...CCM is stabilising, CHADEMA is shrinking and CUF is disappearing!

Tatizo kubwa la Dr. Kitila Mkumbo ni kuwa mkweli na fikra zake kuvuka kiwango cha viongozi wake wa chama, ambao hawataki kukosolewa wala kuhojiwa.

Bahati mbaya ulikuwa umepanda jahazi moja na wenzako lakini ulikuwa haujuhi safari inaishia kisiwa gani umekuja kujua jahazi limeishapigwa na dharuba.

Nakupongeza kwa kukusimamia kile unachokiamini mpaka dakika ya mwisho.
 
Great analysis from the great doctor.
If I were to advise you sir,
I would tell you not to involve in active politics,but rather concentrate in analysis and objections.
Kudos!!
 
Kwanza heshima mbele mkuu wangu.

First, voters are clearly tired of CCM and would surely want to replace it. The problem is that CHADEMA does not seem to be providing a credible alternative. This is mainly because, while CHADEMA has managed to expose the flaws of CCM, it has miserably failed to show that it can be a credible alternative. It is one thing to tell people that the road you are following is bumpy; it is completely another thing to show an alternative route to the bumpy road. It is not that CHADEMA does not have good policies. No. The CHADEMA 2010 manifesto came up with some of the best policies this country has ever produced. The trouble is that CHADEMA leaders are simply note interested in articulating their policy positions and pragmatic approaches to the problems confronting the country.

Mwalimu sidhani hayo maneno niliyo highlight kama yana ukweli na sijui umetumia kipimo kipi kutoa hii conclusion! Itakuwa vyema kama utafafanua zaidi maana hiyo Manifesto ina mkono wako kwa asilimia 100.Labda kujifagilia?

CHADEMA leaders have become so obsessed with digging poles into CCM policies and deeds and at throwing sound bites without substance. Consequently, the audiences truly find a lot of fun in what CHADEMA leaders would say, but nothing more than the fun that it comes with sound bites. Back home at a reflection table voters would find nothing tangible from what they were told at a public rally that can address their basic problems now and in future. The final conclusion: no alternative route and therefore I should continue with my bumpy road until a new road is found.

Doh! Nazidi kupata shida zaidi labda ubovu wangu ktk lugha hii inachangia, Labda ungetaja baadhi ya hayo madai yasiyo na mashiko ili tuone kweli ilikuwa upuuzi wananchi kuandamana badala ya kuongea kwa ujumla!

Nadhani binafsi tatizo si madai au kashfa zinazotolewa na Chadema kutokuwa na mashiko bali binafsi tatizo ninaloliona ni kushindwa kuchukua hatua za msingi baada ya kulalamika then issue inakwisha kimya kimya lakini si kwa Chadema kushindwa kuadress basic problems za wananchi bali kuadress solution za matatizo wanayowaeleza wananchi kila siku.

Kuna vitu vingi pia nakubaliana na wewe katika hoja yako namba 2 na 3 lakini Mwalimu Kitila pamoja na sasa kulaumu sana uongozi wa Chadema uliopo na binafsi pia nakubali yapo mapungufu ya kufanyia kazi kuelekea ukombozi wa kweli lakini siasa za Tanzania kwa Chama kilichoongoza ukombozi wa nchi nyingi Afrika kuliko chama chochote Afrika na chenye mizizi ya kila aina kwenye dola na vyama marafiki ambavyo bado vingi vipo madarakani si kazi rahisi kufanya siasa, au kushinda kwa mbinu tu za kuwaambia ukweli wananchi bila kwanza kuwa na sheria zinazoweza kuweka ushindani unaokaribia walau usawa.

Ni rahisi sana kulaumu na kuandika kweli lakini wewe ni shahidi maana kuna chaguzi ulisimamia mwenyewe na bado ukashindwa na kutoa malalamiko haya haya unayolaumu wenzako.
 
Mwalimu sidhani hayo maneno niliyo highlight kama yana ukweli na sijui umetumia kipimo kipi kutoa hii conclusion! Itakuwa vyema kama utafafanua zaidi maana hiyo Manifesto ina mkono wako kwa asilimia 100.Labda kujifagilia?

