CCM iwaambie Wananchi ilivipataje viwanja inavyovimiliki wakati haikuvijenga bali wananchi walichangishwa

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Ukweli usio na Mashaka Serikali imeomba kuidhinishiwa Pesa kwa Ajili ya Kukarabati Viwanja vya CCM
Najiuliza CCM ilivipata wapi hivyo VIWANJA?

CCM lini ilitangaza MKANDARASI wa kujenga hivyo VIWANJA?

Kwanini CCM itumie KODI za Wananchi wakati ina RUZUKU kubwa?

Ukweli ni Kwamba CCM haijawahi Kutafuta hivyo VIWANJA wala Kuvijenga VIWANJA vyote vimejengwa na Wananchi kwa Kushirikiana na Serikali chini ya WAKUU wa MIKOA na WILAYA

Mfano Viwanja vya NELSON MANDELA Sumbawanga mpaka MANESI na WAKIMBIZI wa KIHUTU walichangishwa Chini ya RC Tumainieli KIWELU

Uwanja wa SOKOINE na KIRUMBA Mwanza Watu walitoa Ngombe Mazao na Pesa leo iweje CCM bila AIBU iseme viwanja ni vyake na pia vikarabitiwe na Serikali ?

VIWANJA vilijengwa na Wananchi bila ITIKADI ya Chama hivyo VIRUDISHWE kwenye MAJIJI MAMISPAA MIJI na WILAYA ile view vya UMMA ni AIBU kwa CCM KUPORA VIWANJA VYA UMMA
 
Ifikie wakati wajisikie aibu na hivyo kuvirudisha viwanja vyote walivyo kwapua kinyemela, ili vikarabatiwe na kuwekwa chini ya usimamizi wa Halmashauri zetu.
 
Hivi malalamiko kwenye vyama vya ushirika vya mazao (Amcos) yalifikia wapi kuhusu kuporwa kwa baadhi ya maghala na CCM?

Au CCM ile iliyoshika dola enzi za hayati comred JPM si CCM ya sasa?
 
Tulieni vumilieni kwanza serikali ikishavikarabati ndo muanze hamasa na harakati zenu za mlipuko kama zile za kukataa mtandao wa Voda.
 
Mambo mengine hayawezi tusaidia.
Hatuwezi kwa njia yoyote kuwanyanganya CCM hivo viwanja

TANU walirudisha hili jengo kwa serikali. Ni muda tu.
KICC_nairobi_kenya.jpg
 
Tulieni vumilieni kwanza serikali ikishavikarabati ndo muanze hamasa na harakati zenu za mlipuko kama zile za kukataa mtandao wa Voda.
Halafu we jamaa una mawazo duni sana ! uliingiaje jf ? unatia aibu sana ! na kwa kweli hasara aliyopata mama yako haipimiki , moderator nisaidieni Ku ignore huyu mtu duni anaweza kuniletea matatizo hapa jukwaani .
 
Viwanja vilijengwa kabla ya 1992 ambapo mfumo wa kisiasa ulikua wa chama kimoja.

Vilijengwa kwa mgongo wa "Chama na Serikali".

Hivyo CCM inahusika moja kwa moja.
Mgongo wa chama na serikali!? Kwa nini viwe mali ya ccm pekee na sio ubia wa ccm na serikali!?
 
Viwanja vilijengwa kabla ya 1992 ambapo mfumo wa kisiasa ulikua wa chama kimoja.

Vilijengwa kwa mgongo wa "Chama na Serikali".

Hivyo CCM inahusika moja kwa moja.
Chukueni pia shule zote zilizojengwa kabla ya mwaka huo.
 
Back
Top Bottom