Kaiche
Senior Member
- Jan 23, 2017
- 141
- 269
CCM MPYA lazima itaendelea kupata misuko suko kama ilivyokuwa kwa TANU chini ya Mwenyekiti wa TANU-CCM Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
•Kabla ya 1961 hadi mapinduzi ya Zanzibar 1964, Mwaka 1958 kiongozi wa juu wa TANU Zuberi Mtemvu alitoka na kuanzisha chama chake cha ANC na TANU iliendelea kuwepo na kuwa imara zaidi.
•Mwaka wa 1967 Waziri mwandamizi wa serekali ya TANU Osca Kambona alijiondoa na TANU ilibaki imara zaidi.
•Mwaka 1959 ASP ilimtumbua Shamte na kuanzisha chama cha ZPPP na ASP ilikua imara na kujipanga hadi kufanya mapiduzi mwaka 1964.
•Mwaka 1984 CCM iliyotokana na TANU na ASP ilimvua madaraka aliekua Rais wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi na CCM wala haikutetereka.
•Mwaka 1984 CCM ilimfukuza Maalim Seif Sharif Hamadi na wenzake 6 CCM haikugawanyika.
•Mwaka 2014 CCM ilimfukuza uwanachama waziri wake mwandamizi(MNEC)Mansour Yusuph Humid na wala CCM haikubabaika.
•Mwaka 2015 CCM ilimfukuza uwanachama Hassan Nassor Moyo na CCM ikazidi kusonga mbele.
•Mwaka 2015 Edward Ngoyai Lowasa alikihama chama cha mapinduzi baada ya jina lake kukatwa ktk kinyang'anyiro cha Urais ndani ya CCM bado CCM ikazidi kuwa imara na kushinda uchaguzi kwa kishindo na kuendelea kuvuna mamia ya wanachama kutoka ktk vyama mbali mbali.
•Tarehe ya leo 30/10/2017 Lazaro Nyalando amekihama chama cha Mapinduzi na tunasema bado CCM itaendelea kuwa imara haitayumba wala kutetereka kwa hawa walafi wa madaraka kukihama chama kwa kukosa wao kuchaguli uwaziri.
•Nataka mfahamu kwamba CCM ina Viongozi wengi na wanaomdu uongozi na mikikimikiki na ndio moja ya sababu ya kuachwa na baadhi ya viongozi/wanachama maslahi, nafikiri hili linasaidia kutoa nafasi kwa wengine hasa wazalendo ili nao watowe mchango wao kwa taifa letu.
Nyarandu wasalimie uendako ktk kaburi la siasa unalojichimbia.
OMBI LANGU KWA WATANZANIA WAELEWA
Si lazima tukubali kila wanachotuambia hawa wanaohama CCM ambao kimsingi wanamaslahi yasiyoendana na yetu wala jamii yetu.
Mhe. Rais John Pombe Magufuli anaposema wasomi wengi wanatuangusha tuwe tunaelewa anachomaanisha.
Wasomi anaowamaanisha Rais. Magufuli ni wale wenye veti vya kujaza viroba kadhaa au masandukuni, na ndio maana anasema yeye msomi ni yule anayefanya ya kizalendo - yaani anayeisumbua akili yake ili ifanye kazi ya kujenga taifa.
Dhana kuu ya Magufuli ni yeyote anayestahili kuitwa msomi ni yule anayeufanya ubongo wake ufanye kazi, wakati wote uzunguke na kubaini kile kinachoendelea, utafute, uchambue, upime, upambanue, usaili, uzue, uainishe, utanzue na utohoe.
Hiyo ndio shughuli ya ubongo wa binadamu; sio kama ma-mbuzi, shughuli ya ubongo wa mbuzi ni kuliwa tu.
Mtazamo huu wa Rais Magufuli unatutaka watanzania tusiwe kama ma-mbuzi, haiwezekani baadhi ya makundi fulani hasa ya vijana na watu wazima wanaojichetua akili kuamini zaidi uongo kuliko ukweli, kushabikia zaidi mambo yanayolibomoa taifa letu kuliko kujenga.
Nimewakumbusha haya kwanza ili wasiojua CCM imetoka wapi angalau waondokane na upofu, upotoshwaji.
Kuhusu Lazaro Nyarandu nitaendelea Makala yangu ifuatayo.........