CCM iwaachie wana-CUF inaowashikilia Liwale na kuwabambika kesi ngumu

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
122
250
CCM IWAACHIE WANA-CUF INAOWASHIKILIA LIWALE NA KUWABAMBIKA KESI NGUMU

CCM inajua kwamba haikushinda Uchaguzi Jimbo la Liwale na kwenye kata nyingi za Jimbo hilo. CCM ilitumia Vyombo vya dola kuvuruga Uchaguzi ule kama ilivyofanya maeneo mengine nchini.

Pamoja na kupora Ushindi na kusababisha vurugu, bado imewabambika Viongozi na wanachama wa CUF kesi ya UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA ( Armed Robbery), ambapo zaidi ya wanachama 14 wanashikiliwa kwa Kesi hiyo ya Kubambikiza. Kwa kuwa CCM iliamua kupora Ushindi na ikafanya hivyo, kuendelea kuwashikilia raia hawa ambao inajulikana wazi kwamba hawahusiki na kusababisha au kufanya vurugu waliyoiandaa ili wapoke Ushindi, ni Jambo baya sana LINALOWEZA KUPELEKEA CHUKI KUBWA IKATUATHIRI NDANI NA NJE Kama Taifa.

Serikali ya CCM ni vema ikatambua kwamba hiki nacho ni kielelezo kinachoweza Kutumika popote duniani kufafanua Ubakaji wa Demokrasia na Utawala wa Kimabavu usiozingatia Sheria. Tunatoa wito kwa wanaohusika wawaachilie na kuwafutia kesi wanachama hawa wasio na hatia ili Maisha mengine yaendelee.

Bado tunasisitiza na tutaendelea kusisitiza kwamba Amani ni tunda la haki.

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!

Eng. MOHAMED NGULANGWA
Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF - Chama Cha Wananchi
Desemba 2, 2020.
 

ZOPPA

JF-Expert Member
Jan 20, 2017
2,636
2,000
Kila lenye mwnzo alikosi kuwa na mwusho .mwisho wao utafika tu ngoma ikilia sana inakalibia kupasuka.
 

Ryaro wa Ryaro1233

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
353
1,000
Kama ni Wanachama wa CUF basi Prof. Lipumba aende Magogoni Kitaeleweka soon. Kumbuka Prof. ambaye ndiye mmiliki wa CUF, ana mafungamano na Utawala wa sasa. So aende mambo yaishe.

Sheltani Hana Rafiki Waenga walisema. CUF kumbukeni kuwa 2015 Prof. wenu alipewa TRIP ya Kigali ili Kufifisha Harakati za Ukombozi so Mtulie tu Sindano inaingia taratibu. CUF inajulikana ni Miongoni mwa vyama Maslahi kwa Sasa, Tulieni Mkinywee Kikombe cha SiSiEM.
 

Sandali Ali

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
5,788
2,000
Huu uliofanywa na CCM ni uovu kama uovu ule uliofanywa na Lipumba wa kutumia dola kuiharibu CUF halisi miaka michache iliyopita.
 

Dunia yakoo

Senior Member
Nov 23, 2019
122
250
Kama ni Wanachama wa CUF basi Prof. Lipumba aende Magogoni Kitaeleweka soon. Kumbuka Prof. ambaye ndiye mmiliki wa CUF, ana mafungamano na Utawala wa sasa. So aende mambo yaishe. Sheltani Hana Rafiki Waenga walisema. CUF kumbukeni kuwa 2015 Prof. wenu alipewa TRIP ya Kigali ili Kufifisha Harakati za Ukombozi so Mtulie tu Sindano inaingia taratibu. CUF inajulikana ni Miongoni mwa vyama Maslahi kwa Sasa, Tulieni Mkinywee Kikombe cha SiSiEM.
Hayo ni mawazo mgando....baada ya hapo ruwasa alibaki chadema....prof aliwambia watanzania CCM ina wagombea wawili baadae chadema wakabaki na aibu ruwasa kurudi kwao.

Watanzania ukweli Kwwtu ni simu.
 

Papy ndombe

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
3,764
2,000
Yule bwana furaha yake ni kuona machozi ya watu wakilia na kuteseka uburudisha Sana moyo wake.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,974
2,000
Moja ya Sifa Mama ya Mtu mwenye Cheo cha Uenezi ni kufanya Propaganda hasa ile ya Kupika ( Kutengeneza ) Uwongo ili Kumchafua Fulani pia.
 

antimatter

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
21,476
2,000
"Mi5 tena" imegeuka mateso kwa taifa.

Kule Arusha wamebambikiziwa kesi za uhujumu uchumi.

Wanatengeneza kesi zisizo na dhamana ili wahanga wasio na hatia wakae tu ndani.

 

antimatter

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
21,476
2,000
Vyovyote vile....leta hoja siyo kubabaisha mambo....Tar 20/12/2020 karibuni sana kwenye KONGAMANO LA uzinduzi wa mchakato wa kudai KATIBA mpya.
Litafanyikia wapi hilo kongamano?
Wazungumzaji wakuu ni kina nani?
Policcm hawatasambaratisha kabla ya kuanza?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom