mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Wanaccm wenzangu nimeshindwa kuvumilia hii tabia iliyozuka ya kuwatukana wanaccm wenzetu walioamua kujitoa uanachama Kwa sababu zao.Tukumbuke kuwa kujiunga Na chama ni hiari vivyo hivyo Na kujitoa.Baya zaidi huyo aliyejitoa CCM alikuwa kiongozi ktk chama Na kuna mazuri amekitendea chama.Leo tumeamua kumtukana je Kesho akiamua kurudi tutaendelea kumtukana au tutakaa kimya? Wanaccm tuwe Na sura ya aibu tuwe Na fadhira .Kuna wakati Hayati baba wa Taifa alitishia kujitoa CCM je kuna mwanaccm angethubutu kumtukana? Cha kusikitisha zaidi kuna viongozi wakubwa wa chama ndio wanaongoza kutukana Na wengine wana muda mfupi ndani ya chama jamani tuache tabia chafu CCM ni chama kikongwe .