Mkuu MTAZAMO, usishangae anaposifia hiyo manifesto kwani aliitayarisha yeye mwenenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma habari nzima na kuielewa.Kwa haraka haraka unaweza kuona vigezo alivyotumia kuonyesha alichokisema ni vizuri sana!!

Well, data zake zimelenga kujenga hoja kuwa kuna tatizo katika uongozi kwa kushindwa chaguzi ili kujaribu kuuosha waraka na kuuwekea thamani.

Kitila ameshindwa kueleza hata kwa mstari mmoja ni kwanini na vipi watu wajiandikishe zaidi ya asilimia 80 na wapige kura chini ya 40%.
Hiki ni kigezo muhimu sana kuliko kuangalia outcome ya namba (19,000 CCM, 12,000 CDM)

Pili, ningependa nimsikie endapo anaridhika na mazingira ya kampeni na upigaji wa kura kiasi cha kuhalalisha namba zake kwa uthabiti kabisa.

Tatu, kusinyaa (shrink) hakuwezi kuwa kwa kupoteza kiti cha udiwani au Ubunge.
Katika mkoa wenye chaguzi 3 za udiwani, chama A kikapoteza chaguzi zote ni ngumu kusema kina sinyaa. Lazima tuangalie na idadi ya wapiga kura na factor nyingine.

Mfano, chama A kimepoteza chaguzi 3 mwaka 2014 kwa idadi ya 1000:800 in favor of B.
Mwaka 2011 chama A kilipoteza chaguzi hizo 3 kwa idadi ya 1000:100 in favor of B
Hapa kuna justification yoyote kuwa chama A kinasinyaa?

Nne, je Kitila haoni mgogoro waliouzusha umechangia sana katika 'shrinking ya chama'
Wakati wa chaguzi CDM ilikuwa inarushiana makombora ya matusi, wakati wa uchaguzi Kitila alikuwa busy akiandika mbadala wa vyama. Hivi hiyo haiwezi kuchangia kusinyaa kwa chama

Na mwisho, matatizo ndani ya CDM tumeyazungumza siku nyingi na hata kusema mambo mengi yapo katika template ya kiCCM. Tatizo la uongozi si la jana ni la muda mrefu, je alipoona hasikilizwi ndani kwanini hakujiuzulu kama njia ya ku draw attention akabaki mwanachama?
 
Nne, je Kitila haoni mgogoro waliouzusha umechangia sana katika 'shrinking ya chama'
Wakati wa chaguzi CDM ilikuwa inarushiana makombora ya matusi, wakati wa uchaguzi Kitila alikuwa busy akiandika mbadala wa vyama.

Hapana sioni hivyo. Mwanasheria Mkuu wa Chama alishauri, na akakubaliwa na vikao husika, kwamba sisi tukifukuzwa chama kitaimarika mara kumi. Chama kimeimarika mara kumi kwa sasa.
 
Kitila Mkumbo,

..nadhani ktk uchaguzi mdogo wa Busanda CDM walifuata campaign script uliyopendekeza hapa. pia kama sijakosea Zitto Kabwe featured very prominently ktk zile kampeni. Sote tunajua matokeo kule Busanda yalikuwa namna gani.

..binafsi nadhani formula ya ushindi iko in between hoja zako na hoja za wanaokupinga. sidhani kama CDM wako completely off the mark. kama wanaweza kujaza watu kwenye mikutano that is a good thing na juhudi na mbinu hizo lazima ziwe appreciated. Pamoja ni muhimu kutambua kwamba kazi kubwa zaidi ni kuwashawishi hao wanaohudhuria mikutano kwenda kukipigia kura chama.

cc Nguruvi3, Tumaini Makene, MTAZAMO
 
Mkuu ndio maana nimesema kuna upungufu wa analysis na data ima kwa bahati mbaya, kutoelewa au makusudi katika kupotosha. Nitafafanua.

Kitila anasema ukuaji wa chama hauakisi hamasa iliyopo mitaani.
Anakubali kuwa katika mikutano hamasa na mahudhurio ni mzauri sana ikiwemo watu kujitoa.

Ukuaji kwa upande wake ni idadi ya wabunge na madiwani ambayo nakubaliana naye kwa kiasi fulani kwa hilo ingawa si jumla ya maan ya ukuaji.

