CCM iringa kufuka moshi ,wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM watofautiana juu ya katibu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM iringa kufuka moshi ,wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM watofautiana juu ya katibu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nsaji Mpoki, Feb 16, 2012.

 1. N

  Nsaji Mpoki JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 396
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  February 15, 2012

  CCM IRINGA KUFUKA MOSHI ,WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM WATOFAUTIANA JUU YA KATIBU


  [​IMG]
  Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bi.Mary Tesha


  Wakati kesho chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kinakusudia kufanya mkutano wake wa Halmashauri kuu ya mkoa ,wajumbe wa mkutano huo wameonyesha kutofautiana na katibu wa CCM mkoa Bi.Mary Tesha na kupanga kutumia mkutano huo kumweka kitimoto ama kumkataa .

  Mtandao huu (Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima) umedokezwa kuwa moja kati ya vikwazo vya CCM kuendelea kukataliwa na wananchi mkoani hapo ni kutokana na katibu huyo kufanya kazi kivyake vyake na kutowajali watendaji wengine.

  Wadai kuwa hata wafanyabiashara na wadau mbali mbali waliokuwa wakichangia chama kwa sasa toka afike katibu huyo wameanza kurudi nyuma na kuwa zipo dalili za CCM mkoa wa Iringa kushindwa vibaya katika chaguzi kutokana na katibu huyo kujijali yeye zaidi kuliko chama na kuomba CCM Taifa kujaribu kufuatilia utendaji kazi wa katibu huyo wa mkoa ambaye wamemfananisha na mfanyabiashara


  Katika pita pita kwenye blogs nimekutana na hili. Swali hivi CCM kuna nini?
   
Loading...