CCM iwe makini na mabadiliko ya Tabia nchi, tishio la ukame na njaa siyo la kulipuuza kisiasa na kiuchumi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,508
141,232
Kada mkongwe mzee Mgaya ametoa rai kwa chama chake CCM kutopuuza tishio la ukame kama ilivyoripotiwa na TMA.

Mzee Mgaya anasema Watanzania hawajazoea njaa na endapo itatokea hali kama ya mwaka 1980 tulipokula ugali wa yanga na ule mweusi wa unga wa mtama basi mustakabali wa CCM utakuwa mashakani.

Ni lazima serikali inunue mahindi yote ya wakulima wetu na kuyahifadhi badala ya kuyauza nje ya nchi, anasema.

Mtanzania akiwa na njaa hadanganyiki kwa pipi, amemalizia Mgaya

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Leo umeandika sense for the whole year. Kweli ukame unatishia maisha. CCM wako kwenye urais 2025.

Udigoni ngombe wameanza kufa kwa ukame (nasikia), kama ni kweli tunakwenda kubaya. Tanga Mjini na maeneo yanayozunguka mji huu, ukame unatishia kila kitu. Ngombe wako at a blink of starvation kama mvua hazitanyesha.
 
1980 tulipata msaada wa mahindi ya njano kutoka Brazil lakini safari hii kuna Corona!
 
Sure tuliyala sana! Nilikuwa nasoma shule nakumbuka sana. Nadhani na wewe kama ulikuwa kijana enzi hizo utakuwa uliula sana huo ugali wa njano! Corona imepungua utakuja tu!

Huku ng'ombe watakufa kama haitanyesha mvua.
 
Kuna nini najiuliza?

Kipindi cha kikwete hali ya ukame ilikuwepo sehemu nyingi Nchini

Kipindi cha JPM mvua nyingi sana hadi mafuriko.

Kipindi cha SSHasani naona hali ya ukame na chakula kupanda bei kimeanza tena.

Kuna nini?
 
Ushauri mzuri hata Chief Hangaya aliligusia Kwenye hotuba yake kule UNGA.

Ila sasa Mzee sijaelewa linakuaje ni iwe ajenda ya ccm badala ya kuwa ajenda ya Nchi na Serikali?

Kuna ukame unanyemelea mwaka huu Kwa mujibu wa TMA na mafuriko kama huko Sudan.

Tuanze kuchukua hili kama ajenda mtambuka,swala la ukimwi sasa like pembeni lije la utunzaji mazingira.
 
ukifanya kazi nzuri inasifiwa. Leo Mgaya kaandika sense.. na huyo kapongeza

Leo Mzee kaandika kwa sababu serikali inanunua mahindi ikilenga kufanya biashara na WFP hasa kupeleka South Sudan , Somalia, na nchi nyingine zenye baa la njaa tayari, hasa wasinogewe na dollari za UN wakauza yote wakasahau hali itakua tete na dalili zinajionesha wazi kwa mfano mkoa wa kagera kiasi cha mvua kimepungua sana miezi hii tofauti na miaka ya nyuma
 
Leo umeandika sense for the whole year. Kweli ukame unatishia maisha. CCM wako kwenye urais 2025.
Udigoni ngombe wameanza kufa kwa ukame (nasikia), kama ni kweli tunakwenda kubaya. Tanga Mjini na maeneo yanayozunguka mji huu, ukame unatishia kila kitu. Ngombe wako at a blink of starvation kama mvua hazitanyesha.
Sasa CCM ndio wameleta ukame? Swala hili limeletwa na wazungu huko sisi ni wahanga ,Rais alipozungumzia kule UNGA kuna watu mlimbeza sasa hivi mnasema CCM CCM.

Mwendazake anhewachana live kwani yeye ndio kaleta. Ukame?
 
Sasa kwa mustakabali huo na ushauri wa mzee mgaya Muyangu, serikali lazima iwaze mara mbili mbili
 
Leo Mzee kaandika kwa sababu serikali inanunua mahindi ikilenga kufanya biashara na WFP hasa kupeleka South Sudan , Somalia, na nchi nyingine zenye baa la njaa tayari, hasa wasinogewe na dollari za UN wakauza yote wakasahau hali itakua tete na dalili zinajionesha wazi kwa mfano mkoa wa kagera kiasi cha mvua kimepungua sana miezi hii tofauti na miaka ya nyuma
Bodi ya nafaka ndio yenye kufanya biashara NRFA wananunua kwa ajili ya hifadhi ya chakula
 
Ushauri mzuri hata Chief Hangaya aliligusia Kwenye hotuba yake kule UNGA.

Ila sasa Mzee sijaelewa linakuaje ni iwe ajenda ya ccm badala ya kuwa ajenda ya Nchi na Serikali?.

Kuna ukame unanyemelea mwaka huu Kwa mujibu wa TMA na mafuriko kama huko Sudan.

Tuanze kuchukua hili kama ajenda mtambuka,swala la ukimwi sasa like pembeni lije la utunzaji mazingira.
Bwashee Wafanya maamuzi wa serikali ndio hao makada wa CCM!
 
Kuna nini najiuliza?
Kipindi cha kikwete hali ya ukame ilikuwepo sehemu nyingi Nchini

Kipindi cha JPM mvua nyingi sana hadi mafuriko.

Kipindi cha SSHasani naona hali ya ukame na chakula kupanda bei kimeanza tena..

Kuna nini?
Kila miaka 5 kunakuwa na mabadiliko fulani ila msijali siku mkija kusikia Nyanda za Juu Kusini hakuna mvua basi hameni nchi mtakufa wote but so long as huku mvua ipo na ndiko kwa wazalishaji wakuu tutawalisha.

Alafu msilete hofu za kijinga zikapelekea bei za vyakula kupanda Kwa hisia tuu.
 
Leo umeandika sense for the whole year. Kweli ukame unatishia maisha. CCM wako kwenye urais 2025.
Udigoni ngombe wameanza kufa kwa ukame (nasikia), kama ni kweli tunakwenda kubaya. Tanga Mjini na maeneo yanayozunguka mji huu, ukame unatishia kila kitu. Ngombe wako at a blink of starvation kama mvua hazitanyesha.
Uyo ni mwezi mchanga,
 
Kwani ukame unatuhusu nini si tulikubaliana sisi ni matajiri wa madini ka maliasili mbona mnaomba poo fasta
 
Hahahaaaa....... Wewe ni bamvua!
Ha ha ha haaaaah!
giphy.gif
 
Back
Top Bottom