CCM Irudishe Hela Iliyokusanya kutoka kwa Wanafunzi kwa Kutumia TCU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Irudishe Hela Iliyokusanya kutoka kwa Wanafunzi kwa Kutumia TCU

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by NguchiroTheElde, Oct 3, 2010.

 1. N

  NguchiroTheElde Member

  #1
  Oct 3, 2010
  Joined: Jun 13, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM Irudishe Hela Iliyokusanya kutoka kwa Wanafunzi kwa Kutumia TCU

  Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu jinsi TCU ilivyokusanya mabilioni ya fedha kutoka kwa wanafunzi na madai kuwa fedha hizo zimeenda kugharamia kampeni za uchaguzi za CCM kinyume na sheria. Utumiaji wa TCU kunyanganya vyuo vikuu na wanafunzi hela kwa ajili ya CCM siyo tu ni kinyume na sheria bali pia ni kinyume kabisa na hali na hadhi ya Usomi wa kiwango cha juu pamoja na hali na hadhi ya Vyuo Vikuu ambavyo ndivyo vinavyotoa huo Usomi wa kiwango cha juu.
  Ili kurudisha heshima ya elimu ya juu na heshima ya vyuo vinavyotoa hiyo elimu ya juu pamoja na heshima ya Tume ya Vyuo Vikuu – TCU – jambo la kwanza kabisa inabidi CCM irudishe fedha za wanafunzi ilizochukua kupitia TCU; na TCU kwa upande wake kama Taasisi ya Uma iweke hadharani mahesabu yake kuhusu idadi ya wanafunzi wlioomba kwenda Vyuo Vikuu kupitia TCU, hela ilizokusanya kutoka kwa wanafunzi, matumizi ya hela hizo kwa mchanganuo wa kuridhisha na balansi iliyoko mikononi mwao kwa wakati huo.
  Hela yote iliyokwenda CCM na nyingine yoyote iliyotumiwa vibaya irudi TCU na kisha igawiwe vyuo vikuu vilivyohusika kwenye mpango huu kwa kutumia reshio ya idadi ya wanafunzi waliopokelewa katika kila chuo. Ni muhimu hela hizo zirudi vyuoni kwani TCU haina haki na hela hiyo kabisa. Hawakufanya lolote la kustahili hizo hela na ni wazi kuwa hawakupata ridhaa ya wahusika. TCU iliwanyanganya hela hizo kwa kazi ya kuvuruga mfumo wa kupokea wanafunzi vyuoni unaotumika dunia nzima na uliozoeleka hapa nchini tangu Mtanzania wa kwanza kupokelewa Chuo Kikuu hadi mwaka huu wa 2010. TCU ilichofanya hawastahili kupewa hata senti moja ya hela hizo na kinyume chake wangeshtakiwa kwa uporaji wa majukumu na hela za watu na taasisi kinyume na sheria.
   
Loading...