanaojaribu kurudisha chama kwenye mstari kwa ajili ya maslahi ya mwanachama mtanzania na nchi yetu kwa ujumla.
   
 7. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  CCM ni chama cha CHUKUA CHAKO MAPEMA, ndio maana mafisadi wamejaa. Si chama cha wakulima na wafanyakazi kamwe, bali ni chama cha baadhi ya viongozi wakiingia madarakani tu wanachukua chao mapema(ufisadi) badala ya kulitumikia taifa.
   
 8. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  CCM ya mwaka 1977 sio CCM ya mwaka 2009, Iliyokuwa CCM miaka hiyo ya nyuma imetekwa nyara na kundi la watu wachache ambao aidha kwa makusudi wameamua kuizika Katiba ya CCM ya awali na kujitengenezea katiba yao ambayo mwongozo wake na matokeo yake ndiyo hayo tunayoyaona na kuyasikia nyakati hizi ama baadhi ya wanaojidai CCM damu hata hiyo katiba anzilishi pengine hawaijui achilia mbali kuisoma.

  Kama CCM ya mwanzo ilijua fika kuwa wakulima na wafanyakazi ndiyo Taifa na lazima waheshimiwe na kuheshimiana wao kwa wao, hilo halipo kwa sasa na CCM hiyo haipo pia. Cha kufanya ni walengwa wa awali (wakulima na wafanyakazi) kutambua kuwa wameshaachwa njiani na kuwa hawana kiongozi wa kuwaongoza kwa sasa hivyo ni lazima kwa ujumla wao waamue njia ya haraka na ya dharura kuhakikisha kuwa wanajinasua kutoka pale walipoachwa.

  WAKULIMA NA WAFANYAKAZI WA TANZANIA, CCM HAIWATAMBUI KWA SASA. NI VYEMA HILO LIKAFAHAMIKA KWENU NYOTE NA KUFANYA MAAMUZI YA KUHAKIKISHA YALE YALIYOLENGWA AWALI YANAFIKIWA, WANAOJIFANYA VIONGOZI NDANI YA CCM SIO WENZENU, MNADANGANYWA, LING'AMUENI HILO SASA, "CCM SIO YA WAKULIMA NA WAFANYAKAZI".
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mchungaji, Muasisi wa Chama Cha Wakulima na Wafanyakazi naye anaghani hivi:

  Na Chama cha Mapinduzi.
  Watambue Viongozi,
  Ni Chama cha Muungano,
  Si Chama cha Utengano.

  Kama mwanachama wake,
  Hazipendi sera zake,
  Atoke, asichelewe,
  Aanze chake mwenyewe.

  Kama Viongozi wetu
  Hawapendi sera zetu,
  Watoke waende zao,
  Waanzishe vyama vyao

  Viko vyama bozibozi
  Vyatafuta viongozi
  Waende waviongoze
  Na hiki tukipongeze

  WASITEKE CHAMA NYARA
  WAKILAZIMISHE SERA
  AMBAZO KATU SI ZAKE,
  NI ZA WAPINZANI WAKE.

  - 'Tanzania! Tanzania' - J.K. Nyerere, 1993, Uk. 33, TPH
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Sisi M kiliacha kuwa chama cha wakulima na wafanya kazi tangu JKN alipoacha uenyekiti wa chama chenyewe, na hapo kili cease kuwa chama cha wananchi tena na kuwa cha wenye nchi!
   
 11. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ukiangalia composition ya CCM , ni mchanganyiko wa watu wa aina mbalimbali ambao kwa uhalisia hawaendani na kushabihiana na chama chenyewe. Wengi wao ni watu maarufu kama waganga wa kienyeji, wanamichezo, wafanyakazi,wafanyabiashara(asilimia kubwa) katika kundi la wafanyabiashara ndio unaweza kukutana na watu wanaopiga ishu za haramu kama vile madawa ya kulevya, ujambazi na ufisadi kwa kushirikiana na wafanyakazi wa serikali wasio waaminifufu. Na kwa kiasi kikubwa wameweza kukiteka chama kwa kutoa bakshishi, posho, michango na kubuni miradi hewa ambayo wao wanadai kwamba inakisaidia chama kumbe ni kwa faida yao(rejea mkataba wa ujenzi wa jengo la Umoja wa Vijana- na Estim Construction).
  Kundi hili la wafanyabiashara lipo kwa ajili ya kutetea na kulinda maslahi yao na wanaweza kutumia pesa yao kumweka madarakani wamtakaye atakayelinda na kutetea maslahi yao.

