CCM inazidi kupoteza uungwaji mkono sababu ya ugumu wa maisha ya wananchi wengi. Inaniuma sana

CCM Music

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
1,036
1,782
CCM ni kwa ajili ya Wakulima na Wafanyakazi (Jembe na Nyundo). Na haya ndio kiini cha maisha halisi ya watanzania na ndio maana hiki chama nakipenda sana.

Lakini, kwa sasa CCM ni chama cha wafanya biashara wakubwa ama cha wenye hela ama cha wenye connection na wenye hela. Period. Hakuna tena cha Jembe wala cha Nyundo.

Sasa asili ya CCM (Jembe na Nyundo) ipo mashakani kwa kiwango cha kutosha sababu kuu ni ugumu mkubwa wa maisha ya washika jembe na Nyundo (wananchi wa kawaida - Wakulima na Wafanyakazi).

Wakulima - CCM hatuna tena mipango ya kisasa ya kuinua maisha ya wananchi kupitia kilimo.

Wafanyakazi - Hakuna ajira kabisa naweza kusema hivyo. CCM tumeishiwa kabisa mbinu za kisasa za kutengeneza ajira. Kuna kilio kila kona ya nchi.

Kwa nchi yetu ya Tanzania, ukikosa mipango thabiti ya ku deal na kilimo Pamoja na kutengeneza ajira basi ujue nchi hii ipo taabani. Tafsiri yake ni kwamba, itazidi kupoteza uungwaji mkono siku hadi siku.

CCM inahitaji re form ya hali ya juu sana kukabiliana na wimbi la siasa za kisasa ambazo huwezi kuwa na ushawishi kwa kutumia kete ya CCM imelikomboa Taifa toka wakoloni; badala yake ushawishi ipo kwenye kete moja tu ya 'better life'.

Wapinzani kwa ujumla wao nao hawana hoja za maana sana basi tu wanatumia udhaifu wa CCM kupata umaarufu. Mindset nyingi za wapinzani zinashahabiana kwa kiwango kikubwa na CCM. Kwa maneno mengine wapinzani ni wana CCM watukutu; yaani ni kama wale wanafunzi watukutu shuleni wao hupingana na kila kitu.
 
CCM imefeli kwenye angle zote, watanzania kwa wingi wao wanalijua hilo ndio maana hawaitaki tena, na CCM kwa sababu ya tamaa yao ya madaraka wameishia kuiba kura na kupora ushindi wa wapinzani tena bila kificho mpaka kutuambia wazi hata tusipowachagua, wao ndio wataunda serikali.
 
😁😁😁
42_609.jpg
 
CCM imefeli kwenye angle zote, watanzania kwa wingi wao wanalijua hilo ndio maana hawaitaki tena, na CCM kwa sababu ya tamaa yao ya madaraka wameishia kuiba kura na kupora ushindi wa wapinzani tena bila kificho mpaka kutuambia wazi hata tusipowachagua, wao ndio wataunda serikali.
Huu ndio udhaifu tulio nao na wapinzani wanapita mle mle
 
Back
Top Bottom