Halafu anakuja na conclusion kuwa CCM ilipata kura 19,000 na CDM 12,000 katika uchaguzi A, B or C.Ana link outcome na raw data then conclusion.

Inatakiwa atueleze pia wapi kuna broken link na kwasababu zipi.
Mfano, Mikutano, hamasa, uandikishaji,mazingira ya kupiga kampen, kujitokeza kupiga kura, kupiga kura, kuhesabu kura na mwisho namba na conclusion.

Kuna factors nyingi sana zinazoweza kuonyesha tatizo na siyo rahisi tu kusema watu 1000 vs 500 kwahiyo CDM inasinyaa!

Kwa mtazamo na maoni yangu analysis ya Dr ilishakuwa na conlcusion halafu zikatafutwa data.
Vinginevyo all broken links zingekuwa highlighted au kugusiwa.
 
Kitila Mkumbo,

..nadhani ktk uchaguzi mdogo wa Busanda CDM walifuata campaign script uliyopendekeza hapa. pia kama sijakosea Zitto Kabwe featured very prominently ktk zile kampeni. Sote tunajua matokeo kule Busanda yalikuwa namna gani.

..binafsi nadhani formula ya ushindi iko in between hoja zako na hoja za wanaokupinga. sidhani kama CDM wako completely off the mark. kama wanaweza kujaza watu kwenye mikutano that is a good thing na juhudi na mbinu hizo lazima ziwe appreciated. Pamoja ni muhimu kutambua kwamba kazi kubwa zaidi ni kuwashawishi hao wanaohudhuria mikutano kwenda kukipigia kura chama.

cc Nguruvi3, Tumaini Makene, MTAZAMO
Swala kubwa hapa ni kwa nini Chadema najaza watu ktk mikutano yake lakini inapofikia upigaji kura wengi hawatokei?
Kwa umaarufu wa majukwaani walofikia Chadema sii chama kushinda kata 5 kati ya 27 sijui 29. Something is very wrong, yawezekana kuwa watu wanakipenda chama hiki kwa kuvutiwa na vuvuzela, vioja na mbwembwe majukwaani kama za msanii Diamond!!!

na msikate kuwa chaguzi hizi ndio kipimo halisi cha mafanikio ya chama. Kuendelea kuamini kinyume ni upofu mwingineo ambao pengine ndio unatulemaza!
 
Mkandara,

..swali ulilouliza ni la msingi kabisa linalohitaji majibu yanayotokana na uchunguzi wa kina.

..watu wengi sana wamejiandikisha kupiga kura lakini unapofanyika uchaguzi hawatumii haki yao hiyo.

..umati unaotokea ktk mikutano ya CDM na mapokezi wanayotokea hauendani na kura wanazopata CDM siku za uchaguzi.

..inawezekana tatizo liko ktk ujumbe unaowasilishwa na CDM kwa wananchi, au njia wanazotumia CDM kuwasilisha ujumbe huo, au watu wanaotumwa na CDM kuzungumza na wananchi.

..kwanini CDM wana guarantee ya kushinda uchaguzi Arusha mjini lakini wanashindwa ktk jiji la Dsm? Tatizo ni ujumbe, style ya kufikisha ujumbe, au messengers wa ujumbe huo?

MWISHO:

..kuna maeneo ambapo idadi ya watu ambao wamejiandikisha lakini hawakupiga kura ni kubwa kulinganisha na tofauti ya idadi za kura baina ya mgombea wa CDM ambaye ameshindwa na yule wa CCM. vilevile CCM imekuwepo madarakani kwa miongo kibao na imeshindwa kuboresha hali za maisha za wananchi.

..vigezo hivyo hapo juu ndivyo vinavyonitia "upofu" niamini kwamba CDM hawapaswi kukata tamaa bali wanapaswa ku-regroup, ku-finesse their message,na kutafuta wajumbe wazuri zaidi kuwashawishi wananchi kuwapigia kura.

Kitila Mkumbo, Tumaini Makene, Nguruvi3
 
Kitila Mkumbo, Tumaini Makene
Mkuu JokaKuu , nashukuru umeenda mbali na kutanua mjadala zaidi.