  Kundi lingine ni la watumishi waandamizi wastaafu wa umma pamoja na wafanyakazi waandamizi wa mashirika ya umma wastaafu ambao ndani yao kuna wasomi (Maprofesa, Madaktari n.k). Moja ya vitu ambavyo vinawafanya wao kugombea ni kutaka kuwakwamua wananchi wa majimbo yao na umaskini na kuwaletea maendeleo wakati mashirika yao wamefilisi. Angalia akina Mwapachu(Bima, ATC n.k), Elisa Mollel (NMC) na listi haiishii hapo. Sasa katika kundi hili unaweza kuwakuta watu wanajiita wao ni makada wa chama, waasisi, watoto wa Nyerere ,wao wanakijua chama n.k n.k Lakini kwa wakati huo ni kwamba wanajua kwamba uraiani hakufai na hivyo wanalinda maslahi yao na pia wanahofia vimeo kwani makaburi yakifufuliwa wamekwenda na maji.

  Watu hawa wanajikuta kwamba sasa wamefunikwa na kundi la wafanyabiashara ambao kwa namna moja au nyingine ndio wanakiwezesha chama kwa kufadhili mambo mbalimbali kuanzia mikutano midogo mpaka ile mikubwa. Kwa kugharamia masurufu mbalimbali kama nilivyoeleza hapo awali. Pamoja na kufadhili chama katika uchaguzi mkuu. Swali ambalo inabidi tujiulize kwa nini wakifadhili Chama Cha Mapinduzi badala ya kufadhili maendeleo na miradi mbalimbali ya wananchi? Manake pesa tunayoisemea hapa sio Milioni 100 au 200 hizo ni peanut. Hapa tunasemea mabilioni ya shilingi. Na mara nyingi pesa hizo hutumika katika michezo michafu ya kisiasa.

  Kinachoonekana bungeni na hii ajenda ya ufisadi ni kama mchezo wa kuigiza lakini ukweli utabaki palepale. Wapo wanasiasa wafanyakazi wastaafu waandamizi Vs wafanyabiashara wanasiasa. Na katika kundi hili la wanasiasa na watumishi wa Umma wastaafu unaweza kumkuta Mzee Malecela na wengineo ambao hawajulikani. Hivi wewe unaweza kujiuliza kuwa Anna Kilango amepata wapi jeuri ya kuongea hovyo bungeni? Kama sio back up ya Mzee. Na uelewe kwamba Mzee ana support.Samuel Sitta kufanyiwa character assassination na kumdhalilisha kama hafanyi kazi yake sawa sawa bungeni ni kutokana na vita hivyo vya chini chini. Sitta yeye ni product ya hawa Wazee waandamizi wastaafu wa chama hayuko katika kundi la wafanyabiashara.

  Kwa hiyo nikijaribu kuweka puzzle zangu sawa sawa, katika kundi hili la wafanyabiashara linafanya mambo yake ya chinichini kwa kushirikiana na wanasiasa wanamtandao. Kwa sababu siasa ni unafiki na uzandiki na wafanyabiashara wapo katika maslahi yao . Unadhani atakimbilia na kumkumbatia yule anayepiga vita maslahi yake na asiye na madaraka? Wao wanajua kitu gani cha kufanya na kwa wakati gani.

