Dunia yakoo
Senior Member
- Nov 23, 2019
- 139
- 214
CCM IWAACHIE WANA-CUF INAOWASHIKILIA LIWALE NA KUWABAMBIKA KESI NGUMU
CCM inajua kwamba haikushinda Uchaguzi Jimbo la Liwale na kwenye kata nyingi za Jimbo hilo. CCM ilitumia Vyombo vya dola kuvuruga Uchaguzi ule kama ilivyofanya maeneo mengine nchini.
Pamoja na kupora Ushindi na kusababisha vurugu, bado imewabambika Viongozi na wanachama wa CUF kesi ya UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA ( Armed Robbery), ambapo zaidi ya wanachama 14 wanashikiliwa kwa Kesi hiyo ya Kubambikiza. Kwa kuwa CCM iliamua kupora Ushindi na ikafanya hivyo, kuendelea kuwashikilia raia hawa ambao inajulikana wazi kwamba hawahusiki na kusababisha au kufanya vurugu waliyoiandaa ili wapoke Ushindi, ni Jambo baya sana LINALOWEZA KUPELEKEA CHUKI KUBWA IKATUATHIRI NDANI NA NJE Kama Taifa.
Serikali ya CCM ni vema ikatambua kwamba hiki nacho ni kielelezo kinachoweza Kutumika popote duniani kufafanua Ubakaji wa Demokrasia na Utawala wa Kimabavu usiozingatia Sheria. Tunatoa wito kwa wanaohusika wawaachilie na kuwafutia kesi wanachama hawa wasio na hatia ili Maisha mengine yaendelee.
Bado tunasisitiza na tutaendelea kusisitiza kwamba Amani ni tunda la haki.
HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!
Eng. MOHAMED NGULANGWA
Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF - Chama Cha Wananchi
Desemba 2, 2020.