Ndugu yangu Mkandara anasema something is wrong, ni kweli labda niongezee kwa sisi wenye mitazamo huru 'something very wrong'.

Nisipokubaliana na Makndara ni anaposema uchaguzi ni kigezo cha ustawi wa chama cha siasa. Mimi nasema ni zaidi ya uchaguzi, ni pamoja na kuangalia stability ya chama kama institution, kina progress gani katika kjitanua na kinavuna nini katika matanuzi hayo.

Ukimsoma Kitila na Mkandara tayari wana conclusion wanayoijua wao. Mimi nasema hapana huko ni ku mislead public, ni lazma conclusion itokane na data zilizopo na siyo zinazochaguliwa.

Wote kwa pamoja wanakubali kuwa katika uhamasiahaji CDM wamefanikiwa na kampeni zao zinaonyesha mafanikio kinyume na matokeo.

Nimeenda mbali na kusema kama watu wanakubaliana hayo waende mbali zaidi na kujiuliza wakati wa kupiga kura watu wanakwenda wapi? Haiwezekani watu wahudhurie mikutano tena mvua zikinyesha halafu washindwe kupiga kura kwa dakika chache?

Swali hilo CCM hawana jibu ingawa hawaonekani kusononeka, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi hana jibu ingawa anapaswa kuwa nalo.
CDM hawana jibu ingawa wanahitaji jibu zaidi kuliko CCM na NEC ya uchaguzi.

JokaKuu kaja na hoja nyingine, hivi iweje Arusha, Mwanza na Mbeya CDM waweze kudhibiti masanduku ya kura lakini Dar isiwezekane?

Je CDM wana right message, wana right people katika maeneo wanayosimamisha wagombea.

Ukiangalia kwa ufupi kuna sababu aina mbili
1. Internal, ambazo tunajua ni weakness ya taasisi, Kuna resentment n.k.
Unaweza kuona Busanda uchaguzi lifanyika kwa 'template' ya Kitila na matokeo hayakuwa tofauti na kwingine. Miezi 18 tunafahamu kuwa ndani ya CDM kulikuwa kuna kung'ongana.

2. External ambazo CDM wanapaswa kuzifanyia kazi. kwanini watu hawapigi kura. Fungu kubwa sana la CCM linatumikaje na kwa njia zipi. Kura zinalindwa vipi, kuna Mamluki n.k.

Hoja yangu ni kuwa hili si suala la kutafuta mchawi tena baada ya 'kifo cha mgonjwa'.
Kwakuwa Nguruvi alimwambia Mkandara 'utaona' basi kila linalomsibu Mkandara hakuna anayeangalia pembeni, wote wanasema 'alisema utaona' hata kama ni malaria au minyoo!

Hili suala linahitaji scientific approach siyo resentment and pre arranged conclusion.
Halihitaji 'plug in data' to justify sababu zozote.

Mkuu jambo moja tu ni kwamba sijafikia conclusion yangu pasipo kutazama takwimu kwanza. haiwezekani kabisa chama kama CDM kinavyopendwa na wananchi ati waje ktk mikutano yao kwa maelfu halafu siku ya uchaguzi wasitokee!.

Na haiwezekani kabisa kusema ati hawakujiandikisha kupiga kura maana umaarufu wa Chadema hauanza leo bali toka 2010 na wale walokuwa miaka 15 leo ni wakubwa wa kupiga kura. Haya walojiandikisha tu mwaka 2010 ni vijana wengi kwa mvuto wa Dr.Slaa ambao nina hakika CDM ingepata hata 1/3 ya majimbo yote uchaguzi huu.

Maadam CDM imeshinda majimbo 3 sijui kata 5 tu kati ya 27 hapa lazima kuna makosa makubwa sana yanafanyika ama wananchi hawana imani na viongozi wanaowekwa kugombea maana Tanzania siasa yetu hutazama mgombea zaidi ya chama.
 
Mkuu ndio maana nasema ninyi wenzetu mna jambo! Mkuu tunaposema kujiandikisha hatuna maana kujiandikisha kwa watu wa Chadema. Tunazungumzia kujiandikisha kwa wapiga kura.

