CCM ipo sana na inayo watu, wapinzani waibeze kwa hatari yao wenyewe

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,471
46,002
Wiki hizi mbili status yangu WhatsApp imejazwa na posti za jumbe za heri kwa wafanyakazi, ndugu jamaa na marafiki wakiwatakia heri watu wao wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM.
Wengine hata sio watu wa siasa kabisa.

Katika mitandao nimeona hadi viongozi wa vyama vya upinzani kama ACT wakiwatakia heri 'watu wao' wanaogembea uongozi ndani ya CCM

Nimeona wafanyabiashara, wasomi, wasiosoma, wanaharakati, wazee kwa vijana wengi na wengine waliotimuka kutoka vyama vya upinzani kama CHADEMA wakigombea nafasi za uongozi ndani ya CCM.

Kuna namna CCM imejifungamanisha na maisha ya raia wengi wa nchi hii, wa kada zote, wa rika zote, wa pande zote, wa dini zote, wa Simba na Yanga na wa kabila zote kama vile samaki na maji. Wanaogelea humo, wanapata oksijeni humo, wanapata chakula humo. Katika mazingira upinzani ni kama nchi kavu katika, hauyumukiniki kwa wala hata haufikiriki kwa wengi.
Kazi ipo.
 
Naona watu wengi zaidi wa upinzani wakitimkia CCM kuliko kinyume chako!
 
Kuwatakia heri hao wagombea wa CCM pekee hakitoshi kuwa kigezo kwako kuamini CCM inakubalika kwa makundi tofauti ya watu..

Kuna sababu nyingi zinazofanya iwe hivyo; urafiki, uoga [kujipendekeza], au nia njema tu ya kuwatakia heri wagombea hao.

Lakini kufanya kwao hivyo, hakumaanishi wanaipenda CCM na wako tayari kuichagua, kumbuka kura ni siri, na tumeshaona mara nyingi CCM ikipumulia oxygen ya tume ya uchaguzi, na polisi licha ya hizo salamu za heri wanazotakiwa.
 
Back
Top Bottom