  Upande mwingine unakutana na wanasiasa Wazanzibari ambao wanaona kama wamefunikwa nao siasa zao za chinichini. Yaani CCM ukianza kuichambua utachanganyikiwa kwa sababu wao ni kwamba aliye katika madaraka ndiye. Wanachama Hawaangalii mustakabali wa chama na hawana maamuzi tena. Mzee Kingunge ni Bendera fuata upepo ambaye hata hivyo anakula kote kote katika kundi la wanasiasa wastaafu na wanamtandao. Ukiangalia katika macho ya wengi utagundua kwamba watu wanaichukulia kwamba watu ambao hawako katika Mtandao ni wale ambao ama walitengwa au kuonekana hawana umuhimu wakati wa utawala wa Mkapa. Hilo sio la kweli. Suala hili la kimtandao limejikita kibiashara zaidi na sio kisiasa kama siasa ingawa mwisho wa siku kila mmoja anapata la kwake analolihitaji nalo ni kuifisadi Tanzania na Wananchi kwa kuhakikisha madaraka na dola viko mikononi mwao.
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  "CCM ni sawa na watu waliotuibia ng'ombe na kutajirika kutokana na ng'ombe hao. Kisha kila misimu ifikapo (chaguzi) wanahakikisha kuwa ng'ombe hao wanatoa maziwa na wana ndama wa kunyonyesha na kuendeleza kizazi, hivyo wanaanza kutuletea maziwa na jibini kama zawadi (kanga, pipi, kofia, fulana). Kwa vile tunakuwa hatujanywa maziwa wala kula jibini muda mrefu, tunatahamaki kwa hamu na baadhi uchu katika kupata hayo maziwa na jibini. Tunasahau kabisa yakuwa mazao hayo yote yanatokana na ng'ombe wetu walio waiba msimu mmoja au miwili iliyopita"
   
  Last edited: Aug 27, 2009
 13. T

  T_Tonga Member

  #13
  Aug 24, 2009
  Joined: Jul 24, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani hamjaelewa maana ya jembe na nyundo kwenye nembo ya ccm nyundo maana yake mpige mlala hoi afe jembe maana yake mchimbie kaburi uumzike hiyo ndio maana yake
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,323
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Huu ndio ukweli...CCM ni chama ambacho kimesheheni historia nzima ya Taifa letu. Lakini, ikafika mahala kuna watu wakatamka eti kama unataka mambo yako yawe mazuri basi ingia CCM. yakaingia hata Majambazi kukifadhili chama na ndio matatizzo yote yalipoanza. Namna pekee ya kujinusuru ni kukisafisha hiki chama.Naamini, bado sera na nia ya kuanzishwa kwake haina ubaya na Taifa letu
   
 15. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Unaposikia wakuu wa CCM wanadai kuwa Bunge ni lao, mithili kuwa ni mali yao binafsi, inabidi ujiulize, je katiba ya CCM inasemaje kuhusu utii wa Katiba ya Jamhuri?


  Je katiba ya CCM ina nguvu kuliko katiba ya Jamhuri?
   
 16. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mawazo nje ya kiboksi chetu...

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=DioQooFIcgE[/ame]
   
 17. idumu

  idumu Member

  #17
  Aug 27, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WATANZANIA WAJINGA, NGOJA TULIWE MAFISADI HWALIPI BILL YA UMEME< MAJI NA KODI ZOTE, wa hali ya chini
   
 18. Freddy81

  Freddy81 Member

  #18
  Aug 27, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo hiki chama kina wababe ambao wanasauti na wanaweza wakawatisha watu, lakini kwa sasa hawana mkono wa Mwenyekiti ndo mana mambo yanaanza kubadilika, halafu hawajui tu kuwa muda wao unakaribia kwisha... siku zote mabadiliko lazima yaje na gharama zake, watnyooshwa tu. Tena naomba iwe hata kabla ya hao wanaojifanya wababe hawajafa ili wakionje cha mtema kuni
   
 19. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka tatizo unachanganya kati ya TANU na CCM. Hawa ni wawili tofauti. Kwani wewe ni sawa na baba yako......

  TANI ilijenga nchi, CCM ikabomoa, tena kwa kishindo cha Tsunami.....

  omarilyas
   
 20. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,517
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Mkuu ahsante sana kwa kuhuisha imani yangu juu ya Chama changu ambacho kila mara nisomapo Katiba yake, sioni ubaya wake. Sasa naingia mtaani Full Mzuka na hata SWAUMU YENYEWE WALA SIISIKII TENA.

  ALUTA CONTINUA!!!!! Watupishe!!! Watupishe!!!! Watupishe!!! Watuachie CCM yetu!!!!! Aaaaaaaagh!!!
   
Loading...