Swali ni kuhusu kujiandikisha wapiga kura bila kujali ni wa chama gani. Jibu la swali hilo wanalo NEC ingawa wanasema hawajui. Kusema hawajui ni kukwepa ukweli kuwa kuna tatizo mahali.

Hivyo mkuu siyo suala la mikutano ni suala la waliojiandikisha wawe CUF/CCM au CDM kwanini hawajitokezi.
Ukiangalia suala ninalozungumzia bila prejudice utaona mantiki. Ukiangalia kwa mtazamo wa CDM utapata majibu tofauti.

Tusijaribu ku plug in data au scenario, tuangalie mambo kwa upana wake.
 
1. Mimi kwanza ningependekeza Tume ya uchaguzi iwe inaboresha daftari la kudumu la wapiga kura walau mara moja katika kila robo ya mwaka kwa maana ya mara moja kila baada ya miezi mitatu na hili ningeomba watakaotuwakilisha katika utungaji wa katiba mpya wasilisahau.
2. Polisi na kutokuboreshwa kwa daftari la wapiga kura mimi sio kama ndo sababu kuu kwa CDM kufanya vibaya katika Chaguzi hizi zilizopita bado kuna kasoro nyingi ndani ya CDM ambazo zinaweza zikawa zinachangia kufanya vibaya kwa CDM kwa mfano; katika chaguzi nyingi tumeshudia watu wengi wanaotruliwa kuendesha kampeni ni watu kutoka makao makuu au wabunge na hata Operation zote. imekuwa ni lazima ziendeshwe na watu kutoka makao makuu au wabunge sasa unajiuliza uko wapi umhimu wa kuunda kanda ikiwa shughuli zote zinafanywa na watu toka makao makuu? kwa mfano ukienda kwenye wilaya nyingi wenyeviti na makatibu wengi wao hata hawafahamiki na hata wakiitisha mikutano watu huwa hawana hamasa sana hadi wasikie amekuja Mbowe au Slaa ndo utaona watu wamejaa
Mimi niwashauri tu CDM wawawezeshe hawa watendaji wa Chama kuanzia ngaji ya kanda, mkoa, na wilaya ili waweze kujitegemea makao wabaki kuwasimamia tu waache huu mtindo wa kila Operation lazima iendeshwe na watu wa makao makuu
 
Mkuu ndio maana nasema ninyi wenzetu mna jambo! Mkuu tunaposema kujiandikisha hatuna maana kujiandikisha kwa watu wa Chadema. Tunazungumzia kujiandikisha kwa wapiga kura.

Swali ni kuhusu kujiandikisha wapiga kura bila kujali ni wa chama gani. Jibu la swali hilo wanalo NEC ingawa wanasema hawajui. Kusema hawajui ni kukwepa ukweli kuwa kuna tatizo mahali.

Hivyo mkuu siyo suala la mikutano ni suala la waliojiandikisha wawe CUF/CCM au CDM kwanini hawajitokezi.
Ukiangalia suala ninalozungumzia bila prejudice utaona mantiki. Ukiangalia kwa mtazamo wa CDM utapata majibu tofauti.

Tusijaribu ku plug in data au scenario, tuangalie mambo kwa upana wake.
Ebu subiri kwanza fafanua hili maana sijakuelewa!
Unachotaka mimi niamini ni kwamba watu wanaohudhuria mikutano ya Chadema ni wanachama wa Chadema? au wale wanaohudhuria mikutano ya CCM ni wanachama wa CCM?.

Swala la Daftari la wapiga kura halina chama wala wanachama ila wananchi wenye uwezo wa kupiga kura na NEC hawawezi kujua kila mtu alojiandikisha ni chama gani. Tusichanganye vitu hapa, kupendwa kwa Chadema haina maana ni uanachama bali kukubaliana na sera zao hivyo uko tayari kuwapa kura yako hata kama wewe sii mwanachama.

Vijana wengi wameonyesha upendo mkubwa sana na wanakikubali chama hiki cha Chadema inakuwaje wakati wa uchaguzi hawaonekani wakati mapenzi yao yalikuwepo kabla ya uandikishaji wa mwaka 2010.
 
Mkuu mbona tupo page moja!!

Nimesema suala la kujiandikisha na kupiga kura halijalishi chama. NEC inatakiwa ilifanyie kazi kupata jibu. Hatuwezi kupa jibu kwasababu NEC ya uchaguzi na NEC ya CCM hazitofautiani sana

Nisichokubaliana na hoja yako ni pale unaposema wasiojitokeza ni wafuasi wa CDM.
Pengine kundi hilo linaweza kuwa na athari kwa CDM kwa namna fulani hasa ikizingatiwa CCM hawana tatizo nalo lakini si tatizo la CDM pekee.
Ni jambo linalohitaji majibu mazito na ndio maana Kitila hakuliongelea.

Kwa kutoliongelea ni sawa na kunyofoa kiungo kimoja muhimu sana katika puzzle.
Tunaambiwa puzzle haina tatizo tatizo ni viongozi, well hiyo siyo sababu pekee ni moja ya sababu.

Si sahihi kuja na takwimu 19,000, 12,000 na 1000 kutoka 32,000 waliopiga kura na si 70,000 waliojiandikisha.

Then kukawa na conclusion kuwa tatizo lipo sehemu fulani na kufumbia macho tukio zima la kuhamasisha, kuhudhuria mikutano, kujiandikisha, kupiga kura, kuhesabu kura na matokeo.

Ndio maana nasema baadhi yetu humu tuna conclusion kinachofanyika ni ku plug in data
 
Sidhani kama tupo ukurasa mmoja ktk hili maanake tunajua wazi kwamba wananchi sasa hivi wamekuwa na mwanga mkubwa kisiasa zaidi ya mika ilopita na haiwezekani asilimia ikaendelea kupungua. hata kama wamejiandikisha 19,000 na wakapiga kura 12,000 bado hiyo 12,000 ni kubwa kuliko ile ya uchaguzi ulopita. Kila mkoa daftari la wapiga kura limeongezeka mwaka 2010 na vile vile hesabu ya wapiga kura japo haikuwa sawa na walojiandikisha, iweje ushindi wa CDM uwe wa kusua sua pengine kuporomoka!

Mimi sipendi kabisa sababu za kubuni ama kutafuta mchawi isipokuwa matokeo yanatupa picha halisi kwa sababu nilipojiandikisha mimi upigaji kura sikwenda na sura wala gwanda la Chadema la wala waandikishaji hawawezi kujua mimi nitakipigia kura chama gani acha hao NEC.

Na katika kundi la watu iwe 19,00o au 70,000 swala ni asilimia ngapi ya ushindi inaweza tu kutumika kama kipimo cha mafanikio. Ikiwa mwaka 2005 tulikuwa na asilimia 10 kwa wapiga kura 10,0000 kisha mwaka ulofuata tukawa na asimilia 12 kwa wapiga kura 12,00 japo walojiandikisha ni asilimia 30 zaidi inaashiria tu kwamba wananchi ambao hawakupiga kura hawakuridhika na siasa za vyama vyote.

Wewe kama rais lazima ujue kwa nini huendi kupiga kura japo umejiandikisha na sababu hizo zitumike ktk kufikiri kwetu. Na haihitaji elimu kubwa sana kufanya maamuzi ya upigaji kura. Msomi anaweza kutokwenda kupiga kura na yule mbumbumbu ndiye akajitokeza ni swala la wananchi kuyataka mabadiliko. Hivyo napoona mikutano ya Chadema watu wakidai mabadiliko kisha wasijitokeze ktk Uchaguzi inaashiria wazi kwamba hawana imani na vyama iwe CCM ama Chadema na hivyo basi Chadema inacho gain ni ushabiki kama mwana Arsenal au ManU aliyeko Tanzania.

Hili ni tatizo kubwa kwa chama na inabid walifanyie utafiti mkubwa na wazi kutambua kwa nini wananchi walojiandikisha kupiga kura toka mwaka 2010 wameshindwa kujitokeza tena mwaka huu ilihali ktk mikutano na mihadhara ya vyama hawakosekani. Chadema itaweza tu kushinda kupitia sanduku la Kura na kama kweli NEC inahusika sana inakuwaje ktk majibmo mengine Chadema imeweza kufanya vizuri hasa ktk mikoa ya Arusha, Mwanza, Mbeya na Mara ambao sote tunaelewa serikali ya JK na CCM kwa ujumla wanaitaka mikoa hiyo sana. Huu ushindi umewezekana vipi ishindikane sehemu nyinginezo!

