CCM ipo hoi bini tabani vijijini na mijini

kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,395
512
Nimezunguka sana wakati huu waka mpeni sehemu mbalimbali za nchi. Nilicho kundua nikwamba watu wanahitaji mabadiliko.

CCM, kwa mwaka huu, wanaiona ni adui wamaendeleo yao. Kiukweli hali ya maisha ya walio wengi vijijini hata mijini ni tete. Sijui ccm wanajinadi vipi kwa wananchi hawa nilio waona.

Tatizo kubwa kwao ni maji, afya na elimu na kilimo. Ccm imesgindwa kutatua changamoto zilizopo kwenye hizi sekta tajwa.

Kwahio wanasema mabadiliko ni lazima, wanahudhulia mikutano ya ccm angalao wapate hela ya kula, ila kura ni kwa upinza.
Wanadai wana wavaa nguo mpya wakati wa uchaguzi tuu ambazo ni sale za ccm. Wanadai hali hii kwa sasa wameicho, wanahitaji kuona uongozi wa chama kingine.

Kiufu wanasema hawana shida na mgombea wa ccm, ila wa hasira na mfumo ccm na kumchagua magufuli ni kuchagua mfumo uleule.

"Change is what they believe in"
 
Roho inaniuma namna CCM inavyotuchezea na kutudharau sisi walimu wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo tuliowafundisha wao pamoja na jitihada zetu za kuendelea kukarabati kizazi cha Taifa la leo na kesho.

Mazingira ya kufundishia si rafiki kabisa,nyumba za walimu ni utata,likizo kizungumkuti,mishahara kiduchu,usafiri ni majanga,matibabu ni dhahama,Usafiri ni mgogoro, mikopo kuipata ni balaa,kujiendeleza ni mbinde,uhamisho ni soo,huduma ya maji ni hadithi zisizokwisha,umeme ni ahadi juu ya ahadi zingine; maisha ya Mwalimu ni kama maigizo,Maisha ya leo ni afadhali ya jana na juzi. Hatuthaminiwi Wilayani, Halmashauri, Benki,Sehemu za Starehe na hata katika vyombo vya usafiri.

Ukijitambulisha wewe ni Mwalimu basi jiandae kudharaulika. Wanafunzi wanaishia kutupachika majina kutokana sisi kuwafuatilia sana kimaadili na Kitaaluma kiasi kwamba tumechoka kimaisha (Mavazi, Malazi, Chakula na Burudani).Leo CCM imewarubuni baadhi yetu watushawishi kuipa tena kura CCM?

Baada ya kuona imekataliwa na Wakulima,Wafanyabishara,Wavuvi,Manesi,Wanafunzi,Wakandarasi,Madereva,Wamachinga,Wanawake,Wajasiamali ,Wawekezaji,Wachimba madini,bodaboda,mama Ntilie n.k!! LOWASSA OKOA TAIFA KWA KUOKOA WALIMU!!
 
Ndugu Abel Ndundulu hiyo idara uliyoitaja ni kama wote wame rogwa na aliyewaroga kafa. Wao walitakiwa kuwa chachu ya madiliko kwa kila nyanja. Yaani wana watu (wanafunzi), jamii ipo karibu nao yaani wazazi na walezi sasa ukiwaangalia unashindwa kuelewa. Waalimu wanaitaji kukombolewa kifikra, hasa kuhusu hatima ya nchi yetu, ile CWT yao inawakata pesa kama hawana akili nzuri yaani hawa jamaa ni balaa. Waombewe
 
Acha uongo, ndugu zangu wengi uko waliko wamenihakikishia wanaipa kura CCM. Subirini mshangao!!!!
 
Mwalimu Abel maneno yako yamenigusa sana aisee. Katika mazingira hayo unayoyaongelea bado utakuta kuna walimu wakereketwa wa mfumo uliopo. Hapo ndio huwa ninaishwa nguvu na uwezo wa kufikiri wa watu wetu.
 
Sasa ni dhahiri kwamba CCM iko hoi kila kona ya nchi! Mgombea urais wake amebaki kama Mgombea binafsi , CCM wengi waapa kutomuunga mkono. Wadai mabadiliko haikua kauli mbiu ya CCM!
 
Lowasa ndo Rais wetu tushaamua ivo kila kitu kishawekwa Sawa
 
Acha uongo, ndugu zangu wengi uko waliko wamenihakikishia wanaipa kura CCM. Subirini mshangao!!!!

CCM ni zaidi ya UKOMA,wapambe wake ni viongozi wa chama na walionyimwa elimu alafu hawaelewi haki zao ndani ya nchi yao
 
Aichaguaye ccm,anamaanisha kuwa anayo ada ya mwanaye,A level hadi chuo kikuu
 
Sekta ambazo zimeajiri watu wengi CCM wamezidharau sana.
Kinachotokea ni kwamba hao wananchi wameamka.
Hawawataki tena.
 
Back
Top Bottom