Mbunge wa CCM
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 475
- 24
ndugu watanzania wenzangu
kwanza nichukue nafasi hii kuwapongeza na kuwatakia utumishi mwema wenye mafanikio mawaziri wote walioteuliwa katika wizara mbalimbali pamoja na wasaidizi wao. nawahalkikishia pia ushirikiano wangu katika kutimiza majukumu yemnu mliyokabidhiwa kwa manufaa ya serikali ya CCM na taifa zima kwa ujumla.
hivi karibuni tumeshuhudia gumzo pana na refu lililohusishwa na kitendo cha wabunge wa chadema kutoka nje ya ukumbi wa bunge mjini dodoma wakati mh. rais akianza kusoma hotuba yake ya kuzindua bunge la 10.
binafsi niseme wazi kuwa sikushtuka wala kushangaa. nilikuwa nimeishajiandaa kwa tukio lile kwani ilishajulikana kuwa ingekuwa vile. ila nilichoona ni kuwa kuna mambo ambayo wanaCCM tunapaswa kujifunza na kuwa tayari kama tunataka chama chetu kivuke wimbi hili la mabadiliko. mambo hayo ni kama ifuatavyo
1. kupeleka itikadi ya chama kwa kundi la vijana amabo wanonekana kushabikia mambo wasiyoyajua vizuri hali inayotafsiriwa kuwa vijana hawakitaki tena chama cha mapinduzi japo uzoefu unaonyesha kuwa vijana wamekuwa hawatabiriki siku zote na katika nchi mbalimbali
2. chama kijikite katika kujenga taswira ya kuaminika machoni pa wananchi ikiwa ni pamoja na kujiweka kando na matendo yanayoweza kukiunganisha na mamabo yanayopigwa vita nchini kwa sasa kama ufisadi nk.
3. chama kupitia serikali yake kijitahidi kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo inayotokana na ilani yake ya uchaguzi ili kidhihirishe kwa vitendo utashi na uwezo wa kusimamia juhudi za kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini
4. kwa wakati huu chama kijitenge kabisa na hatua yoyote ya kukaa na chadema ama chama chochote kingine kujadili jamabo lolote la kitaifa na iwapo itaonekana vyema basi chama kichukue hatua chenyewe bila kushirikisha chamas kingine
5. chama kiimarishe ushirikiano na vyama vya CUF na vingine vilivyo vidogo ili kujihakikishia kuungwa mkono na wadau anwai wa maendeleo
6. juhudi zisizo za dhahiri sana zifanywe kwenye idara za usalama wa taifa na vyombo vingine vya dola kuweka mizania ya chokochoko za udini, ukabila na uzanzibari katika urari ili kupunguza taratibu na hatimaye kumaliza kabisa hofu iliyoanza kujengeka ya kukua kwa hali hizo zisizoendana na utamaduni wa siasa zetu
7. mwenge wa uhuru utumike kuimarisha uzalendo na uwajibikaji wa raia katika kushiriki michakato mbalimbali ya kidemokrasia na kuamsha ari ya kisiasa kwa wale amabo ari hiyo imeshuka (rejea idadi ndogo ya watu waliojitokeza kupiga kura)
8. kujitahidi kulipatia ufumbuzi suala la mambi ya kuasisiwa mchakayo wa kuandikwa katiba mpya lakini bila uharaka na kupeleka turufu yake kwa wapinzani wa CCM
kuna mengi, lakini kwa haya machache niseme kuwa Tanzania yenye ufanisi tele inawezekana chini ya CCM
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZU