CCM isitulaghai watanzania eti wanachama watatu ndio wachafu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM isitulaghai watanzania eti wanachama watatu ndio wachafu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Thesi, Jun 28, 2011.

 1. T

  Thesi JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jana nimemskia katinu mkuu wa ccm Wilson Mukama akisema kuwa chama hicho kamwe hakitakubali kuchafuliwa kwa vitendo vya watu wachache; wawili watatu katika chama hicho. Eti kwa vitendo nya watu hao ndio chama hicho kionekane hakifai machoni mwa wananchi. Kwa maana hiyo watafanya maamuzi maghumu ya kujivua ghamba.
  Sina tatizo na CCM kufanya maamuzi maghumu. Nina tatizo na CCM kufanya maamuzi magumu kwa watu watatu tu. CCM haijachafuliwa na vitendo vya watu watatu tu. Si kwamba hao watatu waachwe lakin hawatoshi. Walioaribu maendeleo ya nchi yetu si hao watatu tu ila mfumo mzima wa CCM uliobeba viongozi wake wakuu wakiwemo kina Mkama. Mfumo mzima wa ccm unaokuza rushwa, ubadhirifu na ubabaishaji katika utendaji wa serikali. Ni utendanji wa chama hicho uliojenga wigo wa kutafuna pesa za serikali pasipo huruma yoyote. Hao watatu ni zao la mfumo huo mbovu na ni sehemu ndogo tu. Kutokana na mfumo huo mbovu wa ccm fedha za serikali zimekuwa kwa kiasi kikubwa zinahudumia mifuko ya watu badala ya kuingia kwenye miradi ya maendeleo. Hivo ccm kutuambia wananchi kuwa inajivua ghamba kwa kuwaondoa wanachama wake watatu ni ulaghai mkubwa. CCM ikitaka kujivua ghamba kwa mbinu ya kuwaondoa watu waliochafuka katika chama hicho ni lazima ianze na mkuu wa nchi Rais JK na kundi lillojenga wigo wa ulaji serikalini. Huyu tumemshuhudia akilea mfumo huo na kuchaguliwa kwa mfumo huo. Ni Kikwete aliyechaguliwa kuwa rais kwa kukwapua fedha za EPA kumfanyia kampeni akiwatumia hao hao wanaotaka kutolewa kafara. Si kwamba nawatetea RACHEL. Wanafaa kupelekwa mahakamani hata sasa lakini si wao tu. Tumeshuhudia wanasiasa wanakuwa matajiri kwa muda mfupi baada ya kupewa nyadhifa serikalini, utajiri usioendana na kipato chao, hao wote tunataka wafukuzwe, wachunguzwe na kupelekwa mahakamani. Sisemi wachunguzwe ndipo wapelekwe mahakamani ila wafukuzwe na kwisha uchunguzi ufuate. Tumefika mahali mtu akiwa na kashfa apishe uchunguzi sio uchunguzi ndio imuondoe madarakani.

  Mbinu ya pili ya kuondoa ghamba ni kuondoa mfumo unaolea rushwa katika chama hicho. Ni mfumo huu unaolea viongozi wa kisiasa kupatikana kwa njia ya rushwa. Je, mwanasiasa aliyepatikana kwa njia ya rushwa ataacha rushwa? Iwepo mfumo unaofanya viongozi wawe watumishi wa kweli kwa wananchi badala ya kuwa watawala na "watafutaji" kupitia pesa za serikali. Hapa tutataka katiba mpya inayotenganisha mihimili ya serikali na kuweka uwajibikaji na kupeleka pesa nyingi za serikali kwa miradi ya maendeleo badala ya kuyaweka kwenye mifuko ya watu wachache.
  La muhimu kabisa ccm ijivue ghamba kwa kuacha siasa za kupandikiza udini kwa watanzania ili ipate huruma ya kura na uungwaji mkono wa upande mmoja au mwingine wa dini kubwa katika taifa letu. Umoja wa taifa letu ni muhimu sana kulindwa, na kwa kuwa ccm imeanza mbinu ya kuhubiri udini na ukabila ni lazima ijiondoe huko ili iweze kuaminika.

  CCM ikifanya haya ndipo itakuwa inajivua ghamba. CCM itaweza? Ni mtego mkubwa kwa chama hicho manake ukweli ni kuwa HAIWEZI kamwe. Imejifunga minyororo ya rushwa ambayo kuiondoa ni kuiua kabisa chama hicho na kuiondoa katika dola, ife au ijipange upya.

  Wananchi kamwe tusilaghaiwe na haya maigizo. Ukweli ni kuwa CCM imezama katika dimbwi la rushwa, ufisadi na maovu ambayo hakiwezi kujiondoa huko. Kuondoa rushwa manake umeiua ccm. Watanzania tujiandae tu kwa mambo mawili. Moja kutafuta chama mbadala na kukipa masharti yetu. Pili kujiandaa na upinzani mkubwa kutoka kwa CCM ikiwa ni pamoja na kuuawa wenzetu watakaokuwa mstari wa mbele kwenye mapambano na chama hicho. Au Mungu aweke mkono wake wapishe pasipo kumwaga damu. Haya lazima yatakuja miaka michache tu ijayo.
   
Loading...