CCM Itambue Upinzani ni dhana pana ambayo huiwezi kuifuta kwa kuhamisha madiwani wa upinzani.

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,562
15,906
Nashangazwa sana na huu mtindo wa CCM kuhamisha madiwani wa vyama vya upinzani kwa matarajio kwamba wanaua upinzani. Nataka niwashauri jambo dogo sana ni sawa kwa namna moja au nyingine wanaweza kudhani kuwa wanauwa upinzani ( kwa akili za kisisiemu).

Lakini upinzani utakaozaliwa utakuwa mbaya zaidi ya huu uliopo. kwa maana nyingine ni kwamba kutakuwa na upinzani wa ndani kwa ndani ambao upo kwenye mfumo uliopo madarakani.upinzani huu ni hatari zaidi ya Chadema.

Otherwise itumike nguvu ya ziada kuuzima kitu ambacho sina uhakika kama kitafanikiwa kwa sababu madhara yake yanaweza kuwa makubwa sana na kuitumbukiza nchi katika majanga mazito.

Kwahiyo labda tu ni niwashauri CCM kucheza kwa step maana hali ya sasa ni tofauti na miaka ya nyuma hivi sasa watanzani wengi wameamka na wanajua mambo yanavyokwenda.
 
mnalialia nini wakati madiwani wenu wamechoka ulaghai na usanii wa viongozi wa chama chenu?

CCM haiwezi kuwalea kwa miaka 20 hata mtoto akizidisha miaka 18 anatambulika kama ni mtu mzima.
 
sijonze na slowslow wana siasa za kishamba hiyo project ya kununua madiwani na wabunge itawagharimu sana ,Tanzania inaweza nyimwa misaada na vikwazo
licha ya misaada na vikwazo. upinzani siyo chadema wala cuf au act. upinzani ni kuwa na mentality tofauti. tumeshaona wengi tu ndani ya ccm wenye mawazo tofauti na magufuli. upinzani wa namna hii ni mbaya sana kwa sababu upo ndani ya mfumo.
 
Back
Top Bottom