Halafu utasikia hao hao viongoz wa Chadema wakisema na kutoa kashfa kwa mikoa ambayo hawakushinda ya kwamba wananchi wake bado wamelala, ni wajinga na pengine vyakula wanavyokula ndio sababu upofu wa bongo zao badala ya kutafuta haswa sababu zilizopelekea kushindwa ktk majimbo hayo!
 
Mkuu Mkandara
Mimi naliangalia tatizo kama la nchi hata kama linaweza kuwa na mkono wa sehemu ya jamii.
Wewe unaliangalia tatizo kama la CDM katika ku justify kile unachokiona si sawa. Hapa ndipo tunaachana.

Sikubaliani na kungalia namba za mwisho bila kujua zimepatikana kwa njia gani.

Haiwezkani watu wajiandikishe 100,000 halafu wapige kura 25,000 tuseme kuwa 3/4 hawakuridhika na siasa za vyama.Na wala hatuwezi kuhalalisha ushindi huo kama parameter ya kukua au kudumaa kwa chama.

Ni kwasababu rahisi kama hizo, CCM iliondoa ushindi wa 50% na kuwa na simple majority kwamba kiongozi wa jimbo anaweza kuchaguliwa na watu 2,000 kati ya 100,000.
Hapa Mkandara ataniambia kama wameshinda CDM ni ishara ya kukua chama au CCM itakuwa ni kuimarika. Tunaangalia namba za mwisho ambazo ni 1500 vs 500 na kusema CDM wanaimarika

Kuna kitu kinaitwa 'voters suppression' ambacho kina namna nyingi sana za kutekeleza.
Kwa mfano, bomu la mkutano wa Arusha lililenga kujenga hofu miongoni mwa mambo mengine. Turn out ya voters ikawa ndogo na kuacha vyama vikipigiwa kura na political base' na si wananchi

Uchaguzi wa Mbeya vijijini ilidhihirika kulikuwa na ununuzi wa kura na hivyo kujiandikisha hakukuwa na maana kwasababu waliotakiwa kupiga kura hawakupiga.
Hii ni sehemu ya suppression ya voters.

Mikoa uliyosema ukiiangalia ni ile iliyokubali mabadiliko kwamba watakula pesa au kutoa taarifa za hujuma.Ndivyo EL alivyoshindwa Arumeru licha ya kumwaga pesa za kutosha.
Ndivyo mwanza na Mbeya wafanyavyo.

Sina sababu za kutetea matokeo mabaya ya CDM, nisichokubaliana nacho ni kutafuta namba kuzipika na kuja na conlcusion bila kufuata taratibu.

Takwimu za Kitila kwa mtu wa kawaida zina make sense sana, kwa mtu anayeangalia vitu kutoka angle tofauti takwimu zinaeleza jambo moja kwamba zimetafutwa ili ku justify theory iliyokuwepo.

Ubovu wa CDM mbona tumeshauongelea sana. Hata hili la wapiga kura wachache tumeshawaeleza siku nyingi kuwa lazima wawe na daftari lao la wapiga kura wao kwanza.

Leo wangekuwa na mahali pa kuanzia kusema kama zipo hujuma au la.
Leo wangeweza kuunga mkono hoja ya Kitila au kuipinga kwa takwimu.
Kwasababu hawana utaratibu huo hii imebaki kuwa open kwa kila mmoja kuamini atakavyo.

Kuna ubovu sehemu kubwa tu hata katika mikuatano.
Hakuna anayefuatilia kuona impact yake na nini kifanyike baadaye.
Kuna madhaifu ya kutotambua potential candidates katika maeneo wanayosimamisha wagombea.

Yote yanaweza kuchangia kwa namna moja au nyingine, na kama kuna ushauri ni wao kukaa na kuangalia wapi kuna tatizo na walifanyie nini.

Hata hivyo hawapaswi kuongozwa na takwimu zitakazowaondoa mbali na ukweli wanaoutafuta.
 
Back
Top Bottom