CCM ishtakiwe kwa nchi wahisani kwa kuendeleza utemi badala ya demokrasia


M

Membensamba

Senior Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
157
Likes
0
Points
33
M

Membensamba

Senior Member
Joined Nov 4, 2010
157 0 33
Ulimwenguni sasa hivi nchi zinazofadhili mataifa ya ulimwengu wa tatu sehemu ya bajeti na misaada mbalimbali zinafanya hivyo kwa msharti ya nchi husika kuendesha siasa za vyama vingi. Hii ni kwa lengo la kuhakikisha kuwa kuna demokrasia ya kweli na utawala bora kwenye nchi hizo. Kwa maneno mengine watu hawa hawako tayari kumwaga fedha zao kwa madikteta na mafisadi. Tanzania ni moja ya nchi zinazopata misaada toka nchi wahisani kwa masharti hayo. Hata kuanza mfumo wa vyama vingi hapa tz ilikuwa ni shinikizo la hawa wababe wa kiuchumi duniani. Sio tu ushauri wa hayati mzee kifimbo kama wengi wanavyodhani.

Ukaidi wa serikali ya ccm wa kubadili katiba ili iendane na mfumo wa vyama vingi, na itoe haki wa vyama shiriki vyote, na kuunda tume huru ya uchaguzi ni ushahidi kuwa serikali ya ccm haikuwa na hata sasa haiko tayari kwa mfumo wa vyama vingi. Hi geresha tu kudanganya wahisani kuwa nasi tuna demokrasia ya vyama vingi. ccm ni chama cha kitemi. Kinapenda kutawala milele, na hata viongozi wake wanachofanya ni kurithisha watoto wao nchi mithili ya watemi wa kale. Kama unabisha, chunguza ni watoto wangapi wa vigogo walio kwenye siasa sasa hivi, tena wanaoandaliwa kwa nafadi kubwa baadaye. Watanzania hawajashtuka tu, lakini ccm ni mkoloni mpya. Hakikuanza hivi, kilianza kama chama makini cha wakulima na wafanyakazi, lakini with time kilibadilika. Sasa hivi imani ya ccm, na miiko yake imebaki kwenye kitabu, sio mioyoni mwa wanachama. Sasa sio tena chama cha wakulima na wafanyakazi, ila kwa kweli ni chama cha mafisadi.

Katika hali hii mazungumzo pekee nao ya kubadilisha katiba yatachukua muda mrefu mno. Ipo haja vyama vya siasa na wanaharakati kuwajuza wahisani hii janja ya ccm, ili nao waishinikize wakubali demokrasia ya kweli. Vinginevyo wimbo wa mabadiliko unaweza kuimbwa mpaka kizazi cha tatu na cha nne kutoka sasa bila mafanikio. Kama mnadhani iko njia bora zaidi karibuni wanjf, nijuzeni.
 

Forum statistics

Threads 1,236,304
Members 475,050
Posts 29,253,402